BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,390
- 8,155
#TAWLA imesema pendekezo hilo linafuatia ongezeko la kesi zenye Sura tofauti za Ukatili zikiwemo zinazohusiana na malalamiko ya Wanawake kulazimishwa kufanya Tendo la Ndoa pamoja na Kuingiliwa Kinyume na Maumbile.
Hadi sasa Sheria inatamka kwamba ni Kosa la Jinai kumlazimisha Mwanamke kufanya Tendo la Ndoa Bila Idhini Yake ambapo Wanaharakati hao wameshauri Kitendo cha Mume Kumbaka Mkewe Kitajwe na kitambuliwe kama Kosa la Jinai kwenye Sheria.
==============
Mjadala wa mume kumbaka mkewe jana ulikuwa ni miongoni mwa hoja za wanaharakati wa masuala ya kijinsia baada ya kushauri marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 ili kumuwajibisha mume.
Sheria hiyo kwa sasa inatamka kwamba ni kosa la jinai kumlazimisha mwanamke kufanya tendo la ndoa bila idhini yake.
Hata hivyo, wanaharakati hao wameshauri pia kitendo cha mume kumbaka mkewe kitambuliwe kama kosa la jinai katika sheria hiyo kutokana na changamoto ya kukithiri matukio hayo kwenye ndoa.

MWANANCHI