Mwanamke kupata mimba pasipo ridhaa ya mwanaume liwe kosa la jinai

Ardhi haipangiwi kuwa ioteshe mmea au isioteshe labda kama utaweka mbegu mbovu shambani, haitoota, ila ukiona kuwa haitaki mbegu iote shambani, basi iache ndani ya magunia.
 
Wanawake wengi wanapitiia changamoto ya mfumo wao wa hedhi ukiachana na wachache wanaoamua wenyewe kuibambika, wangeanza kupewa elimu ya mzunguko wa siku zao kwanza, unakuta dame analalamika mi siku zangu zipo tofauti mwezi ulopita nimeona tar14 mwezi huu tar21 as if anataka zijirudie tar14 hiyohiyo kila mwezi mpaka unamshangaa
 
Wanawake wengi wanapitiia changamoto ya mfumo wao wa hedhi ukiachana na wachache wanaoamua wenyewe kuibambika, wangeanza kupewa elimu ya mzunguko wa siku zao kwanza, unakuta dame analalamika mi siku zangu zipo tofauti mwezi ulopita nimeona tar14 mwezi huu tar21 as if anataka zijirudie tar14 hiyohiyo kila mwezi mpaka unamshangaa
Yaani hawaelewi kabisa maana ya mzunguko. Mtu anataka iangukie tarehe hiyo hiyo kila mwezi badala ya kuzingatia interval kati ya period moja na nyengine.
 
Serikali ya JMT hili nalo mkalitazame na mlifanyie kazi.
Hakika Ni Jambo ambalo linaweza kuleta tija katika jamii zetu.
 
si itasaidia lakini??
si itasaidia lakini??
Ni vizuri offcourse hata mm siwez pata mimba bila kuhitaji na tukubaliane na huwa Niko wazi kbisa Kwa mtuwangu Kwamba hiki sihitaji na nikitaka aseme pia nae anahitaji twendesawa nami km nitaridhia

Lkn sio sawa kunawanaume pia ni waharabifu wa mabint anajua haitaji mtoto why asiseme wapnge njia ya Uzazi wawe salam wote
 
Wanawake wengi wanapitiia changamoto ya mfumo wao wa hedhi ukiachana na wachache wanaoamua wenyewe kuibambika, wangeanza kupewa elimu ya mzunguko wa siku zao kwanza, unakuta dame analalamika mi siku zangu zipo tofauti mwezi ulopita nimeona tar14 mwezi huu tar21 as if anataka zijirudie tar14 hiyohiyo kila mwezi mpaka unamshangaa
Ni Kweli lkn kuwawazi ni muhimu Pia km hauhitaji aisee mm nasema kbisa
 
Yaani hawaelewi kabisa maana ya mzunguko. Mtu anataka iangukie tarehe hiyo hiyo kila mwezi badala ya kuzingatia interval kati ya period moja na nyengine.
Ni kweli, mabinti wengi wanapata mimba wala hawapendi, ila hawajui kabisa mizunguko yao ipoje, mtu ana mzungguko wa siku28 anahesabu kama mtu wa siku30, lazima siku moja itanasa tu
Ni Kweli lkn kuwawazi ni muhimu Pia km hauhitaji aisee mm nasema kbisa
Ishu inakuja kuwa kwa mahesabu yako wewe ulopiga unaona upo siku safe kusex lakini kumbe kimahesabu upo danger days, so unashtuka after a week unaamka umechokachoka huelewi ndo tayari hivyo
 
MWANAMKE KUPATA MIMBA PASIPO RIDHAA YA MWANAUME LIWE KOSA LA JINAI.

Anaandika, Robert Heriel

Sisi kama wanaume tumekubali kabisa kuwa Kufanya ngono na Mwanamke Chini ya miaka 18 hiyo itahesabika kama Kosa la JINAI, Kwa jina la Ubakaji, bila kujali hiyo Binti alifanya Kwa ridhaa yake au Kwa kulazimishwa. Tumekubali.

Pia kesi ya ubakaji inaweza kuwa hata Kwa Mwanamke mwenye zaidi ya miaka 18 ikiwa tuu hakukuwa na makubaliano ya ridhaa Kwa Mwanamke. Na adhabu yake sio mchezo, ni Mvua ya miaka 30, yes miaka thelasini. Sawasawa! Tumekubali.

Sisi kama wanaume tunafanya Mapenzi Kwa sababu kuu ambayo ni Starehe Kwa 99%, kufurahisha Nafsi na mioyo yetu. Hiyo asilimia 1% iliyobaki ndio inahusu mambo ya Kupata Watoto ikigawana na kutafuta heshima Kwa wanaume wasio na Pesa.

Wakati wenzetu Wanawake, Dada zetu, Mama zetu hufanya mapenzi Kwa sababu nyingi Sana ikiwemo
I)Kuturidhisha Sisi wakitaka kupendwa, 25%
ii) Kupata Fedha na mambo ya kiuchumi 50%
iii) Kustarehe, 24%
iv) Kupata Watoto. 1%

Wanawake lazima waelewe Sisi tunapowatongoza tupo kwaajili ya Jambo moja kuu nalo ni Starehe tuu. Yaani ukiona mwanaume amekutongoza au anakukodolea macho basi elewa hapo anachotaka ni Starehe tuu. Tena akiwa ameoa ndio kabisa.

