Mwanamke kamkataa mtoto wangu

Mwanamke kamkataa mtoto wangu

Tuacheni longolongo wakuu, hivi kuna mwanaume wa kumlea mtoto wa mwanaume mwenzake hapa?
nyie ndo wa kwanza kabisaa " kama unataka ndo na mimi, huyo mtoto mrudishe kwa baba yake kwanza"
kumbe linauma eee?
 
Nifanyaje sasa maana huyu mwenzenu hataki kabisa kukaa na huyo mtoto nimeshawishi nimeshindwa na kutumia nguvu naweza ila sasa si atamnyanyasa.

Kaka mama mzazi yupo?
Una kinadada wangapi?

Fanya hiv, huyo dada unaemlelea mtoto wake mpe wako naye!!
Lengo ni mkeo atambue lengo ni kulea mtoto nasi vinginevyo

Au mpeleke mtoto boarding likizo kwa bibi zake kokote atakako yeye!!

Coz hata kama maneno yapo kwamba atamtesa nilidhan kuwafumba midomo ilitakiwa amchukue, but what I see huyo alitaka ndoa tu!
 
Mkeo sio ndugu yako,Mwanao huwezi achana nae abadani, kwa kutambua hili , utajua nn cha kufanya.

Mpe option hii, mtoto aje nyumbani au yeye aondoke....achague moja hapo....then msikilizie atajibu nini...mwanaume lazima uwe na msimamo kaka.

achana na huyo mwanamke hakufai

Sikiliza,ndugu yako ni mtoto na si mkeo,ndoa ya kanisani ni bora kuliko mwanao?
Chukua mwanao ukae nae,hataki aondoke yeye akuachie watoto wako,utatafuta hata hg akuangalizie watoto.
Kwanza dogo mkubwa hyo,lini atapata mapenzi toka kwako,baadae atakukana hyo kwamba hukumlea.
Wanawake wapo tu,lakini huwezi jua hyo mwanao mola kampangia riziki gani.

Huyo mtoto mpeleke kwa mama yako kama yupo hai, baadhi ya wanawake wanaakili finyu sana hawezi kumkataa mtoto aliyemkuta ila kama umemzaa ukiwa na uhusiano nae hapo anahaki yakukataa. usimlazimishe kumlea asije kumnyanyasa tu mtoto. natamani umwache na yeye ili aone uchungu wa mtoto wa mtu.

Mtoto wangu wa damu nisikae nae kisa mwanamke?solution ni moja tuu aondoke nikae na mtoto wangu, kwa namna anavyoonyesha ana roho mbaya?hata akikubali sasa umlete siyo wa kumuamini tena

Kwani kakuzalia watoto wangap mpaka hanakupelekesha kama mburura?!?!piga chini,be a man,act like a boss.


Wanawake tuna kazi sie...
Unakubali vipi kuolewa na mwanaume mwenye mtoto huku unajua kabisa huwezi kulea?

Na mnaomshauri amuache mkewe mnadhani ni rahisi tu? Ingekua rahisi kwake nadhani angeshafanya.
Dhambi ya wazazi inamtesa mtoto asie na hatia na ataitwa sana Mwanaharamu...
Mbaya sana.
 
Pole kaka,me mke wangu nilimueleza before na juzi mtoto kaletwa nyumban wala hakuna kelele kabisa,akina wifi walishaanza kusema hawez kumlea ingawa walikuwa wananiambia mm kwa pembeni,ni kwasabab hawajui nini tuliongea na wife kabla hata mtoto hajaletwa home
 
Tuacheni longolongo wakuu, hivi kuna mwanaume wa kumlea mtoto wa mwanaume mwenzake hapa?
nyie ndo wa kwanza kabisaa " kama unataka ndo na mimi, huyo mtoto mrudishe kwa baba yake kwanza"
kumbe linauma eee?

Mwanaume kukataa kulea mtoto ni sawa maana mtoto yupo upande wa mme lakini mwanamke inakuwa ngumu.
 
Mue mnatulia nyakati zingine. Ona sasa mtoto hana hatia mnataka kumpa shida. Mtufute mama yake mzazi umueleze. Kama yeye ataona ndoa yake itakuwa mashakani hata wewe pia mwambie ndiyo yako ipo mashakani. Kwani mama ndiyo mlezi mzuri sana wa mtoto kuliko hata baba. Baba ni mzuri kwenye kuhudumia.
 
ntakupa mfano hai... ndugu yangu wa damu alikumbwa na mkasa kama unaofanana na wako....yeye alioa na kuzaa mtoto mmoja kisha mkewe kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari...kaka akabaki na yule mtoto akilea mwenyewe mpaka akafikisha miaka 5 (mama alifariki mtoto akiw ana mwaka mmoja)...baada ya hapo kaka akaamua kuoa tena...lakini kabla ya zoezi hilo alimtaarifu mke mtarajiwa kuwa ana mtoto na akamweleza kila kitu (kama ulivyofanya mleta mada kwa huyo mkeo)....mke mtarajiwa wa bro alikubali kumtunza mtoto kama mwanae...kabla ya ndoa kufungwa nami nikiwa likizo huko nyumbani kaka alinieleza hayo na pia shemeji yangu mtarajiwa aliitwa na nikatambulishw apale kisha kaka akarudia maneno yale mbele ya mke mtarajiwa na mbele yangu...yule shemeji alionekana kuwa mpole na mstarabu kweli....

ndoa ikafungwa na wakaanza kuishi pamoja...mambo yakabadilika ..shemeji akaanza kuonyesha hisia hasi dhidi ya yule mtoto..akaanza kumnyima chakula akitoka shule...anampiga na kisha anamzuia kumweleza baba yake....kaka yangu alibaini kuwapo kwa hali hiyo baada ya kuona mtoto amebadilika sana...akafanya utafiti akabaini ukweli...akanishirikisha mdogo wake tukashauriana kuwa ampeleke boarding....kijana akamishiwa boading..bado mke wa bro akawa na tabia hasi dhidi ya mtotoo...wakati wa likizo mtoto akirudi home hali ile ya awali inarudi ya manyanyaso nk....

siku moja mtoto akiwa shule shemeji akaenda kumtembelea huko...kuna zawadi alimpelekea ikiwapo na chakula lakini chakula kile alikitia sumu...wakati akiongea na mtoto alimpa chakula akala na alipomaliza kula yeye aliaga na kuondoka haraka sana shuleni....huku nyuma mtoto akaanza kuumwa na hali ikawa mbaya...walimu wakashangaa kuona mara baada ya mama kuondoka mtoto amenza kuumwa..wakampa tiba ya kwanza kisha wakampeleka hosp..taarifa zikafika kwa mume ...akaenda hospitali mtoto alikuwa na hali mbaya sana..akapiga simu kwa mke wake haikupatikana...akarnda nyumbana akakuta hayupo....akarudi hosp kuendelea kumuuguza mtoto....

alinipigia simu na kunijulisha yote...nilipandwa na hasira na uchungu mkubwa sana..nikasafiri hadi huko nyumbani, wakati huo mtoto alikuw akeshatoka hosp...tukampeleka kwa wazaz wetu (babu na bibi yake) ....kisha tukapitiliza hadi kwao shemeji(mke wa bro) huko kilimanjaro..hatukumkuta kwao...ikabainika yuko kwa shangazi yake tukaenda kule....wazazi wake na sisi pamoja na yeye na ndugu wengine tukakaa na kumuuliza kwa nini alikusudia kumuua mtoto...hakutoa majibu yoyote isipokuwa alikuw analia na kuomba asamehewe......eti shetani alimpitia...

nilikaa na kaka yangu kama watu wazima tukashauriana na kufikia mwafaka kuwa abaki kwao....sisi tukarudi ..ndani ya moyo wangu nilikuwa na azimio lingine ambalo sikutaka kumweleza kaka yangu wala mtu mwingine yeyote....nikakaa kimya...

yule shemeji akarudi kwa mumewe baada ya miezi kama miwili hivi wakati huo mimi nilikuwa nimekwisharudi kazini...kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 nilirudi tena nyumbani na kukuta hali ya maisha ya kaka yamebadilika sana kaka amekuwa kama mjinga mjinga hivi...mke katawala nyumba na kila kitu kaka hana usemi wowote...

nikamwambia hukufunga ndoa kanisani ili uteseke na maisha yako yawe ya manung'uniko namna hii....ulioa ili uishi kwa upendo na furaha lakini si katika hali hii...kakayangu hakunielewa kabisa maana alikuwa tayari amekuwa kama chizi hivi....ili kuokoa maisha ya ndugu yangu na mwanawe na kwa ustawi mkubwa wa ukoo wetu na kwa kuangalia historia ya madhira aliyoyaleta yule mke wa kaka yangu ...she was configured and given a permanent resting place.....

mleta mada....the future and the destine of ur kid is in ur hands.....show ur wife that u are in control...mtoto wako hawezi kuteseka na kupata maisha mabaya na hata wewe eti kisa ndoa ya kanisani..(my foot).....unadhani hatima ya yule mtoto ni nini kama sio mabaya kumkuta....

lazima uwe baba mwema na mume mwangalifu
 
kwanin ung'ang'anie the other side of a story? What if thats a plain truth? Can't you give your comment though?
nimewah kukutana na hali kama hii kwa ndg wa karibu ndo mana nasema huyu kuna kitu anaficha hapa
 
Nimeshuhudia mama kambo akimnyanyasa mtoto naogopa sana sipendi mtoto anyanyaswe muda mwingi sipo nyumbani nasafiri mara kwa mara.
Una nia kweli ya kumchuka mtotio wako? Sijui kwa nini naona kama Mke wako anakucontrol. Kama alijua kuwa una motto na mlikubaliana mtamchukua ilikuwa tu kumuarifu kuwa mwezifulani namuendea motto wetu na kumpa warning kuwa asije mtesa mototo wako. Japo namshangaa huyo aliyeolewa na kumuacha mtoto wake!!!!!!!
 
Mkuu de'levis mkasa wa kaka yako umenisikitisha sana, ila kwa uzoefu wangu huyo mwanamke alitaka kumuua huyo mtoto ili asiwe kwenye list ya wenye haki na mali za baba
 
Last edited by a moderator:
asie... mtt hana kosa..ana ak ya kupewa malez nawe km baba!! cc wanawake somtm n mbwa sn... uawezaje kumkana mtt amby umemkuta??? mkumbushe huyo mtt alpatkana kabla ata yy hamjafahamiana... mchukue mwanao... km upo vzr kiuchum...mpeleke boardng schools za academy...lkz c vby ukawa nae...n kw muda tu.. huyo mkeo ana roho mbaya
 
Una nia kweli ya kumchuka mtotio wako? Sijui kwa nini naona kama Mke wako anakucontrol. Kama alijua kuwa una motto na mlikubaliana mtamchukua ilikuwa tu kumuarifu kuwa mwezifulani namuendea motto wetu na kumpa warning kuwa asije mtesa mototo wako. Japo namshangaa huyo aliyeolewa na kumuacha mtoto wake!!!!!!!

Mkuu unawajua wanawake kweli nikilazimisha yanaweza tokea mengine.
 
asie... mtt hana kosa..ana ak ya kupewa malez nawe km baba!! cc wanawake somtm n mbwa sn... uawezaje kumkana mtt amby umemkuta??? mkumbushe huyo mtt alpatkana kabla ata yy hamjafahamiana... mchukue mwanao... km upo vzr kiuchum...mpeleke boardng schools za academy...lkz c vby ukawa nae...n kw muda tu.. huyo mkeo ana roho mbaya

Mkuu mbna kma unamwogopa mkeo chukua mtoto wko ishi nae nyumbani kwako hiyo ni damu yko act like a man,wewe ndio kichwa cha familia huyo mke wko inaonekana ananguvu kuliko wewe au yuko loaded nini
 
Una nia kweli ya kumchuka mtotio wako? Sijui kwa nini naona kama Mke wako anakucontrol. Kama alijua kuwa una motto na mlikubaliana mtamchukua ilikuwa tu kumuarifu kuwa mwezifulani namuendea motto wetu na kumpa warning kuwa asije mtesa mototo wako. Japo namshangaa huyo aliyeolewa na kumuacha mtoto wake!!!!!!!

Jamaa itakua anamwogopa mkewe hivi damu yako kwanini iteseke wakati wewe upo hai,mtoto wko anapaswa kuishi nawe nyumba 1 unachokula baba n mtoto anakula hichohicho,mwanaume unatakiwa kua n msimamo inaonekana mkewe ananguvu ndani y nyumba kuliko baba hpo iko shida
 
Utakuwa umeoa jini bro...kwani unadhani ndoa ni kifungo cha maisha au pete inakuzingua? Kila mtu achukue 50 zake na kila mmoja apite zake vile...wala sio dhambi
 
Hivi ni mtandao upi wa kijamii huwa nakuta mada kama hizi?
Wanaume wanashawishiana na kukatazana kulea mtoto aliemkuta kwa mkewe?
Nadhani sio jamiiforums.
Hhahahshhahahahahahaha sio huu banaaaaa!
itakuwa mtandao wa kwenu Kisiju huko!
hahahhahhh mwe umeniwacha hoi!
hakyamama sio humu!
 
mpeleke kwa ndugu zako kwanza

ila akienda si atajua unamtumi pesa na kumtunza, hakikisha kuwa haumleti home hata akijifanya anataka aishi nae sasa...ni uongo wivu unakuja kuwa unampa pesa so ukimleta atamtesa sana.
 
Mkuu huna maosa kabisa kwenye hili. Ulikuwa muwazi na kumwambia ukweli huyo mkeo kwamba una mtoto na yeye kuonyesha hana tatizo kwenda kumtembelea mkiwa pamoja na hata kukubali kumlea kama mkioana. Sasa iweje tena baada ya kufunga pingu za maisha ayageuke makubaliano yenu ya nyinyi kama mke na mume kuishi na mtoto wako ambaye ulimpata kabla ya kuwa naye? Weka msimamo unaoeleweka ili arudi kwenye mstari kuhusu makubaliano yenu, hataki piga chini kwani waswahili walisema damu ni nzito kuliko maji.

Nilimwambia mapema kabisa kuwa nina mtoto hata kabla ya ndoa tungali wapenzi na tukawa tunamtembelea mtoto tukiwa wote lakini baada ya ndoa akasema hawezi kulea mtoto wa mwanamke mwingine cha ajabu kuna mtoto wa dadangu nakaa nae anaishi nae vizuri tu nongwa inakuwa kwa huyu wangu.
 
Wanawake wana roho mbaya sana....yalishanikuta wakati nipo mdogo....na nikafanya maamuzi magumu...na mpaka leo nipo huru....lakini bado nasisitiza wanawake wana roho mbaya sana....nahisi huwa wanatumia ndude zao kufikiria na kufanya maamuzi badala ya vichwa....katika kesi kama hizi mwanaume unatakiwa usimame kidete haswaaa....la sivyo mwanao ataishia kuwa chokoraaa.....nimejifunza mengi sana kwa mama wa kambo....na nimepata kuwajua wanawake vizuri kwa kuwa mwalimu wao ni mmoja na roho zao zinafanana....chonde chonde ndugu usimtupe mwanao kwa sababu ya mwanamke...mtoto ni damu yako na mwanamke ni mpita njia tu kwenye maisha yako.....kwanza una uhakika kama hao waliopo nyumbani ni wa kwako kweli au amebambikia tu...nenda kapime DNA....wanawake wenyewe wa miaka hii hawaaminiki ndugu.....inakubidi uishi nao kimachale machale....mguu nje mguu ndani..muda wowote anaweza akawekea sumu kwenye msosi ili wewe ufe na yeye akaishi na bwana mwingine.....unaweza ukaona ni jinsi gani hawa wenzetu walivyo na akili ndogo....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom