asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,039
ningekupenda pia tatizo moyo umekufa ganzi
Tumia ubongo , achana na mambo ya moyo.
ningekupenda pia tatizo moyo umekufa ganzi
Mimi huwa namvuto Sana na Malaya , nitazungukaaa weeee ila lazima niangukie mikononi mwa mmoja wao.
ubongo natumia kusaka pesa.Tumia ubongo , achana na mambo ya moyo.
huyu anasema mkewe alimkubali mwanzoni sasa kama hamtak basi kuna ishu
it is either mkewe kagundua kwamba anauhusiano wa karibu na mzazi mwenzie so kukata mzizi wa fitina bora matatizo akayaskie kwa jiran.............iyo pia ni possible
Achaa na ww kutetea ujinga ana husiano gan angali alishakwambia mzazi mwenzake alishaolewa kitambo na ana maisha yake huko mengine.
Seek peace kwanza kabla ya kuchukua uamuzi wowote. Ukiwa katika hali ya amani na utulivu unaweza kuona kila kitu katika mwanga tofauti. Kwasasa unaweza ukachukua maamuzi ukiwa unaendeshwa na emotions na matokeo yake yakawa matatizo zaidi baadae. Hapa unaomba ushauri kwa sie tusie kujua vyema na tusiojua mazingira yako pia na tutakupa ushauri kutokana na misukumo yetu binafsi.
Zingatia tu, kuwa wewe ni Mzazi wa huyo Mtoto na ni Guardian wake hapa duniani na unawajibika katika makuzi yake kiakili na kimwili.
Zingatia pia wewe ni mume wa huyo Mama pia ni mwenzi wako kimwili na kiroho una jukumu la kumuongoza kwa kutumia busara na upendo
Zingatia pia wewe ni mtu/roho binafsi mwenye maono juu ya maisha yako na jinsi unataka kuyaendesha. Muhimu tafuta msingi mzuri wa kusimamia unapofanya maamuzi.
heheee upo dunia ya ngapi mbona kupasha viporo ndo habari ya mjini!
Nilimwambia mapema kabisa kuwa nina mtoto hata kabla ya ndoa tungali wapenzi na tukawa tunamtembelea mtoto tukiwa wote lakini baada ya ndoa akasema hawezi kulea mtoto wa mwanamke mwingine cha ajabu kuna mtoto wa dadangu nakaa nae anaishi nae vizuri tu nongwa inakuwa kwa huyu wangu.
Mtoto wangu wa kwanza ana miaka 8 nilimpata nikiwa mwaka 2 chuo ambapo kutokana na mamake kutokuwa mvumilivu kunisubiria nimalize kusoma aliamua kuolewa na kumuacha nyumbani kwao mtoto, nilipohitimu chuo na baada ya kupata kazi niliamua kumtafuta mwenza wa kuoa ambapo kabla ya yote nilimwambia ukweli kuwa nina mtoto na yeye akakubali atamlea lakini mara baada ya ndoa akanigeuka hataki kumuona mtoto huyo na kule anakokaa mtoto wanataka nimchukue.
Nimetumia kila njia imeshindikana msimamo wake ni hataki kumlea mtoto wa mwanamke mwingine, nifanyeje hapa wakuu maana nikilazimisha (uwezo huo ninao) anaweza kuwa anamtesa mtoto kipindi sipo akamsababishia matatizo ikitegemea huwa nasafiri mara kwa mara na sikai nyumbani sana na kuvunja ndoa siwezi maana ni ya kanisani na tayari tuna watoto
wengine wawili.
Ushauri wakuu
Katika wanawake elfu...unaweza ukampata mmoja tu..wa aina hiyo.....na hao walikuwa wanawake wa zamani waliokuwa wanajua uchungu wa uzazi....sio hawa wanaojifungua kwa operesheni...
Huyo mwanamke bado anabaki kuwa ni mtu mwenye roho mbaya....na ndivyo wanawake walivyo linapokuja suala la mtoto wa mwanaume kuishi na familia mpya...lazima kuwe na mushkeli....na hata hao wanaokubali kuwalea hao watoto wa kambo huwa maamuzi yao hayatoki moyoni isipokuwa wanaogopa kuvunja ndoa tu.....maamuzi yao kuwalea yanamfanya mtoto kuwa mtumwa ndani huku akifanyishwa makazi kama punda kipindi ambacho baba haupo......wanawake wanaomudu kuwalea watoto wa kambo katika malezi mazuri kwa maana ya malezi ni wachache sana...na huwa ni wale wenye hofu ya MUNGU ndani ya nyoyo zao.....hofu yao ya muumba inawafanya watambue utu wa kila kiumbe na kuuheshimu....lakini wengi wao hugeuka kuwa mashetani na kuwafanyia ushetani kuliko hata shetani mwenyewe......na hali inakuwa mbaya zaidi kama huyo mwanamke awe tasa......tumekuwa tukisikia kesi nyingi sana za mama wa kambo wakiwafanyia vitendo vya kikatili watoto zao....ukatili ambao katika hali ya kawaida hayapo kwenye ubinadamu hasa kwa malaika asiyekuwa na hatia.....na kingine kikubwa zaidi kinachofanya au kujenga dhidi ya watoto wa kambo huwa ni mali....kama mzee kidogo alikuwa ana vitega uchumi vinavyoihakikishia familia uhakika wa kupata mahitaji yote ya msingi na yale ya ziada hapo ndipo mtoto wa kambo anapotazamwa kwa jicho baya....anatazamwa kama mtu ambaye atakuja kuharibu mipango ya mirathi hasa katika mgawanyo wa mali.....na vita huwa kali mpaka wakati mwingine hupelekea watu kutoana roho....nimeshuhudia mama mmoja akiwafundisha wanae kumkana dada yao mahakamani ili hali waliishi nae nyumbani ingawa ni hivyo hivyo kimkanda mkanda......usingekuwa ushupavu wa yule dada katika kupigania haki yake asingeambulia kitu....maana yule mama alifoji mpaka document kadhaa za mali ili kujihalalishia umililki wa mali....hapo ndipo yule dada alipotambua unafki wa yule mama aliyejinadi kuwa anampenda kuliko wanawe.....na wanawake kama hawa huwa wanakubali kuishi na watoto wa ndugu kwa kuwa wanajua kuwa ni watu wa kupita tu na hata kwenye mirathi hawahusiki kwahiyo kunakuwa hakuna sababu ya chuki dhidi yao...na baada ya mgawanyo wa mali ndio ukawa mwisho wa mahusiano baina yao......katika mambo kama haya mwanaume unatakiwa uwe na msimamo wa hali ya juu sana....maana kwa kiasi kikubwa msimamo wako ndio utakaoamua hatima ya mwanao.....usipokuwa na msimamo wa kiume mwanao anaweza kuwa chokoraa na hakuna atakayejali....mwanamke hata siku hawezi kunipanda kichwani na kuniamulia mambo yangu...nikiamua kuwa mwanangu anakaa hapo nyumbani atakaa kama hataki ataondoka yeye...na ndio utakuwa ndio mwisho wa ndoa yetu......siwezi kukaa ndani na kuandalia TV ili hali sijui mwanangu anaishije huko nje eti kwa sababu ya mwanamke kasema.....siwezi kukaa baa na kula nyama nikumiza kichwa eti nikamuhifadhi wapi mwanangu wakati nina nyumba kubwa kwa sababu mwanamke kasema.....nitakuwa ni mpumbavu miongoni mwa wapumbavu......vuta picha umekaa baa na marafiki ghafla anaingia mwanao akiwa na roba la machupa ya maji akibangaiza ilihali wewe uwezo unao wa kumtunza mwanao lakini mkeo hataki.....lakini ukija nyumbani unakutana na msururu wa ndugu zake wanaokula na kusaza bure ndani ya nyumba yako huku mwanao akila kwa kuotea......jenga picha upo kwenye foleni ya barabarani ghafla anatokea mtoto anafuta kioo chako cha gari ili apate japo hela ya kununua muhindi wa kuchoma ili angalau aipitishe siku ukiinua unakuta ni mwanao.....ama kwa hakika sitayavumilia yote hayo hata iwe katika mazingira gani.....mwanangu ni mwanangu na kwangu ataishi hata kama uwe hutaki au unataka...na nikisikia habari kuwa mwanangu umemfanya kuwa kijakazi ndani ya himaya yangu...ndio utakuwa mwisho wa ndoa yetu ya kinafiki.....bora niishi bachela kuliko kuwa na mwanamke kama huyo...........UKIPENDA BOGA BASI UPENDE NA UWA LAKE..........hapo sasa unatukosea hishma wanawake tuliojifungua kwa operesheni. Aliyekwambia uchungu wa mama kwa mtoto ni yale masaa machache ya uchungu nani? Una habari kuna wanawake hawapati uchungu? Na aliyekwambia operesheni ni mteremko nani? Tumbo linalopasuliwa ni msuli wenye damu na nyama. Donda la upasuaji linauma. Tuache hayo. Usitudanganye kuwa eti wanawake wa siku hizi ndo wanachukia watoto wa kambo? Hapo juu nimekumbushia mfano wa sara mke wa ibrahim, kuna visa vya lea na rahel, tena hawa ni ndugu wa tumbo moja. Chuki chuki mpaka akaambukiza watoto mpaka wakafikia kuazimia kumuua ndugu yao wa kambo yusufu.
Watu wanatoa hukumu na solutions rahisi rahisi bila kutilia maanani complexity ya tabia ya mwanadamu. Wachache hapa wanajaribu kuangalia woga wa huyu mke na namna ya kuutafutia ufumbuzi. Molembe hapa kasema mkewe anaishi na mtoto wa wifi yake bila shida na wanapendana na wifi yake. Mimi nimeona cha kujifunza hapa. Vipi kuhusu mahusiano ya huyu mama tunayemsimanga na mama mzazi wa huyo mtoto? Huyu mke ana amani na "mke mwenzie" ingawa tunaambiwa alishaolewa?
Huyu kaka abadili approach, mke afunguke kuwa woga wake ni nini. Si ajabu kuskia Molembe si mwaminifu kwenye ndoa na mke anahisi akiruhusu kulea mtoto mmoja wa kambo huenda akaletewa mwingine na mwingine. Sijui, nasema tu. Au labda huyu mke ana wivu wa kupindukia kwa hiyo anachukia mtu yeyote anayetishia penzi lake na mumewe akiwemo mzazi mwenza katika picha ya mtoto.
Kitendo cha huyu mke kuweza kumlea mtoto wa dadake Molembe vizuri kinaonyesha huyu mke si mchoyo maana hakuna mahusiano magumu kama ya wakewenza na mawifi. Si vizuri kujumuisha kuwa wanawake ni wabaya kwa sababu tu mtu aliangukia kwenye mikono ya mama wa kambo mbaya au shemeji mbaya. Kama kuna watu walifikia hata ya kumuua mama wa kambo mbaya ili kumnusuru mtoto na baba tuichukulie hiyo kesi kipekee na hii tuichukulie kipekee maana watu na mazingira hayafanani.
Mnavyomshauri Molembe amuache mkewe wanayelea pamoja watoto watatu kwa ajili ya mtoto mmoja halafu aoe mwanamke mwingine, sijui aajiri mama wa kulea sijui kama mnajua mnachoshauri. Na huwa sioni kama ni sahihi kulinganisha mke/mume na mtoto kwa kusema mtoto ni muhimu zaidi kuliko mwenza. Hakuna wa muhimu zaidi ya mwingine. Kila mmoja ana nafasi yake ya kipekee, na ndo maana Molembe hapa anamtaka mke na anamtaka mtoto.
Kwamba Molembe amekosa "control" kwa mkewe siamini kama ni kweli. Na kama control hapa inamaanisha kufanya maamuzi ya kimabavu basi kuna shida. Uwezo wa kufanya maamuzi kimabavu anao, lakini itakuwa kwa gharama ya nani? Ya mtoto. Anachotaka ni njia mbadala itakayohakikisha usalama wa mtoto, na mimi naongeza, usalama wa mke.
Molembe mama mzazi wa huyo mwanao yuko wapi? na nini ilikuwa sababu ya wewe kutoishi nae? Zipi ni tabia za huyo mwanao? Unadhani unawajibu kwa mkeo na huyo mwanao? kama ndio ni upi? Ukianza kuleta majibu ya haya maswali machache naweza kukusaidia ufikirie zaidi kuliko kukushauli.
nimewah kukutana na hali kama hii kwa ndg wa karibu ndo mana nasema huyu kuna kitu anaficha hapa
Huyo mwanamke bado anabaki kuwa ni mtu mwenye roho mbaya....na ndivyo wanawake walivyo linapokuja suala la mtoto wa mwanaume kuishi na familia mpya...lazima kuwe na mushkeli....na hata hao wanaokubali kuwalea hao watoto wa kambo huwa maamuzi yao hayatoki moyoni isipokuwa wanaogopa kuvunja ndoa tu.....maamuzi yao kuwalea yanamfanya mtoto kuwa mtumwa ndani huku akifanyishwa makazi kama punda kipindi ambacho baba haupo......wanawake wanaomudu kuwalea watoto wa kambo katika malezi mazuri kwa maana ya malezi ni wachache sana...na huwa ni wale wenye hofu ya MUNGU ndani ya nyoyo zao.....hofu yao ya muumba inawafanya watambue utu wa kila kiumbe na kuuheshimu....lakini wengi wao hugeuka kuwa mashetani na kuwafanyia ushetani kuliko hata shetani mwenyewe......na hali inakuwa mbaya zaidi kama huyo mwanamke awe tasa......tumekuwa tukisikia kesi nyingi sana za mama wa kambo wakiwafanyia vitendo vya kikatili watoto zao....ukatili ambao katika hali ya kawaida hayapo kwenye ubinadamu hasa kwa malaika asiyekuwa na hatia.....na kingine kikubwa zaidi kinachofanya au kujenga dhidi ya watoto wa