Kuna madai mengi mtaani yanayosema kuwa mwanamke akiwa kwenye hedhi husababisha kunyauka kwa mboga na matunda ikitokea amechuma. Mdau mmoja wa JamiiForums amendika pia kuhusu suala hili.
Baadhi ya tamaduni huwazuia kabisa wanawake wasichume vitu hivyo. Kisayansi, madai haya yana ukweli?
Baadhi ya tamaduni huwazuia kabisa wanawake wasichume vitu hivyo. Kisayansi, madai haya yana ukweli?
- Tunachokijua
- Hedhi ni tendo la kiasili na kibaiolojia linalotokea kwa mwanamke baada ya kufikia umri wa kuvunja ungo. Tendo hili huwa na umuhimu mkubwa katika kupima uimara wa afya ya uzazi ya mwanamke. Huundwa kwa damu, ute wa mlango wa kizazi, majimaji ya uke, tishu za mji wa uzazi, madini ya chuma, sodium, calcium, phosphate na chloride
Kwa mujibu wa UNICEF, 26% ya wanawake wote duniani wapo kwenye umri unaoruhusu tendo hili litokee maishani mwao.
Tamaduni za nchi nyingi duniani huchukulia hedhi kama jambo lisilofaa kutokana na uwepo wa nadharia nyingi zisizo na uthibitisho wa kisanyansi. Utafiti uliofanywa na UNICEF kwenye nchi za Afghanistan, Bangadesh, Ethiopia, Ghana na Indonesia unathibitisha ukubwa wa tatizo hili. Mfano nchini Afghanistan, wasichana hukatazwa kula nyama, mboga za majani pamoja na kunywa maji ya baridi. Aidha, hukatazwa pia kuosha vyombo na nguo.
Kwa Tanzania, tamaduni za jamii nyingi hukataza wasichana kuchuma mboga wala pilipili, baadhi hukatazwa kubeba mtoto mchanga kwa madai ya kumdhuru au hata kumsababishia homa na maambukizi na wengine huambiwa kukaa mbali na Wanyama kwa kuwa wanaweza kushambuliwa nao. Hii ni mifano michache tu kati ya mingi.
Ukweli wake kisayansi
Kisayansi, tendo la hedhi haliwezi kwa namna yoyote ile kukausha mboga, kupukutisha pilipili, kuchafua maji pamoja na kusababisha maambukizi ya aina yoyote kwa mtoto mchanga. Hizi ni nadharia zisizo na mashiko kisayansi.
UNICEF na WHO wanataja ukosefu wa elimu ya kutosha kwenye jamii zetu kama chanzo namba moja kinachofanya mitazamo na nadharia hizi ziendelee kushika kasi kwenye jamii zetu.
Kisayansi, madai haya sio sahihi. Hedhi ni kitu kinachopaswa kuchukuliwa kama jambo la kawaida kwenye maisha ya binadamu na baadhi ya wanyama kwani ndiyo msingi wa muendelezo wa kuuleta uhai mpya duniani.
Kwa msingi wa hoja hizi umejijenga kiimani, JamiiForums inachukulia suala hili kama nadharia inayopaswa kuchunguzwa zaidi ili kupata uthibitisho unaoweza kupimwa kwa njia zilizo wazi.