Mwanangu wa miaka miwili amesema ameona wachawi

Mwanangu wa miaka miwili amesema ameona wachawi

kwenye elimu ya mbingu nipo ziro,nilipoamka tu niliamua kumtafuta sangoma mtaani kwetu kanipa black powder ndo nimetoka kutekeleza maagizo usku huu,sasa nione kama usiku huu itajitokeza tena au la!
Na hapo ndipo ulipofanya kosa, wachawi hawakubali kushindwa. Wakitaka kuja wakaona wanashindwa kuingia kisa Kuna dawa umeweka basi jua kuwa umetangaza vita nao, watarudi kukuwekea vikao na hakuna rangi utaacha kuona. Ulitaka kwa imani yako uombe Mungu tu
 
Nakumbuka nikiwa mdogo nina miaka kama miwili, nilishuhudia kitu cha ajabu, mpaka leo sielewi ni uchawi ama nini. Na hii kumbukumbu ilishatoka lakini leo nimekumbuka kumbukumbu ya muda mrefu sana.
Nilikuwa naumwa miaka hiyo na ndiyo tulikuwa tumehamia kwenye nyumbani kwetu, na nyumba haikuwa imemalizika vizuri, hakukuwa na umeme na juu ya paa hakukuwa na ceiling board hivyo kunakuwa na kauwazi juu.
Basi siku hiyo mida kama ya usiku, nilikuwa napewa dawa maana Mama alikuwa ni muuguzi. Taa ilikuwa ya chemli inawaka, sasa wakati nimelala kuangalia juu, nikamuona mwanamke anatisha sana mrefu kasimama upande wapili ya chumba, na ameegemea ukuta kama ananichungulia hivi. Aisee nilikuwa kama nimegandishwa nikashindwa hata kuwaambia ndugu zangu ninachoona. Na mpaka leo sijawahi kumwambia mtu. Hiyo ilisababisha nikawa mwoga sana utotoni mida ya usiku hata chooni nilikuwa siendi ntabana mkojo mpaka asubuhi.
 
Ungekua muislamu ningekuelekeza cha kufanya ila imani ni tofauti
 
Watoto wanaona, hata ungeongea naye kiutani utani ... bebi eti yule ni nani vile.. ntakupa pp au mpe anachopenda atakuambia.

Sasa usipanic yafanyie aliyoyaona kazi.

Dua, sala, maombi
Absolutely !!
 
Acha kumlisha mtoto ujinga
mkuu hapana neno nimemlisha mtoto zaidi ya mimi kuhamaki kilichonenwa na mtoto hususani usku wa manane ili hali tunajuwa mambo mengi ya ulimwengu wa giza hufanyika nyakati hizo za ucku
 
mkuu hapana neno nimemisha mtoto zaidi ya mimi kuhamaki kilichonenwa na mtoto hususani usku wa manane ili hali tunajuwa mambo mengi ya ulimwengu wa giza hifanyika nyakati hizo za ucku
Mtoto anasema yale amesikia mkisema
 
Hayo mambo ni magumu sana.Mtoto kaongea halafu bati linakwaruzwa.Yaweza ikawa ni coincidence tu.Mtoto asisimuliwe hadithi za wachawi/ushirikina na asioneshwe filamu za kutisha zinazohusiana na uchawi.Ataweweseka usiku halafu ihusishwe na ulozi.

Maana ulimsimulia wewe?
 
1:Wachawi, malaika,majini
2:Ukikuwa memory inafutika mfano tuu ziwa la mama unajua utamu wake leo hii.

Ziwa la mama ni uchawi, mtu anapokua mdogo utambuzi kwake inakua ni changamoto. Ndio maana tunakuja humu kusema watoto wanaona uchawi
 
Mkuu kumbe unaishi Simba wanga mmmh Nisalamie huyo Sangoma uliekwenda kuchukua black powder Ila nafuu siumepata mkuu siumeweka na Kinga kila la kheri Mzee wa Simbawanga Ila hakikisha unaomba Dua kabla ya kulala na ukiamka umshukuru Mungu Kwa kuwaamsha mkiwa salama.
 
Wacha niwasaidue hilo
Kuna kitu kunaitwa spirit femament
Kuna watoto wamepewa ufahamu wa rohoni tangu kuzaliwa So ma-anga yao ya kiroho yamefunuliwa yako wazi
Wanaweka wakaona, wakatambua, vile ambavyo wengine hawawezi ona
Hadi hapo fahamu zao zitakspopigwa na ibilisi shetani wapofuke kama wanadanu wengine.

Kuna wengine nafsi za zimechukuliwa kuzimu tangu tumboni
Shetani amewafanya watumushi wake
Wanatumika kuzimu na wanaona mambo ya rohoni kabisa ambayo wengine hawaoni
 
Msiwe mnamuacha aangalie movie za ki-Nigeria...
 
Mi mwanangu ilishatokea kastuka usingizini akaenda moja kwa moja dirishani. She was around 2 years na alikua na mama yake, mi sikuepo. Mama nae ile kuamka kuangalia dirishani wanamuona mtu nje anaondoka. Hawakujua ni mchawi/mwizi au nani bt kilichoshangaza ni mtoto kuamka usingizini then kwenda kuangalia dirishani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom