gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,714
nyokooo........Acha ubishi , main object ndiyo hiyo mtoto amekataliwa.
yeye alikuwaje akapata mashtuzi?
nyokooo........Acha ubishi , main object ndiyo hiyo mtoto amekataliwa.
aisee i wish to hear the other side of the story before giving my comments
nyokooo........
yeye alikuwaje akapata mashtuzi?
hata mimi nahisi kuna zaidi kilichojificha upande wa pili, siamini hilo jibu jepesi eti hataki kulea mtoto wa mke mwingine wakati alijua before
Binadamu ni vigeugeu tu , kwahiyo ndiyo atumie njia hiyo kumuadhibu?
Hlf hapo toka amuoe mpaka wanapata watoto wawili walikuwa hawakai na huyo mtoto mkubwa.
Wanawake wa zama hizi mnalegezewa legezewa ndiyo maana mnaota mapembe.
Toa mfano wa sababu ya mtu kuweza kumkataa mtoto.mleta mda hajaleta hoja za kuridhisha manake haiingii akilini eti mke amkatae mtoto ambaye tayari alikuwa kesha ambiwa uwepo wake kirahisi hivi
am telling you huyu mleta mda kuna vitu anatuficha na kwasabb nina experience ya scenario kama hii kwa my own brother ndo mana nakomaa adi mwisho
huyu anasema mkewe alimkubali mwanzoni sasa kama hamtak basi kuna ishu
it is either mkewe kagundua kwamba anauhusiano wa karibu na mzazi mwenzie so kukata mzizi wa fitina bora matatizo akayaskie kwa jiran.............iyo pia ni possible
Iko vizur hii ila sijui kama atawezaMuambie mkeo unahama hapo ukatafute nyumba ukae na mwanao. Yeye mtakuwa mnatembeleana kama mtu na bf wake. gfsonwin, namaanisha hapo sio utani. Hivi wewe kama mtu kakukuta na mwanao na mnaoana anajua huyo ni mwanao. Then anakuambia simtaki huyu mtoto ungefanyaje? I would have done exactly that
Mtoto wangu wa kwanza ana miaka 8 nilimpata nikiwa mwaka 2 chuo ambapo kutokana na mamake kutokuwa mvumilivu kunisubiria nimalize kusoma aliamua kuolewa na kumuacha nyumbani kwao mtoto, nilipohitimu chuo na baada ya kupata kazi niliamua kumtafuta mwenza wa kuoa ambapo kabla ya yote nilimwambia ukweli kuwa nina mtoto na yeye akakubali atamlea lakini mara baada ya ndoa akanigeuka hataki kumuona mtoto huyo na kule anakokaa mtoto wanataka nimchukue.
Nimetumia kila njia imeshindikana msimamo wake ni hataki kumlea mtoto wa mwanamke mwingine, nifanyeje hapa wakuu maana nikilazimisha (uwezo huo ninao) anaweza kuwa anamtesa mtoto kipindi sipo akamsababishia matatizo ikitegemea huwa nasafiri mara kwa mara na sikai nyumbani sana na kuvunja ndoa siwezi maana ni ya kanisani na tayari tuna watoto
wengine wawili.
Ushauri wakuu
Du.
Nyie watoto wa kiume siku hizi hamtaki kabisa jukumu la kuwa kichwa cha familia. Mnakimbilia always the easy way out!!!!
Sijui labda na mie kwa kuwa ni mwanamke naside na huyu mama kabisa!!!!
Kulea mtoto wa mwenzio kunahitaji mkataba wa ziada zaidi ya kile kiapo cha wakati wa kufunga ndoa.
Mimi nilipitiwa na hio kitu. Wakati wa mwanzo kabisa niliambiwa kuhusu mtoto wa alikuwa mume wangu.
Nilitafakari sana. Sema kwa kuwa mm tangu mwanzo sikuwa na mpango wa kuolewa nilitaka kulea mtoto anaeteseka kama yatima au vitu kama hivyo so haikuwa shida kukubali aje home alihamia immediately tuliporudi toka honeymoon tulimkuta home. Na ilikuwa makubaliano kabla ya ndoa.
Baada hapo ni shukrani kwa Mungu, majaribu ya shtani, woga, kukata tamaa, kufurahi sana. Namuita mtoto wa bonus. Tunamuita baraka kimoyomoyo.
Ila ni mtihani kutisha unaohitaji sala ila ni baraka kubwa ya ziada!! I would mot change a thing!!
Wanangu wana kaka mkubwa anawachemsha wanaacha kudeka. Mama yake mzazi yupo na wanapendana kama inavyopasa mzazi na mtoto. Huwa namuambia amshukuru Mungu kwa kupewa mama wawili wanaompenda.
Acha woga simama kiume fanya maamuzi kubali ulichemsha ujanani omba samahani tambua ndoa yako tambua udhaifu na woga wake msaidie usimshangae wala kumhukumu kwa kosa lako mwenyewe mtoto alelewe kama mtoto mwenye baba na mama.
Kuwa wazi kwa mkeo kuhusu mali zinazoitwa za ndoa yenu. Huyu ana nafasi gani? Uwazi utakuweka huru.
ukikosa pa kumpeleka na roho yako ikakubali nipe huyo mtoto kama ni wa kike nimpeleke kwa mama yangu. Kwa shart moja tu,
ukubali asome shule ya kawaida ya pale nyumbani lengo ni kwamba awe karibu na mama na malezi bora. Yaan aende shule jion arudi nyumbani.
Matunzo atapata pale kwetu akimaliza drs la saba ataamua yeye ukijiskia kutuma matumzo ni juu yako tho sio lazima na ada ya primary na matunzo yote atapata home.
Nyumban atakaa kama mdogo wetu na si mfanyakazi, mfanyakazi yupo.
Ukijiskia njoo pm.
Iko vizur hii ila sijui kama ataweza
Ngumu dada@mankam maana nikimuacha itabidi nichukue watoto na nioe mwanamke mwingine je, yeye hatawatesa atawalea kama watoto na yeye akikataa kulea hao watoto(ujue hapa watakuwa watatu) nimuache??
Ngumu aisee
Nilimwambia mapema kabisa kuwa nina mtoto hata kabla ya ndoa tungali wapenzi na tukawa tunamtembelea mtoto tukiwa wote lakini baada ya ndoa akasema hawezi kulea mtoto wa mwanamke mwingine cha ajabu kuna mtoto wa dadangu nakaa nae anaishi nae vizuri tu nongwa inakuwa kwa huyu wangu.
aisee i wish to hear the other side of the story before giving my comments