kambo huwa ni mali....kama mzee kidogo alikuwa ana vitega uchumi vinavyoihakikishia familia uhakika wa kupata mahitaji yote ya msingi na yale ya ziada hapo ndipo mtoto wa kambo anapotazamwa kwa jicho baya....anatazamwa kama mtu ambaye atakuja kuharibu mipango ya mirathi hasa katika mgawanyo wa mali.....na vita huwa kali mpaka wakati mwingine hupelekea watu kutoana roho....nimeshuhudia mama mmoja akiwafundisha wanae kumkana dada yao mahakamani ili hali waliishi nae nyumbani ingawa ni hivyo hivyo kimkanda mkanda......usingekuwa ushupavu wa yule dada katika kupigania haki yake asingeambulia kitu....maana yule mama alifoji mpaka document kadhaa za mali ili kujihalalishia umililki wa mali....hapo ndipo yule dada alipotambua unafki wa yule mama aliyejinadi kuwa anampenda kuliko wanawe.....na wanawake kama hawa huwa wanakubali kuishi na watoto wa ndugu kwa kuwa wanajua kuwa ni watu wa kupita tu na hata kwenye mirathi hawahusiki kwahiyo kunakuwa hakuna sababu ya chuki dhidi yao...na baada ya mgawanyo wa mali ndio ukawa mwisho wa mahusiano baina yao......katika mambo kama haya mwanaume unatakiwa uwe na msimamo wa hali ya juu sana....maana kwa kiasi kikubwa msimamo wako ndio utakaoamua hatima ya mwanao.....usipokuwa na msimamo wa kiume mwanao anaweza kuwa chokoraa na hakuna atakayejali....mwanamke hata siku hawezi kunipanda kichwani na kuniamulia mambo yangu...nikiamua kuwa mwanangu anakaa hapo nyumbani atakaa kama hataki ataondoka yeye...na ndio utakuwa ndio mwisho wa ndoa yetu......siwezi kukaa ndani na kuandalia TV ili hali sijui mwanangu anaishije huko nje eti kwa sababu ya mwanamke kasema.....siwezi kukaa baa na kula nyama nikumiza kichwa eti nikamuhifadhi wapi mwanangu wakati nina nyumba kubwa kwa sababu mwanamke kasema.....nitakuwa ni mpumbavu miongoni mwa wapumbavu......vuta picha umekaa baa na marafiki ghafla anaingia mwanao akiwa na roba la machupa ya maji akibangaiza ilihali wewe uwezo unao wa kumtunza mwanao lakini mkeo hataki.....lakini ukija nyumbani unakutana na msururu wa ndugu zake wanaokula na kusaza bure ndani ya nyumba yako huku mwanao akila kwa kuotea......jenga picha upo kwenye foleni ya barabarani ghafla anatokea mtoto anafuta kioo chako cha gari ili apate japo hela ya kununua muhindi wa kuchoma ili angalau aipitishe siku ukiinua unakuta ni mwanao.....ama kwa hakika sitayavumilia yote hayo hata iwe katika mazingira gani.....mwanangu ni mwanangu na kwangu ataishi hata kama uwe hutaki au unataka...na nikisikia habari kuwa mwanangu umemfanya kuwa kijakazi ndani ya himaya yangu...ndio utakuwa mwisho wa ndoa yetu ya kinafiki.....bora niishi bachela kuliko kuwa na mwanamke kama huyo...........UKIPENDA BOGA BASI UPENDE NA UWA LAKE..........
Achaa na ww kutetea ujinga ana husiano gan angali alishakwambia mzazi mwenzake alishaolewa kitambo na ana maisha yake huko mengine.
relax mumie!!!!!!!!!!!yani kaniumiza!
mi opereshen imenilaza miezi mitatu chini siwezi hata kubeba mwanangu vizuri halafu kuna mtu anawaza kujifungua kwa opereshen ni starehe fulani hivi ambayo inafanya tendo la kuleta kiumbe duniani liwe la kubezwa?
dah!
Hapo kwa red ndo huwa mnachanganya madesa wanawake, hivi unafikiri huyo mtoto kwa kukaa huko ndo hana haki kwenye mali za baba yake??? mnadanganyanaga sana khs hili, sikulaumu manake nimeona wanawake wengi wanakuwaga na mawazo kama haya - wanadhani asipo kuja kuishi hapo eti hana haki kwenye mali, weeee!!!
nahisi hata mke wa jamaa ana mawazo hayo, ndo maana mi naamini kuna zaidi ya kusema eti hawezi kulea mtoto wa mwanamke mwingine