Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

baada ya kufulia uchaguzi wa serikali za mitaa wametoa single mpya kutuondoa kwenye mstari
 
Ni Aibu kwa serikali hii kukaa na wahujumu uchumi hadi wanapata nafasi ya kujihudhuru!.Kwani mpaka wao wanajibaini kuwa walifanya makosa! na serikali yenye madaraka kamili, inakaa kimya???.
Kweli hii mnatutendea haki wananchi!? Inamaana hamtaki kuwawajibisha kwasababu gani ya msingi?Ukiangalia walio jiudhuru kwa kashifa ya kukwapua mali za umma ni wengi na hakuna yeyote aliye chukuliwa hatua yoyote!. Hila kama kungekuwa na mtu aliyewajibishwa kwa ufujaji wa mali ya umma, nidhahiri watu wangeogopa, ndiyo maana watendaji wa serikali wanaweza kuchukua rushwa kubwa wakijua anaweza akajiudhuru na ikawa poa!. Sasa wabunge pelekeni mswaada bungeni kwa yeyeote atakayepatika na hatia ya kukwapua mali ya Umma akae maabusu kwa miaka 3 then ndiyo kesi yake itajwe na asiwe na dhamana.

Mbona nchi nyingine anajiudhulu na anawaJibishwa hiyo sheria hapa haipo bado???! hiyo hatua ni ya kwanza halafu huyu tumbili aturudishie pesa watu wanaku
Fa kwa kukosa dawa zamseto mahospitalini:thumbdown::thumbdown::thumbdown::thumbdown: yeye anasema atakata watu vichwa akiwa anafahamu kabisa kachimbia Pesa sehemu ,na aendelee kuishi kwa jasho letu milele noooooooooooooooooooo marekan na wote waliositisha msaada kataen mpaka hela zirudi kama zile za rada
Period😡😡😡😡
 
Wewe ni Rais wa wapumbavu jinga kabisa wewe.

Wewe lazima utakuwa mpambe wa Mengi au kafulila, Nenda kamwambie Kafulila ajiuzulu kwa kupaza Sauti baada ya kupokea mamilioni toka kwa mengi. Tambua kuwa Kafulila hakuifanya kazi kwa Uchungu toka moyoni bali alifanya kazi baada ya kulipwa mapesa kibao, na yeye ajiuzulu kwa kuchukua pesa ndipo afanye kazi badala ya kujituma mwenyewe.
 
Nukuu "Peresedor kamshukuru jaji kwa utumishi wake ulioongozwa na UAMINIFU NA UADILIFU" mwisho wa kunukuu...

Asee haya mambo yanawezekana tz pekee, mean kuwa maelekezo yote yalitoka juu na kutafsirika tofauti, ki ukweli kuna viongozi walisha wafanya watz kama mashabiki wa ngoma...

Hyo kauli haikupaswa kutolewa na mkuu wa kaya kama yy, means anataka kutuambia kuwa asinge jiuzuru ikulu isingemuajibisha??

Tanzania bila ........ inawezekana.
 
Ndugu zangu mh. Mnyika alishatuambia Urais na Rais wakiwa dhaifu haya ndiyo madhara take. Hii sinema tunayoina ni udhaifu wa taasisi ya Urais na Rais mwenyewe. Huwezi kuwa kiongozi makini katika hali kama hii unamwambia MTU ajiuzuru kwa uchafu wa namna hii halafu unadhihaki umma kwa kuwaamvia MTU huyu ni mwadilifu na mwaminifu! Upuuzi kabisa. Lazima kiongozi awe na uwezo wa kusoma akama za nyakati. Katika issue ya Escrow taasisi ya Urais imechafuka na imezidi kujidhailisha.
 
Mh.Profesa Jakaya kumpongeza Werema ni kuwakosea heshima watanzania wanaotaabika baada ya ukwapuzi wa fedha zao,au na wewe ni sehemu ya wezi?
Hali ya maisha imekuwa ngumu kwa sababu ya escrow then "eti"unatoa pongezi hii ni kejeli ya hali ya juu sana,nimekuchana live tena makavu.Katika dhambi umefanya JK hamna dhambi kubwa kama kumpongeza mwizi werema
Rest In peace Mwalimu Nyerere!
 
baada ya kufulia uchaguzi wa serikali za mitaa wametoa single mpya kutuondoa kwenye mstari

Pia Kafulila naye amejaa mapesa kibao toka kwa Mengi, Mkono na Membe.kufa kufaana.
 
mkuu, mbona una hasira sana? Au ni malalamiko baada ya kukosa mgawo?

