Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Inakera sana ila naumia kwa sabab sina cha kufanya kwa wakati huu ila najua kura yangu mwakani itawahukumu.Ndugu zangu watanzania,tusiwe wajinga na kugeuzwa watoto wadogo wanaodanganywa na pipi,hebu tijiulize,kujiudhiru tu inatosha kuwajibika juu ya upotevu wa mabilioni ya pesa!!?au ndio tunampa muda wakwenda kuzitumia vizuri hizo pesa.!!
TANZANIA TANZANIA naipenda nchi yangu ila sipendi viongozi wake!!!
 
Wewe lazima utakuwa mpambe wa Mengi au kafulila, Nenda kamwambie Kafulila ajiuzulu kwa kupaza Sauti baada ya kupokea mamilioni toka kwa mengi. Tambua kuwa Kafulila hakuifanya kazi kwa Uchungu toka moyoni bali alifanya kazi baada ya kulipwa mapesa kibao, na yeye ajiuzulu kwa kuchukua pesa ndipo afanye kazi badala ya kujituma mwenyewe.

Kama amelipwa mapesa na mtu binafsi ili kufichua majizi yaliyoiba hela za umma, naona bora yeye maana hizo alizopewa hazinisababishii umaskini, ila hizo mlizokwiba hadi sasa zimeniacha hoi bin taaban. Acheni kutafuta visingizio eti alitumwa na nani kulipua ishu hiyo...suala la msingi hapo ni kwamba wezi waliiba pesa za umma, basi! Mengine tutaangalia baadaye.
 
Naona kama mamlaka ya uteuzi ilifanya sawa kumshukuru mtuhumiwa ambaye alistahili kuwajibishwa. Unless aseme anamshukuru kwa kumpinguzia mzigo wa kumwandikia barua ya kumwajibisha.
 
Mtu akiomba kustaafu maana yake anastafu kwa heshima,huyu ----- AG alitakiwa astaafishwe kwa maslahi ya uma na kisha kustakiwa kabisa,kwanza anaonekana ni mbulula wa sheria kwa ushauri wake mmbovu kwenye fedha za escrow akaunti ambazo ni fedha za uma.
 
Wakati napita pita kwenye facebook nikakutana na hii ya Mh Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kasazini

zito kabwa.jpg


Mh Zitto Nakupendaje Lol
 
Huyu kashinikizwa ajiuzulu sio yeye kama yeye.viongozi wa hapa Tanzania kujiuzulu kwa matakwao yao huwa haipo mpaka washinikizwe kwani kwa hiari yao huwa ngumu.na hakupaswa kujiuzuru bali kikwete alipaswa kumfukuza kabisa maana hafai

Kikwete atathubutu vipi kumfukuza wakati Werema anawajuwa wezi wenzake akiwemo huyo Profesa wa kichina?
 
Wewe ni mtu wa kwanza kumtetea kwa nguvu huyo Feleshi. Nataka ujue tu kuwa hadi mtu mpole na mvumilivu kama Kikwete akuondoe ujue hufai kabisa!

Sidhani kama unamfahamu Dr. Feleshi , ni mtu mwadilifu mchapakazi na mzalendo , alicho sema jamaa ni sahihi. Ukitaka kujua fanya research. Mengine ni fallacy iliyojengwa na akina Hosseah, Werema na Masaju.
 
Habari wadau
Nimejaribu kumtathimini rais kiukweli nimeshindwa,sijui nimuweke kundi gani? kiongozi wa uma mwanasheria mkuu wa serikali ambae sisi wananchi tunajua amesoma na anafahamu sheria zote,anliingizia taifa hasara kwa kuruhusu wachache kukwapua pesa zetu tena akiwa anafahamu kabisa.

Leo anajiuzulu tena kwa shinikizo na muheshimiwa rais anampongeza kwa kummwagia sifa nyingi,eti muadilifu!!!!! muadilifu huwa anajiuzulu? kwa heshima ya watanzania naomba rais afute kauli yake
 
Nadhani viongozi wa vyama vya upinzani, Viongozi wa dini zote, taasisi za haki za binadamu na wananchi wote kwe ujumla. Huu ni wakati wa kuamka. Hii nchi ni yetu sote. siyo nchi ya kikwete na genge lake la wezi kutumia nafasi tulizowapa kujitajirisha wao na vizazi vyao. Kikwete mhuni tu hana lolote.
Makundi niliyoyataja hapo wanapaswa kuamka sasa hivi. siyo muda wa kuoneana aibu. Wananchi tukipata watu wa kumobilize atushindwi kudai pesa zetu zirudi. Mambo ya kutumia amani kama kinga ya kutonyonya ifikie mwisho sasa. Amani gani hiyo ya baadhi ya watu kujitajilisha kwa mali zetu utadhani wao ndo watanzania pekee. Acha amani ipotee watakao baki waishi kwa kuheshimiana. Tumeona sehemu nchi nyingi watawala walivyogeuza ofisi za umma kwa manuafaa yao, wananchi walivyo amua kuchukuwa hatua, kuna waliokufa lakini waliobaki sasa hivi wanaheshimiana. Angalia nchi kama china mwaka 1927 -1946 walipigana kwa sababu za kisiasa kama hizi baada ya upande mmoja kujiona kama wao ndo wenye haki la kula kila kitu cha umma (kama wanavyofanya akina Kikwete). Kama tunavyojua vita wakufa walikufa lakini baada ya hapo heshima ilikuwepo na leo angalia China ilipo kiuchumi. Rwanda nayo ni sababu kama hizo wakati wa utawala wa Abyarimana. Ndani ya serikali ya kiongozi huyu kiliibuka kikundi kilichokuwa kikitumiwa na huyo kiongozi kwa kupora na kuchukuwa mali za umma kama anavyofanya kikwete. (Hiki kikundi cha watu wachache ndani ya serikali kiijita akazu ikiwa na maana ya kajumba. Akazu walikuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote nchini Rwanda. Tuliona wananchi walipochoka akazu kalianga na leo Rwanda ina uchumi mzuri.

