Not_Yet_Uhuru
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 1,304
- 444
zamani nikiwa bado Form 3 nilikuwa nasoma tabora boys mwaka 2004,nikaja huku dsm rikizo ya mwezi wa kumi na mbili kwa shangazi yangu aliyekuwa anaishi karibu na ubungo plaza kwenye nyumba za national house.
Alikuja Masaju akawa anamsimulia shangazi,kuna kesi alitoka kuisimamia kama wakili wa serikali morogoro ilikuwa kati ya serikali na tajiri mmoja wa kihindi.Alipofika Morogoro kesho yake ndiyo kesi yenyewe alifikia guest ya kawaida alafu akajifungia ndani tu siku nzima,akawaambia wahudumu akija mtu kumuulizia aseme hamna mgeni.Basi yule Mhindi alihaha siku hiyo kila guest Morogoro akienda anamuulizia anatembea na picha yake anaenda anaulizia amefika mgeni anaonyesha picha yake.
Yule mhindi alitaka amhonge kabla hawajasimama mahakamni.Mhindi alimkosa Morogoro nzima.Nayeye alilijuwa hilo,nayeye hakutaka hata kuonana naye.Kesho yake wakati wakesi mahakamani mhindi mbele ya hakimu anashangaa kumuona ghafla na ni mbele ya mahakama.Alifanya mambo kwa haki pasipo influence ya rushwa.Ni mtu wa dini sana na mpenda haki.Mimi Mwenyewe ni Graduate mwaka 2011 pale UDSM sijapata ajira ,nachukia system iliyopo ,inayoendekeza urasimu.
Cake ya taifa inaliwa na watu wachache katika taifa.Viongozi wanatembea na maprado na maisha ya kifahari huku wengine wakiwa katika umasikini wa kutisha.Tofauti na wakati wa Nyerer e cake ya taifa ilikuwa inagawanywa kwa watu wote kwenye taifa,Mbuge wa zamani wakati wa nyerere ukimumuona saiz huwez kuamin kama alikuwa mbuge,cake ya taifa ilikuwa inagawanywa kwa watu wote sawa.Uingereza yenyewe Siasa siyo se hemu ya kutokea ni kazi ya kujitolea.Nimeona nilisemee hili siyo kwamba namtetea.
Acha sanaa...! tumeshuhudia wezi wakijitetea hadi kugalagala chini kuwa hawana kosa...Pinda alisema na kulia kuwa kuwa yeye ni mtoto wa mkulima, maskini na asiye na lolote, kumbe fisadi anayechechemea kwa kuelemewa na uongo, na unafiki..!
Hapo umeeleza kuwa huyo mhindi alizunguka hoteli zote akimtafuta akamkosa, je wewe ulikuwa na mhindi au na Masajo? na kama mhindi alimtafuta hoteli zote, Masajo ni nabii? Je alikuwaje huko nje na kuona anatafutwa hoteli zote? na je kama alipokea hizo rushwa angekuambia wewe na mama yako? ni ujasiri wa ccm au uongo tu umewajaa? Hadi bungeni wanadanganya, sembuse waje sebuleni kwako? useless!