Rais pamoja na busara zake anamshukuru mwizi? tena kwa press release, dah!! kweli Only in Tanzania.Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Kweli wewe ni Minyoo........inaelekea wewe umekariri na kuamini kile ulichokariri pekee! Jaribu kubalance pande zote usiishi kwa kukariri kuwa Kafulila katokea Mbinguni kaja kuibua hayo pekee, jaribu kujiuliza iweje Kafulila amkomalie sana Mhongo pekee wakati kuna Wizara Tatu zimehusika? Kumbuka Kafulila si Mungu wala Mengi aliyemtuma si mungu nao wanapaswa kujadiliwa pia.

utashangaa mangapi ndugu yangu kwa TZ hii??
Mkuu unadhani kaisema kwa bahati mbaya,anajua hasa Alichokisema......huyo Ndio JK anayemshangaa labda sio Mtanzania.......hiyo kauli imetoka kwa uthabiti, ww na mimi tunamuona Werema mzembe na pengine mwizi,kwa JK Ni jembe Tena la uhakika,hiyo Ndio CCM....Au Umesahau wale askari wa mwavuli waliosema hata ikibidi tule majani lkn lazima ndege mbovu ya rais ipatikane....... Sasa ili kukomesha hizo kauli dawa Ni kuwatoa 2015 wezi Hawa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
Mkuu kuna tofauti kati ya Source na Sauce,hata nikiachia hapo nadhani utanielewa kwani wewe ni msomi ambaye unaweza kuwa umeghafilika au kwa kusudi ulijualo.Tomato au Chili?
Sasa amepongezwa kwa lipi?hii nchi majanga matupu!
Habari wadau
Nimejaribu kumtathimini rais kiukweli nimeshindwa,sijui nimuweke kundi gani? kiongozi wa uma mwanasheria mkuu wa serikali ambae sisi wananchi tunajua amesoma na anafahamu sheria zote,anliingizia taifa hasara kwa kuruhusu wachache kukwapua pesa zetu tena akiwa anafahamu kabisa.
Leo anajiuzulu tena kwa shinikizo na muheshimiwa rais anampongeza kwa kummwagia sifa nyingi,eti muadilifu!!!!! muadilifu huwa anajiuzulu? kwa heshima ya watanzania naomba rais afute kauli yake