Serikali lazima itutendee Haki wanaume, Kustarehe sio kosa kisheria, na kisheria hakuna kosa la Kustarehe na Wanawake ikiwa tuu sio Wake za Watu, au Watoto Chini ya miaka 18.

Haiwezekani unakutana na Mwanamke kwaajil ya Kustarehe alafu anakuletea mambo ya Mimba, huo ni uhuni. Ushenzi na sio uungwana.

Serikali iweke sheria kuwa Mwanamke kubeba mimba ya mwanaume pasipo ridhaa ya mwanaume ni kosa la jinai, na adhabu itungwe. Huo ni uhuni.

Najua kuna Watu wataniona hamnazo au nimechanganyikiwa, au ninatabia za kishenzi lakini Kwa upande wangu nipo Mbele ya Muda. Ninazingatia Haki za Pande mbili, yaani Mwanamke na Mwanaume.

Mwanamke kwenye Hii Dunia ana-control mambo makuu mawili natural, ambayo ni Sex na reproduction. Mwanamke ndiye anatawala tendo la Ndoa pamoja na ishu ya Uzazi. Hayo mambo mawili.

Ni jukumu la Mwanamke kudhibiti suala la mimba. Na ikiwa anataka kubeba mimba ni lazima aongee na Mwanaume wakubaliane. Huo ndio uungwana, hiyo ndio HAKI.

Sheria Hii ya Mwanamke kubeba mimba pasipo ridhaa ya mwanaume italeta tija ndani ya jamii yetu. Kama ifuatavyo;

1. Itapunguza migogoro ya kijinga ambayo haina maana.

2. Itawafanya Wanawake wasikubali kubeba mimba bila ya Ndoa au pasipo kuandikishana(makubaliano maalumu) iwemo sahihi ya Mwanaume, ikiwa Mwanamke hajaolewa.

3. Itapunguza single mother ambao wengine Kwa Makusudi hujibebesha mimba Kwa maamuzi Yao wajitegemea liwalo na liwe, au wakidhani watapata huruma au mapenzi ya wanaume.

Kuzaa Watoto hakuna uhusiano wowote na kuongeza hisia za mwanaume kama hakupendi. Acha niseme ukweli WA moja Kwa moja.

4. Itapunguza Wanawake wanaoingilia ndoa za Watu na kujibebesha mimba na kuharibu ndoa za Watu. ATI kisingizio mwenye kosa ni Mwanaume Kwa sababu alimfata. Ni Kweli mwanaume alikufata lakini alifuata Starehe lakini sio Watoto. Zingatia makubaliano yenu, Kabla hujalala na Mwanaume muulize swali ikitokea Umepata mimba nini kitatokea, uone atakujibu vipi, majibu hayo muandikishe aweke sahihi. Uone kama hataghairi.

5. Itapunguza Watoto kuzaliwa bila ya Ndoa, makubaliano.
Ndoa ndio sehemu pekee mtoto anazaliwa Kwa ridhaa. Ukishaolewa jua tayari umesaini makubaliano ya kuzaa Watoto.

Lakini kama haujaolewa hiyo sio kazi yako. Kazi yako ni Starehe na unatakiwa kulipwa.

Haiwezekani umetoka zako kwenye Starehe na Mwanamke na lengo likiwa ni Starehe alafu mtu akuletee vitu visivyoeleweka.

Serikali hasa watunga sheria wajue kuwa ni ukiukwaji wa Haki za binadamu hasa Kwa wanaume kumbebea mimba pasipo ridhaa yake. Ni jinai ambayo haijawekwa kwenye sheria. Iwekwe.

Ooh! Wakati unafanya hukujua mimba inaweza kutokea? Wanaouliza maswali haya sijui wanatumia Akili ipi, ni uhuni, Utapeli na unyanyasaji Kwa wanaume. Kumpa kazi isiyomhusu.

Kama lengo ni kuwapendelea Wanawake Kwa kubinya Haki za Wanaume ni Sawa, lakini hiyo kamwe haiwezi kuwa Haki.

Unakuta kijana wa Watu Hana Mpango WA kuwa na Watoto lakini hiyo haimaanishi hapaswi kufanya ngono/mapenzi. Mapenzi yapo sio kwaajili ya Uzazi tuu Bali pia ni Starehe.

Wataalamu washeria na mnaopenda Haki liangalieni Jambo hili, mlifanyie kazi.

Nimemaliza! Mnaochukia mchukie, wenye matusi mtukane. Ila Sio HAKI kubeba mimba ya mwanaume pasipo ridhaa yake. Huo ni ukatili wa kijinsia.

Nawatakia Sabato NJEMA.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mimi mwenyewe ni mwanamke lkn hoja yako ina mashiko. Hii itasaidia kupunguza ukatili dhidi ya watoto. Na kesi nyingi sana za kutekelezwa ukisikiliza unakuta mama aliamua kubeba mimba ili iwe kigezo cha kupata ndoa au fedha za kujikimu.

Wakiweka sheria hii itatutafanya tufikirie mara mbili kabla ya kufanya maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom