Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000

Mwanza: Auawa na mabaunsa kisa Tsh 8000

Kesi ya kuua Tanzania inachapwa na zile mashine za typewriter ili maandishi yasifutike leo wala kesho hao mabaunsa mpaka wanahukumiwa watakua na mwili kama Rais wa Rwanda...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Polee yake sana kijana mdogo, kapoteza uhai kwa sababu zisizo za msingi. Lol
 
Mmiliki anapotezaje kila kitu! Sheria haihukumu mtu ambaye hakushiriki tukio la uhalifu.

Watakaopoteza kila kitu hapo na ikibidi kuishia jela ni wahusika wote wa hilo tukio. Kama mmiliki alikuwepo eneo la tukio na pia kushiriki mumpiga marehemu; ndiyo nitakubaliana na hoja yako.
Watu hawanywi au kula sehemu ambazo wanaua watu ( reputation damage) na kwa sheria za bongo unaruhusiwa kushitaki business/owner for any damage or injury , na kwa wafanyakazi wako you are responsible for their actions while on duty, atashitakiwa kwa kilichotokea for big compensation, ila baunsas kesi ya mauaji inawahusu
 
View attachment 3587608
#HABARI Kijana mmoja mfanyabiashara mkazi wa Mbugani Jijini Mwanza, anayejulikana kwa jina la Mzafaru Yunus (26), amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa kikatili ndani ya Baa iliyopo Kona ya Bwiru, Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, kufuatia kushindwa kulipa bili ya vinywaji yenye thamani ya Sh 8,000.

Tukio hilo limeibua taharuki miongoni mwa wakazi huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likiwashikilia watu tisa wanaodaiwa kuhusika, wakiwemo walinzi wawili maarufu kama mabaunsa.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema marehemu alishambuliwa kwa ngumi, mateke, vipande vya mbao pamoja na bomba la chuma sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza maisha.

Soma Pia: Arusha: Polisi auawa na wananchi akidhaniwa kuwa mwizi, Sita wakamatwa kwa tuhuma za mauaji

Amesema miongoni mwa waliokamatwa ni meneja wa baa hiyo, wafanyakazi wa usafi na walinzi wawili, huku watuhumiwa wengine wakidaiwa kutoroka kabla ya kukamatwa na polisi wanaoendelea na uchunguzi wa tukio hilo. #EastAfricaTV
....Hivi SI ingetosha TU kumkata na Kumpeleka Polisi kuliko kumpiga Hadi Kumjua Mdau wa Bar Yao ?? 🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom