Mwanangu wa miaka miwili amesema ameona wachawi

Mwanangu wa miaka miwili amesema ameona wachawi

Huyo mtoto hajarithi uchawi kweli? kwa mtu , Maana ukiona mtu anasema ameona wachawi na yeye ni mchawi.
 
Vijana WA sikuhizi mnashindwa kujua ishara MUNGU anawapa,ukiona mpaka mtoto anaona wachawi basi ujue nyie wazazi sio watu WA maombi....
hiyo ni alert kuwa mnahitaji kuomba MUNGU Kwa bidii ili aweze kuwa msaada wenu,usikubali kuishi Kwa kutegemea nguvu zako na Akili zako
Kweli kabisa, kuna mmama alinihadithia jambo kama hili. Binti yake wa miaka miwili na miezi aliona wachawi usiku wamelala, akamuamsha mama yake. Akamuonyesha kuwa kuna watu kwenye kona moja ya chumba. Mama yake katika hali ya uoga akaanza kuomba mara ghafla akaanza kuwaona kweli na ndipo wakaanza vita wachawi wanataka wakaribie kitanda yeye anawazuia kwa Fire in Jesus name. Anasema ilikuwa kama movie hivi. timaye alifanikiwa kuwafukuza na hali hiyo haijawahi kujirudia.
 
Magreat thinker usikuwa wa leo skupata usingizi kabisa baada ya mwanangu mdogo kabisa wa miaka 2 na miezi 8 hivi kushituka usingizini na kutamka maneno ambayo hajawahi kuyatamka kabla tangu ajue kuongea.

Maneno aliyoyatamka ni haya, "wachawi na nyie wachawi nimewaona", sasa alivyoshituka mimi na mama yake pia tulishituka kumsikiliza alivyo maliza tukasikia mkwaruzo juu ya bati, sasa basi kwa ninyi mainteligensi hii ni hali gani?
hizo ni dalili za malaria muwahishe mtoto hospital
 
Huyo mtoto hajarithi uchawi kweli? kwa mtu , Maana ukiona mtu anasema ameona wachawi na yeye ni mchawi.
Huo ni uongo ambao unaenezwa na wachawi wenyewe ili kuzuia watu wasiwaite wachawi. Wachawi wapo na mtu yeyete mwenye nguvu ya kiroho anaweza kuwaona
 
Nakumbuka kuna nyumba niliwahi panga nayo ilikuwa na mauzauza ya wachawi
Basi nakumbuka siku moja mtoto chumba cha jirani alikuwa analia Sana kitendo kilichopelekea mama wa mtoto huyo kukosa usingizi

Ila KWAKUWA braza Mshana aliwahi kusema mtoto akiwa analia Sana usiku mpake kitunguu saumu kwenye paji la uso, nami nikasema ngoja nikamshauri huyu mama

Ile natoka nje nikakutana na mpangaji mwenzetu kajifunga nguo ya kaniki ile kuniona tuu akapotea

Nikajua huyu ndiye alikuwa anamfanyia yule mtoto michezo

Wachawi wanatabia moja wakiona unatofauti nao halafu unamtoto mdogo basi humsumbua huyo mtoto wakiamini kwamba huyo mtoto akilia basi hata wazazi wake hamuwezi pata usingizi kama kuupata ni alfajiri kalibia na kukicha, wachawi Nyoko Sana wanatesa sana
 
Huo ni uongo ambao unaenezwa na wachawi wenyewe ili kuzuia watu wasiwaite wachawi. Wachawi wapo na mtu yeyete mwenye nguvu ya kiroho anaweza kuwaona
Nguvu ya kiroho ya kuona wachawi ni mtazamo wa makanisa ya kisasa,sio mtazamo wa kibiblia
 
Nisiwe muongo ila siwezi kung'amua ni nini kimetokea.
Ila binti yangu akiwa na umri huo kama wa mwanao...tukiwa kariakoo ila sijui ule ni mtaa gani....nilikua nimembeba akaniambia...baba angalia wale hawajavaa nguo...na amekazia macho watu kama watatu walikua wanapita.
Na nilimuuliza zaidi ya mara moja na yeye alikazania kua hawajavaa nguo.
Sijui aliona nini na kwasababu gani...ila ndo ivo.
Hii pia ilishawahi nitokea kwa mwanangu akiwa na miaka around 3. Tena akawa anaonyesha kwenye pembe ya chumba ananiambia mami watu wale pale naogopa (huku anajificha uso)

Kwa kweli kulikuwa na matukio mengi sema kwa maombi tupo salama mpaka sasa.
 
kwenye elimu ya mbingu nipo ziro,nilipoamka tu niliamua kumtafuta sangoma mtaani kwetu kanipa black powder ndo nimetoka kutekeleza maagizo usku huu,sasa nione kama usiku huu itajitokeza tena au la!
Black powder gani? mnazidi kujiharibu
 
Nimecheka kuna mdau kanena ety watoto wanauwezo wa kuona vitu vingi ila kusema ndio inakua shida. Hizo ni story za kusadikika maana hakuna findings iliyokuja na proof. ( nani katika utoto wake aliwai ona wachawi)

Chunguza cycle ya mtoto wako, watu anaocheza nao, muvi anazo angalia, story anazopiga na wenzake. Ubongo unapenda kufanya marejeo kwa yale unayowaza zaidi/ kusemwa zaidi.
Pumbavu kweli wewe. Mimi nina ushuhuda, nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaona wachawi wanaingia nyumbani.

Na hili nilishalieleza kwenye nyuzi zangu za nyuma humu humu.
 
hiyo sio hadithi ila ni kweli amewaona watoto wanao uwezo wa kuona vitu ambavyo sisi watu wazima hatuwezi kuona na ndiyo maana hata Yesu alisema kuwa WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU lakini pia kuna ule msemo kuwa watoto wadogo ni MALAIKA haka kamsemo kana ukweli ndani yake....
mimi mwenyewe kipindi hicho 2007 au 2008 tukiwa nyumbani familia nzima mida ya saa nne mdogo wangu aliinuka akatatuta fimbo akawa anapiga kwenye pipa huku akisema fulani huyu hapa amekuja kunichukua baba alikuwa anamzuia asipige baadaye akasema kuna mmoja amekaa hapo mlangon kichwan amebeba chungu cha moto ananinyooshea kidole nisiseme na kunitishia familia yetu ilikuwa haiamin hayo mambo kama yapo ila ile siku wote tulipigwa na butwaa hatujui nini kimetokea maana ana ona peke yake wengine sisi wote watu wazima hatuoni kitu ila sijui walimfanyaje akawa haoni tena....hivyo basi haya mambo yapo na yanatokea kila cku wenye macho yao wanaona wenzangu na sisi ndiyo hivyo hatuambulii kitu
 
hizo ni dalili za malaria muwahishe mtoto hospital
shughuri yangu ni health services provider hivyo nililizingatia hilo kwa kumfanyia mrdt also B/s lakini neg zote na yupo anacheza bila tatizo ndugu
 
Magreat thinker usikuwa wa leo skupata usingizi kabisa baada ya mwanangu mdogo kabisa wa miaka 2 na miezi 8 hivi kushituka usingizini na kutamka maneno ambayo hajawahi kuyatamka kabla tangu ajue kuongea.

Maneno aliyoyatamka ni haya, "wachawi na nyie wachawi nimewaona", sasa alivyoshituka mimi na mama yake pia tulishituka kumsikiliza alivyo maliza tukasikia mkwaruzo juu ya bati, sasa basi kwa ninyi mainteligensi hii ni hali gani?
Hao kiboko yao ni damu ya Yesu,jifunze jinsi ya kuitumia hutapata shida...
 
Black powder gani? mnazidi kujiharibu
mdau hiyo nayo ni sayansi,ni wengi nimekuwa nikiletewa kwenye huduma ya matibabu lakini kwa elimu na utalaamu wangu unapokoma bila mafanikio huwa natoa go ahead lakini wengi wanaingia kwenye tiba mbadala na baada ya muda nawaona wapo shwari kabisab hivyp huku wanga ni high rate
 
Kweli kabisa, kuna mmama alinihadithia jambo kama hili. Binti yake wa miaka miwili na miezi aliona wachawi usiku wamelala, akamuamsha mama yake. Akamuonyesha kuwa kuna watu kwenye kona moja ya chumba. Mama yake katika hali ya uoga akaanza kuomba mara ghafla akaanza kuwaona kweli na ndipo wakaanza vita wachawi wanataka wakaribie kitanda yeye anawazuia kwa Fire in Jesus name. Anasema ilikuwa kama movie hivi. timaye alifanikiwa kuwafukuza na hali hiyo haijawahi kujirudia.
Uongo mtupu.
 
hiyo sio hadithi ila ni kweli amewaona watoto wanao uwezo wa kuona vitu ambavyo sisi watu wazima hatuwezi kuona na ndiyo maana hata Yesu alisema kuwa WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU lakini pia kuna ule msemo kuwa watoto wadogo ni MALAIKA haka kamsemo kana ukweli ndani yake....
mimi mwenyewe kipindi hicho 2007 au 2008 tukiwa nyumbani familia nzima mida ya saa nne mdogo wangu aliinuka akatatuta fimbo akawa anapiga kwenye pipa huku akisema fulani huyu hapa amekuja kunichukua baba alikuwa anamzuia asipige baadaye akasema kuna mmoja amekaa hapo mlangon kichwan amebeba chungu cha moto ananinyooshea kidole nisiseme na kunitishia familia yetu ilikuwa haiamin hayo mambo kama yapo ila ile siku wote tulipigwa na butwaa hatujui nini kimetokea maana ana ona peke yake wengine sisi wote watu wazima hatuoni kitu ila sijui walimfanyaje akawa haoni tena....hivyo basi haya mambo yapo na yanatokea kila cku wenye macho yao wanaona wenzangu na sisi ndiyo hivyo hatuambulii kitu
Mliamini? Acheni kuwaonyesha watoto mamovie ya kichawi.
 
Hayo mambo ni magumu sana.Mtoto kaongea halafu bati linakwaruzwa.Yaweza ikawa ni coincidence tu.Mtoto asisimuliwe hadithi za wachawi/ushirikina na asioneshwe filamu za kutisha zinazohusiana na uchawi.Ataweweseka usiku halafu ihusishwe na ulozi.
Wewe mchawi acha kuficha mambo yenu nyie wachawi mpo sana mnatuwangia sana na familia zetu afu mnazuga labda ndoto mi mwenyewe nimewahi shuhudia wachawi mara nyingi tu live
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom