Mwanamke kamkataa mtoto wangu

Mwanamke kamkataa mtoto wangu

Mtoto wangu wa kwanza ana miaka 8 nilimpata nikiwa mwaka 2 chuo ambapo kutokana na mamake kutokuwa mvumilivu kunisubiria nimalize kusoma aliamua kuolewa na kumuacha nyumbani kwao mtoto, nilipohitimu chuo na baada ya kupata kazi niliamua kumtafuta mwenza wa kuoa ambapo kabla ya yote nilimwambia ukweli kuwa nina mtoto na yeye akakubali atamlea lakini mara baada ya ndoa akanigeuka hataki kumuona mtoto huyo na kule anakokaa mtoto wanataka nimchukue.

Nimetumia kila njia imeshindikana msimamo wake ni hataki kumlea mtoto wa mwanamke mwingine, nifanyeje hapa wakuu maana nikilazimisha (uwezo huo ninao) anaweza kuwa anamtesa mtoto kipindi sipo akamsababishia matatizo ikitegemea huwa nasafiri mara kwa mara na sikai nyumbani sana na kuvunja ndoa siwezi maana ni ya kanisani na tayari tuna watoto
wengine wawili.

Ushauri wakuu

Kama mwanaume haupaswi kuomba ushauri kwa hili. Chamsingi Fanya maamuzi ambayo kwako utahisi yana usahihi.
Mwenza unaweza ukamtafuta mwingine, lakini mtoto wako huwezi ukamtafuta mwingine, Thaminisha mtoto na mke/ mume then unaweza ukapata jibu sahihi.
Mtazamo wangu ni, Kama mke/ mume hampendi mwanao hapo maanayake huyo mwenza wako hakufai.
Over....
 
hana option ya kutoa aseme ukweli tatizo limetokana na nini??
mkewe hawez kukurupuka tuu kumkataa mtt alomkuta ndoan
gfsonwin, wapo wanawake/ wanaume wanao wakataa watoto wanano wakuta kabla ya kufunga ndoa.
Binafsi nilikutana na mchumba na nilipo mwambia ninao watoti mapacha, alinijibu yehawezi.
Na hapo niliamua kukata mawasiliano na yeye.
Over...
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke hata aolewe na nani hakubali kimwacha mwanawe,sasa wewe unakuaje unamuacha mwanao?
Uwezo unao kwa nini usikae nae? Kama hataki atimue
utawalea ndugu zake wewe mwanao hayupo hapo.
Chagua mke ai mtoto?
Nakusuikitikia sana ndugu,wanawake ni wabinafsi sana.
 
Nimeshuhudia mama kambo akimnyanyasa mtoto naogopa sana sipendi mtoto anyanyaswe muda mwingi sipo nyumbani nasafiri mara kwa mara.

utawajua wanaotegeshea ndoa.
Anyway peleka mtoto boading, akifunga shule akae kwako week siku zilizobaki mpeleke kwa dada yako. Kwan wew hauna mama?
 
Mtoto wangu wa kwanza ana miaka 8 nilimpata nikiwa mwaka 2 chuo ambapo kutokana na mamake kutokuwa mvumilivu kunisubiria nimalize kusoma aliamua kuolewa na kumuacha nyumbani kwao mtoto, nilipohitimu chuo na baada ya kupata kazi niliamua kumtafuta mwenza wa kuoa ambapo kabla ya yote nilimwambia ukweli kuwa nina mtoto na yeye akakubali atamlea lakini mara baada ya ndoa akanigeuka hataki kumuona mtoto huyo na kule anakokaa mtoto wanataka nimchukue.

Nimetumia kila njia imeshindikana msimamo wake ni hataki kumlea mtoto wa mwanamke mwingine, nifanyeje hapa wakuu maana nikilazimisha (uwezo huo ninao) anaweza kuwa anamtesa mtoto kipindi sipo akamsababishia matatizo ikitegemea huwa nasafiri mara kwa mara na sikai nyumbani sana na kuvunja ndoa siwezi maana ni ya kanisani na tayari tuna watoto
wengine wawili.

Ushauri wakuu

ukikosa pa kumpeleka na roho yako ikakubali nipe huyo mtoto kama ni wa kike nimpeleke kwa mama yangu. Kwa shart moja tu,

ukubali asome shule ya kawaida ya pale nyumbani lengo ni kwamba awe karibu na mama na malezi bora. Yaan aende shule jion arudi nyumbani.

Matunzo atapata pale kwetu akimaliza drs la saba ataamua yeye ukijiskia kutuma matumzo ni juu yako tho sio lazima na ada ya primary na matunzo yote atapata home.

Nyumban atakaa kama mdogo wetu na si mfanyakazi, mfanyakazi yupo.

Ukijiskia njoo pm.
 
Hao watoto wanageuka shubiri mzazi wakiume akitoweka duniani..huwo mkeo anautazama mwishowake na watoto wake.
 
Huyo mtoto mpeleke kwa mama yako kama yupo hai, baadhi ya wanawake wanaakili finyu sana hawezi kumkataa mtoto aliyemkuta ila kama umemzaa ukiwa na uhusiano nae hapo anahaki yakukataa. usimlazimishe kumlea asije kumnyanyasa tu mtoto. natamani umwache na yeye ili aone uchungu wa mtoto wa mtu.
 
Unaambiwa ukipenda boga penda na ua lake, kama mkeo anakupenda kwa dhati hawezi kuikataa damu yako hasa kama alitambua hilo tangu awali, hapo kuna tatizo kama hawez kuishi na mwanao which means hataweza kuishi na ndugu yako yoyote (common kwa familia za kiafrika ) au hata mzazi wako akiugua hatoweza kaa nae amsaidie, na ujue kua kwa tabia yake hiyo hata
Mama yako mzazi akitoka kijijin kuja mjini kwa matibabu atafukuzwa kama itamlazimu kufikia kwako .
Kuepukana na hayo kuwa na msimamo mlete nyumban hataki kumlea aondoke maana hakuna namna nyingine ,huwez acha mwanao anatanga tanga we ule bata mjini.
Ukimleta hakikisha unakuwa makini kuona anapata matunzo sawa na wanao wa ndoani kwani wote ni sawa, dhambi yako ya ujanani isimtafune mtoto.
Mwambie mkeo atambue harusi ni zaidi ya kuvaa shela na kupigiwa matarumbeta kuna majukumu mazito baada ya matarumbeta kunyamaza na watu kuvunja kamati.
 
Haya mambo simepesi kama mnavochangia .. Ogopa sana MTU asiekua na upendo.. Ni muuuaji alishaonyesha hayuko tayari .. Ni mbinsfsi atambagua tu mtoto haya kama utalazimisha.. Muache huko aliko mpaka ajitabue... Ndo aje nyumbani... Nlisha baguliwa mtoto nlifedheka sana.....
 
Mtoto wangu wa damu nisikae nae kisa mwanamke?solution ni moja tuu aondoke nikae na mtoto wangu, kwa namna anavyoonyesha ana roho mbaya?hata akikubali sasa umlete siyo wa kumuamini tena
 
Ndugu zangu hawana matatizo na sijawahi kuyaona halafu huyu mwanamke anampenda huyu mtoto wa dadangu sana na wako karibu sana na huyo dadangu kuhusu ugomvi wa familia haupo kabisa.

aisee i wish to hear the other side of the story before giving my comments
 
gfsonwin, wapo wanawake/ wanaume wanao wakataa watoto wanano wakuta kabla ya kufunga ndoa.
Binafsi nilikutana na mchumba na nilipo mwambia ninao watoti mapacha, alinijibu yehawezi.
Na hapo niliamua kukata mawasiliano na yeye.
Over...

huyu anasema mkewe alimkubali mwanzoni sasa kama hamtak basi kuna ishu
it is either mkewe kagundua kwamba anauhusiano wa karibu na mzazi mwenzie so kukata mzizi wa fitina bora matatizo akayaskie kwa jiran.............iyo pia ni possible
 
Kwani kakuzalia watoto wangap mpaka hanakupelekesha kama mburura?!?!piga chini,be a man,act like a boss.
 
Mlee mwanao

Ila mfatilie kwa ukaribu maana kuna wanawake magaidi

Na pia chunguza nini kimetokea hadi amkatae mtoto sasa
 
Kwani kakuzalia watoto wangap mpaka hanakupelekesha kama mburura?!?!piga chini,be a man,act like a boss.

Mkuu unaona hilo ni suluhisho kweli nitakaemuoa tena akiwakataa nimuache.
 
Ndoa ni nini bila mapenzi?

Kama alikuahidi kulea mwanao halafu sasa kagauka, mkeo si mwaminifu kwa mengi sana usiyoyajua.

Wanaokushauri utelekeze mwanao kisha umwacho mkeo afurahie ndoa yake, hata maana ya furaha ya ndoa hawajui.
Mwanamke hawezi kufurahia ndoa na mwanamme anayehuzunikia ndoa. Furaha ya ndoa ni amani kwa wote wawili, si mmoja kufurahia mateso ya mwenzie.

Mtoto ni wako na huwezi kumpatiliza mateso ya maisha kwa makosa yako. Nina imani huyu mke uliyenaye ni superior kuliko wewe kwa mambo mengi na nyote wewe na yeye mnalijua hilo. Na kama hawezi kutumia superiority yake kukukamilisha, anataka uwe mtumwa, hiyo si ndoa na believe me ana lengo lingine likitimia hayuko nawe. Ukristo si kwenye ndoa tu, bali ni maisha yote kwa ujumla.

Naunganana King'ast, achana naye, nenda kaanze maisha na mtoto wako, tafuta mama mtu mzima awe anakaa naye nyumbani kwako akimlea kwa malipo.

Ukilazimisha, unaweka rehani maisha ya mtoto wako. Anaweza kuuawa, kufanyiwa kilema ama akaathirika kisaikolojia maisha yake yote yakaharibika. Mama wa kambo si watu!. labda apende mwenyewe.

Huyo mkeo kama anakuhitaji (ila kukupenda hakupo), muwe mnakutana lakini usimpe mtoto wako!.
 
Aiseeeeh kuna binadamu ni vigeugeu hatari!
Panga nyumba kando huko , weka mwanamke mwingine ndani , kusanya watoto wako muishi humo.
Ndiyo nshakushauri na akili zangu za Grants.
 
Back
Top Bottom