Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 912
- 4,247
Mhe. Rais ameelekeza korosho yote ya Mtwara isafirishwe kwa njia ya meli kupitia bandari ya Mtwara; vinginevyo ukitaka kusafirisha kwa barabara lazima uombe kibali kwa mkuu wa mkoa na polisi ikieleza kwanini uruhusiwe kutumia barabara.
Kwanini amri hii imetolewa ? Kuna faida gani kutumia bandari na kuna hasara gani kutumia barabara? Je, kwa wananchi wa mikoani watatumia bandari? Nchi jirani je nao wakitaka korosho watatumia bandari? Naombeni elimu kuhusu hoja hizi na faida kwa mkulima endapo tutatumia bandari
Hivi karibuni Mhe. Bashe alisema muda wa kumdhibiti mkulima wapi auze mazao yake umeisha sasa hivi mkulima anayo haki ya kuchagua nani amuuzie........je kauli ya Mhe. Bashe kwenye korosho haitahusika?
Lakini pia naona kama jeshi la polisi siyo taasisi sahihi kudhibiti biashara NCHINI hasa pale ambapo hakuna sheria iliyolipuliwa; kwa mfano mfanyabiashara amekamatwa anasafirisha korosho kwa barabara jeshi la polisi litatumia sheria gani kumchukulia hatua?
Lakini pia kauli hii haijaweka wazi, ni wakati gani polisi wataanza kuhesabu kwamba umesafirisha korosho kwa barabara? Ukitoka Mtwara au hata ndani ya Mtwara? Vipi mikoa mingine ambayo bandari ya Mtwara siyo sehemu sahihi yakupakia?
Mwisho utatofautishaje korosho za Pwani na zile za Mtwara? Najaribu kupata concept ya matumizi ya bandari ya Mtwara vs mfumo wa ununuzi wa korosho sipati majibu sahihi.......naona hata zile korosho za kula sasa zitaondoka super market na wananchi wanaofanya biashara hiyo wataathirika sana...
Serikali itoe mwongozo kwenye hoja hii kabla ya wapinzani kuichukua na kuifanya agenda