Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000

Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000

Uwa napenda nikienda bar nibebe cash ,nijaze hela kwenye laini zangu za simu ila niwe na chawa incase of anything nisidharirike japo na miguu yangu uwa iko upande wangu daima ikiwa mambo yataharibika kabisa .
Mimi kanuni yangu bar yoyote ni kutengeneza urafiki na mabaunsa. Nikiingia bar naakikisha angalao mabaunsa watatu nimewatoa 5K kila mmoja. Hapo hata nikianzisha ugomvi mabaunsa wanakua upande wangu
 
kwa wabongo naowajua mimi hapo ukute kilichomkosti huyo marehemu itakuwa ni majibu aliyokuwa anawapa hao wadai wake. utakuta kanywa bierre za kutosha mwenyewe halafu hana hata mia mbovu ya kulipa na bado anatoa kauli mbovu za kibabe. hii nimehisi tu lakin.
 
Mmiliki kapoteza kila kitu hapo, probably wote wataishia jela for life, make sure ukiajiri unatoa mafunzo kwa wafanyakazi wako ili kuzuia disaster kama hizi, ujumbe kwa mabaunsa kazi yenu ni kudhibiti sio kupiga na kuumiza au kuua mtaishia jela na kuharibu maisha yenu
Mmiliki anapotezaje kila kitu! Sheria haihukumu mtu ambaye hakushiriki tukio la uhalifu.

Watakaopoteza kila kitu hapo na ikibidi kuishia jela ni wahusika wote wa hilo tukio. Kama mmiliki alikuwepo eneo la tukio na pia kushiriki mumpiga marehemu; ndiyo nitakubaliana na hoja yako.
 
Majibu ndo tatizo. kuna mtu anadaiwa 300k anaachwa anaondoka, Huyu anadaiwa 8000 kapigwa mpaka kafa.

Ni jinsi unavo ongea na watu.
 
Mmiliki anapotezaje kila kitu! Sheria haihukumu mtu ambaye hakushiriki tukio la uhalifu.

Watakaopoteza kila kitu hapo na ikibidi kuishia jela ni wahusika wote wa hilo tukio. Kama mmiliki alikuwepo eneo la tukio na pia kushiriki mumpiga marehemu; ndiyo nitakubaliana na hoja yako.

Sema bar yake inaweza loose reputation.
 
View attachment 3587608
#HABARI Kijana mmoja mfanyabiashara mkazi wa Mbugani Jijini Mwanza, anayejulikana kwa jina la Mzafaru Yunus (26), amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa kikatili ndani ya Baa iliyopo Kona ya Bwiru, Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, kufuatia kushindwa kulipa bili ya vinywaji yenye thamani ya Sh 8,000.

Tukio hilo limeibua taharuki miongoni mwa wakazi huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likiwashikilia watu tisa wanaodaiwa kuhusika, wakiwemo walinzi wawili maarufu kama mabaunsa.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema marehemu alishambuliwa kwa ngumi, mateke, vipande vya mbao pamoja na bomba la chuma sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza maisha.

Soma Pia: Arusha: Polisi auawa na wananchi akidhaniwa kuwa mwizi, Sita wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Amesema miongoni mwa waliokamatwa ni meneja wa baa hiyo, wafanyakazi wa usafi na walinzi wawili, huku watuhumiwa wengine wakidaiwa kutoroka kabla ya kukamatwa na polisi wanaoendelea na uchunguzi wa tukio hilo. #EastAfricaTV
Mfanya biashara anauawa kisa 8,000 huyo alikuwa mvuta bange tu asie na maisha, hakuna mfanya biashara wa hivyo
 
Mmiliki kapoteza kila kitu hapo, probably wote wataishia jela for life, make sure ukiajiri unatoa mafunzo kwa wafanyakazi wako ili kuzuia disaster kama hizi, ujumbe kwa mabaunsa kazi yenu ni kudhibiti sio kupiga na kuumiza au kuua mtaishia jela na kuharibu maisha yenu

Polisi kitengo cha Elimu kwa jamii kianze kutoa elimu kwa hawa jamaa, Ni darasa la saba hawa nguvu nyingi akili kidogo.
 
Ukisha kosa akili ukawa maskini wa mali na akili.Kupigana huwa kipao mbele cha kwanza kwa wanaume +Wanawake.

Umaskini huzaa tabia nyingi sana za kichawi chawi.Mtu mlevi kuna namna za kudeal nao na akawa mteja mmoja Mkubwa sana.
Tuna wapa kazi vichaa na watu wenye msongo..plus kuna walevi nao wako na msongo basi kila kitu ni hovyo hovyo.
 
Hatari sana, vijana sijui kwanini wana ujasiri wa lwenda sehemu za starehe na hela hawana! Unakutana na kijana ana nguvu kabisa anakuomba bia unabaki unashangaa!
Ko hutaki kuombwa bia weyee?? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mwaka Jana nilisimama hapoo mjini Dodoma nilikuwa naenda Monduli kukamilisha vipengele vya ndoa.Sasa Ile asubuhi kuanzia 11 mpaka 3 na kitu bill inakuja laki sita na ushee .Aisee tulizungukwa na mabaunsa ,wahudumu ,wapishi ,Kwa Yale macho wangetuua washenzi wale.Option ilikuwa imebaki ni kuzinesa tu au kulipa.Aisee.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nawachukia sana hawa mambavu ya mbwa kujifanya kila kitu utadhani maisha wamemaliza,, wakati kazi yao ni ukuwadi kuwakuwadia wahudumu kwa wanaume domo zege,, acha waishie Butimba sasa,,
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom