CAPTAIN MORGANI
Member
- Jul 27, 2013
- 29
- 5
Nafasi ya tumbili katika msitu wa nyika yadhihirika
Huyu kashinikizwa ajiuzulu sio yeye kama yeye.viongozi wa hapa Tanzania kujiuzulu kwa matakwao yao huwa haipo mpaka washinikizwe kwani kwa hiari yao huwa ngumu.na hakupaswa kujiuzuru bali kikwete alipaswa kumfukuza kabisa maana hafaiMwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
sasa simbachawene si amesoma open university hajawa na practice ya sheria, utasemaje ni mwanasheria, halafu si ndo alikamatwa na mke wa mtu singida gesti, umesahau? achen kupeleka makapi kwenye ofisi nyeti kama ile.chuki chuki chuki tuuuu
Mimi nimeshasema. Kikwete anazidi kuunda matatizo makubwa zaidi kwa taifa. Eti anamsifia kwamb utumishi wake uliongozwa na uaminifu sijui na uadilifu. Inahitaji ujasiri wa kifisadi kutamka maneno haya hadharani bila hay akwa mhusika wa kashifa iliyo dhahiri.
Asije kumpa kazi nyingine ama kumfanya balozi kwa sababu anazidi kuhatarisha usalama wa nchi. Hawezi kuimarisha mtandao wa majizi kana kwamba nchi hii ni yake. Ninaamini maneno yaliyozagaa kwamba Accounts za escrow, zilizokuwa Stanbic, ni za kikwete, mkewe na familia yao ndiyo maana anaishia kujiuma uma na kufanya unafiki ili kuwapoza mafisadi wenzake, wasimuumbue. They are team mates!.
Tunahitaji watu wote waliohusika kwa kashifa ya escrow wawajibishwa kisheria na warudishe fedha zote. Hadith za kijinga n kuwafaya watanzania wote ni wajinga hazikubaliki.
Tulijua nia ya kikwete na lowasa kwenda ikulu haikuwa kuwatumikia wananchi. Ilikuwa ni kukidhi tamaa zao za anasa na mtamanio binafsi lakini hatukujua zitakuwa na syndicate ya wizi mkubwa kiasi hiki. Kikwete ni mwizi na ni kiongozi mkuu wa mafisadi. Anastahili kuwajibishwa kwa kushindwa kazi na kuhujumu uchumi wa nchi huku akijenga misingi ya machafuko nchini.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
umbea mwingine bana. Sasa hapo ndo umeandika nn?
Bahati mbaya sana, haujui kitu. kikwete huyohuyo amekiri kuwa alikuwa misled kumwondoa, na hata alipotaka kumrudisha baada ya kumpa ujaji, feleshi alikataa. ameshakuwa jaji sasa nini tena, si akapumzike, ila ukweli ambao hauna kupindisha, WANAOMJUA FELESHI SIO WATU WA NJE YA OFISI ILE, NI WAFANYAKAZI WA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AU YEYOTE AMBAYE ALISHAWAHI KUPITIA ILE OFISI AU HATA KUFANYA KAZI NAYE. hao ndio wanaoweza kukwambia feleshi yukoje wakilinganisha na waliopita. hakuna dpp aliyekuwa imara na aliyepambana na system kama feleshi, ninajua hata wakimteua anaweza kukataa sijui wambembelezeje kwasababu kule alikoenda kuwa jaji ni sehemu ya kupumzika hakuna kuumiza kichwa. na kama atakubali, ofisi ile itakuwa na mabadiliko ya ajabu kama ilivyokuwa kipindi cha mwanyika ambaye naye aliibadilisha ofisi kwa utendaji mzuri sana lakini mafisadi wakamfanyia zengwe na kumtoa wakamweka werema ambaye mawakili wa serikali wote wanamsema kuwa hajafanya kitu chochote chenye faida kwenye ile ofisi zaidi ya kuiaibisha ofisi. MASAJU ambaye ni homebody wa werema wakimrudisha pale ni walewale tu.Wewe ni mtu wa kwanza kumtetea kwa nguvu huyo Feleshi. Nataka ujue tu kuwa hadi mtu mpole na mvumilivu kama Kikwete akuondoe ujue hufai kabisa!