Mwandishi wa Ivory Coast ahoji AFCON 2027 kufanyika Afrika Mashariki yenye barabara mbovu na miundombinu mibovu

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Katika mkutano wa CAF uliofanyika hivi karibuni, Kuna kipande cha video cha mkutano huo kimeibua maswali mengi hususani kwa watu wa Afrika Mashariki, ikiwemo wakenya ambao kwenye kurusa za mitandao yao ya kijamii video hii imekuwa ikisambaa sana.

Video hii inamhusu muandishi wa habari kutokea Ivory Coast ambaye aliuliza swali ambalo lilionekana kuwakera watu kutokea Afrika Mashariki. Alisikika akisema

Sasa lingine linaenda katika nchi tatu za Afrika mashariki ambako tayari nilishafika. Hakuna barabara ndani ya nchi hizo. Baadhi ya wenzangu kutoka Afrika Mashariki waliniambia kutoka nchi moja hadi nyingine itakuchukua siku mbili kuendesha gari. Alafu wasiwasi wangu mkubwa na wasiwasi wa wengi wanahangaika kujua kama hatutashusha kiwango kwa kupeleka mashindano Afrika Mashariki au suluhu ni nini? maana tumeona sasa tuko Morocco, lakini AFCON ilitakiwa iwe Guinea Republic kwa sababu hawakuwa tayari ikahamishiwa Morocco na hii ni AFCON yenye kuhusisha nchi 24. fikiria katika Afrika labda ni nchi nne au tano zenye miundombinu isiyofaa ya kuikaribisha michuano. Je, kuna uwezekano wowote kwamba itaondolewa katika nchi hizo tatu au kuahirishwa tena? Hilo ni swali langu.

View: https://youtu.be/nttda6OWiCg?si=tvkAFrxBTawORycW

Wakenya na watu wengine wa Afrika Mashariki wamekasirishwa na kitendo cha Mwanahabari huyo ambacho limetafsiriwa kama ni kuchongea au kutoa habari ya uongo kuharibu taswira nzima ya Afrika Mashariki. Watu imebidi waende kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumzonga kwa maneno mbalimbali. Ukurasa wake ni huu

Screenshot_20260118_203625_Instagram.jpg
 
Kwanini wasingeliomna wao ku host?
 
Kama alizungumza bila kuwa na ufahamu sahihi wa mazingira yaliyopo kwanini asisalimiwe kwenye akaunti yake ili siku nyingine atafute taarifa rasmi kabla hajanyanyua kinywa chake.

Waliotoa nafasi kwa hizi nchi waliona inapendeza na wanastahili kuhost ndio maana wakapewa nafasi. Wao wanajionaga kama pekee ndio wanastahili hizo nafasi
 
Yeah kwa Miaka mingi limekuwa likifanyika huko kwao, lakini bado mioyo yao imejaa husda baada kuletwa ukanda huu
 
Katika mkutano wa CAF uliofanyika hivi karibuni, Kuna kipande cha video cha mkutano huo kimeibua maswali mengi hususani kwa watu wa Afrika Mashariki, ikiwemo wakenya ambao kwenye kurusa za mitandao yao ya kijamii video hii imekuwa ikisambaa sana.

Video hii inamhusu muandishi wa habari kutokea Ivory Coast ambaye aliuliza swali ambalo lilionekana kuwakera watu kutokea Afrika Mashariki. Alisikika akisema

View: https://youtu.be/nttda6OWiCg?si=tvkAFrxBTawORycW

Wakenya na watu wengine wa Afrika Mashariki wamekasirishwa na kitendo cha Mwanahabari huyo ambacho limetafsiriwa kama ni kuchongea au kutoa habari ya uongo kuharibu taswira nzima ya Afrika Mashariki. Watu imebidi waende kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumzonga kwa maneno mbalimbali. Ukurasa wake ni huu

View attachment 3531575

Kwani uongo !?
 
Amesema kweli
 
Sasa uongo uko wapi hapo!

Usafiri baina ya nchi za Afrika Mashariki unavhukua siku 2 kwa sababu ya ubovu wa barabara?

Yaani kwamba ukitoka Nairobi, unatumia masaa 48 kufika Arusha/Dar es Salaam au Kampala?
 
Back
Top Bottom