Mwanza: Mlipuko wa baruti waua na kujeruhi watu saba

Mwanza: Mlipuko wa baruti waua na kujeruhi watu saba

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,034
Reaction score
6,891
Mtu mmoja amefariki dunia na saba wamejeruhiwa kufuatia mlipuko wa baruti uliotokea leo tarehe 01 Julai 2026 majira ya saa 12:46 asubuhi kwenye kibanda cha kahawa katika Mtaa wa Sahwa ya Juu, Kata ya Lwanhima, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafungwa amesema aliyefariki dunia katika ajali hiyo ni Marco Msenyere (52), mpasua mawe na mkazi wa Semba-Lwanhima. Wakati wa tukio hilo, marehemu alikuwa na wenzake wakinywa kahawa kwenye kibanda hicho akiwa na begi dogo ambalo ndani yake lilikuwa na baruti hizo.

Akielezea chanzo cha tukio hilo Kamanda amewataja kwa majina watu waliojereuhiwa katika tukio hilo.Aidha Kamanda Mutafungwa amesema chanzo cha mlipuko huo ni uzembe wa utunzaji wa baruti kwani Marehemu alibeba baruti hizo na kukaa nazo karibu na jiko la mkaa lililokuwa linawaka kwenye kibanda hicho cha kahawa huku akifahamu wazi kuwa baruti hizo zikipata joto hulipuka.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa viongozi wa Serikali za mitaa na wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu watu wanaotumia na kumiliki baruti pasipo kuwa na kibali huku akiwataka wenyeviti wa mitaa kufanya ukaguzi ili kuwabaini watu hao katika mitaa yao.
 
Hizo kitu zikiwa zimeungwa cortex vizuri na V6 vizuri, imeshindiliwa vizuri unafurahia show
 
Chadema ni tatizo
Mboni una nongwa sana na hawa jamaa?

Walikutemea kohozi kwenye kalio nini maana mtoto wa kiume kuzunguka jukwaa zima ukizungusha viuno huku ukiwataja taja wanaume wenzako bila mpangilio inatupa wasiwasi kidogo.
 
Back
Top Bottom