Huu ni wakati wa mabadiliko. Kwenye mabadiliko huwa kuna sacrifices. Kote dunia viongozi wa mabadiliko mara nyingi huwa hawayafaidi. Lakini watoto wao na ndugu na jamii nzima itakayo baki itawakumbuka kwa juhudi zao za ukombozi. Mfano mzuri ni Dr.Martin Luther King jr. Mwanzilishi wa vuguvugu la kupinda ubaguzi wa rangi huko Marekani, Japo kuwa hakuyafaidi mabadiliko hayo lakini leo hii anakumbukwa. Watanzania tunahitaji viongozi wenye nia ya ukombozi. Itishine maandamano tujikombowe kwenye mfumo wa ukandamizaji uliojaa rushwa wizi na kila aina ya uovu wa huyu kikwete.
 
Pesa zilikuwa BOT aliyesema zitoke zilipwe ni Werema na sasa kaachia ngazi, Mhongo akitoka lazima Gavana,Waziri wa Fedha,Waziri wa Viwanda na Biashara nao wang'oke kwani walifanya kazi sambamba iweje Mhongo ashinikizwe peke yake? Kisa ana Ugonvi na Mengi juu ya Udalali wa Vitalu vya Gesi, huku Mkono akiwa na Uchungu wa kunyang'anywa kazi zote za kisheria Wizara ya Nishati, Mhongo ni Shinikizo Binafsi la Mengi na Mkono kwa Manufaa yao, Tunaomba Kafulila na Zito nao wajiuzulu kwa kuwa walipewa pesa na Mengi ili wapaze sauti kwa Manufaa ya kuwafurahisha kisha kuwaaminisha wananchi ili wawaonee huruma mengi na mkono ambao pia si walipaji kodi ipasavyo, wao pia wakichunguzwa na FBI wana Madhambi lukuki, Nchi hii hakuna aliye Msaafi kiasi cha kumnyooshea mwenzake kidole, Watumishi wengi wa Umma wanaishi Kinyume na Vipato vyao Harisi, wakiletwa FBI hapa wawachunguze wote wenye Mali hakuna ambaye atapona.

Dawa inaendelea kuingia vizuri tulia kichaa kikuishe vizuri WWW ndio utakua na huelewa wakutofautisha mbichi na mbivu ili huache kuleta story za vijiweni wakati watanzania tunajadili mambo ya msingi kwa taifa letu
 
Nukuu "Peresedor kamshukuru jaji kwa utumishi wake ulioongozwa na UAMINIFU NA UADILIFU" mwisho wa kunukuu...

Asee haya mambo yanawezekana tz pekee, mean kuwa maelekezo yote yalitoka juu na kutafsirika tofauti, ki ukweli kuna viongozi walisha wafanya watz kama mashabiki wa ngoma...

Hyo kauli haikupaswa kutolewa na mkuu wa kaya kama yy, means anataka kutuambia kuwa asinge jiuzuru ikulu isingemuajibisha??

Tanzania bila ........ inawezekana.

Lazima Amshukuru kwani escrow imesaidia watu Kusahau Katiba pia akina Warioba na makongamano yao yamesahaulika, hata Lundenga anapumua sasa watu wamesahau juu ya miss Tz aliyejiuzulu, Werema amesaidia sana kuwasahaulisha watu juu ya Katiba lakini kosa alilofanya hakumpa Ganjia mwenzake Samweli Sita ambaye inasemekana ndiye aliibua hili sakata la IPTL
 
Ameondoka kwa kuharibu credibility ya Majaji na Mahakama ......ni wakati wake Majaji wamehongwa wazi wazi ,Mahakama imewekwa chini ya wanasiasa , kumbuka sheria ya utumishi wa mahakama alipopendekeza MADC na RC wawe wenyeviti wa kamati za utumishi wa mahakama .......amekuwa Jaji wa kwanza kutukana hadharani na kutishia kuua hadharani .........
 
Rais ajiuzulu haraka kwa kauli yake.
Hatuwezi kuwa na rais wa asiyemwadilifu
 
Dawa inaendelea kuingia vizuri tulia kichaa kikuishe vizuri WWW ndio utakua na huelewa wakutofautisha mbichi na mbivu ili huache kuleta story za vijiweni wakati watanzania tunajadili mambo ya msingi kwa taifa letu

inaelekea wewe umekariri na kuamini kile ulichokariri pekee! Jaribu kubalance pande zote usiishi kwa kukariri kuwa Kafulila katokea Mbinguni kaja kuibua hayo pekee, jaribu kujiuliza iweje Kafulila amkomalie sana Mhongo pekee wakati kuna Wizara Tatu zimehusika? Kumbuka Kafulila si Mungu wala Mengi aliyemtuma si mungu nao wanapaswa kujadiliwa pia.
 
Back
Top Bottom