Sina hasira, ila lazima tuwe watu wenye nia safi, sio kutetea ujinga kwa sababu ya Chama....hivi Lumumba mnamonitor akili za watu wenu humu kwenye Jukwaa? kuna wengine wanaharibu baada ya kusaidia propaganda za chama chenu....nachukuia hizi tabia za kusafisha mpaka waliojipaka vinyesi.
 
"Brownie, you are doing a heckuva job" - George W. Bush.
 
NaniniBaraka mimi nakuunga mkono kabisa. Mimi niliwahikusema kazini kwangu tokea ile issue ya EPA nikasema uwezo wa kikwete ni mdogo sana kuongoza taifa. Yaani uwezo wake wa kuchambua mambo hata binti yangu aliyoko darasa la tatu anamzidi mbali huyu jamaa. Kwa sababu kwa kiongozi mwenye kufikiria kwa kutumia kichwa chake hawzi kuthubutu kumpongeza mwizi aliyesababisha hasara kubwa hivyo kwa taifa. Labda huyu kikwete hatumii kichwa kufikiri. Haiwezi kumuuingia akilini mtu yeyote mwenye akili timamu kwa wizi uliofanywa na hawa wapuuzi kuona kiongozi wa nchi unatoa sifa kuwa alikuwa mwadilifu. Vipi kipimo cha uadilifu kwa kikwete ni kipi?
Kwa mtindo huu hawa viongozi wetu wanajenga radicals katika jamii biala wao kujua. Kwa mtu yeyote anayeumizwa na vitendo hivi vya viongozi kujitwalia mali za umma halafu wanalindana namna. Vijana wakiamka itakuwa kama tunavyoona Syria, Pakistan ambako watu wanajitoa muanga.

Amempongeza kiutu Uzima na hasa yeye amelenga kule kwenye Katiba ambapo kwa kushirikiana na Sita walifanya manuva hadi watu sasa wamesahau wapo busy na Tegeta A/c
 
Baada ya mzee wa pimbi kujichomoa unahisi NANI anafwata kesho ni swali langu m na we we....
Sty tuned

Pimbisode Part 2
 
Nukuu "Peresedor kamshukuru jaji kwa utumishi wake ulioongozwa na UAMINIFU NA UADILIFU" mwisho wa kunukuu...

Asee haya mambo yanawezekana tz pekee, mean kuwa maelekezo yote yalitoka juu na kutafsirika tofauti, ki ukweli kuna viongozi walisha wafanya watz kama mashabiki wa ngoma...

Hyo kauli haikupaswa kutolewa na mkuu wa kaya kama yy, means anataka kutuambia kuwa asinge jiuzuru ikulu isingemuajibisha??

Tanzania bila ........ inawezekana.

Tanzania tuanahitaji kuwa wajasiri sn wa kuhoji mambo,kikwete kakaa ikulu akidhani kuna cd itakuja kubadilisha mziki wa Escrow kachemsha,inahitaji muda gani kuwashughulikia wezi ambao ushahidi ni wa moja kwa moja,ndio maana wananchi wanakidirishwa na utendaji dhaifu wa rais wao,haitaji elimu yoyote kujua Escrow ulikuwa wizi,yaliyomkuta Mwinyi ya kuzabwa vibao yanaweza mkuta pia rais dhaifu mstaafu mtarajiwa,serikali inasimama na kutetea uwongo,kwa sasa hivi serikali haina pesa za kulipa wazabuni,na hata wakati mwingine Mishahara ya wafanyakazi!
Tuepukane na wanaotubeza kwa kukosoa serikali
 
Kikwete ana "I don't Care Attitude" Unadhani ana uchungu na Watanzania? Yeye na familia yake wameshajilimbikizia mali ambazo hata vitukuu hawawezi kuzimaliza.
Kwa kuwa wote ni wezi alikuwa hana nia ya kumwondoa ndo maana anampongeza kwa maana nyingine haoni sababu ya Werema kujiuzulu.
 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.


Mhe Rais kwa upepo huu kweli ameshindwa kuishia tu ... anamshukuru kwa utumishi wake NUKTA sasa alichoongezea mi sielewi sijui labda Watanzania muelewe
 
Back
Top Bottom