Mwanamke kamkataa mtoto wangu

Mwanamke kamkataa mtoto wangu

umejenga? kama umejenga chukua chumba mojawapo umwekee house girl mwakikishie asijihusishe naye kabisa kama anafanya kazi hapo safi kama mkeo ana kazi hapo majanga mpeleke boding.
 
Wamama tuna tabu jamani ci mchezo. Huyo mama kama ana akili nzuri huyo mtoto ndio chachu ya mapenzi kwa munewe. Hajui atachokikosa kutoka kwa moyo wamumewe. Hii ndii ingekuwa tiba tosha ya penzi na ndoa yao. Akina mm wenzangu hawa watoto wana utofauti gani na yule utaemzaa wewe? Huna formula ya maisha anaweza kuja kuwa mkombozi wako baadaye. Waweza zaa wakawa mataahira wote yuke unayemkataa akatoka kimaisha utajuta!!!
 
Hehehe huyo mwanamke ningemrusha kichura hadi kwao. eti Nini? unakataa damu yangu? who r u by the way. Juzi tu nilimpiga wife beat hio akatulia. Swala la wanangu ni NON NEGOTIABLE wewe lolote linaweza tokea. Full fukn stop.
 
Nasikitika nimeposti lkn siioni comments zangu. Kwa nyongeza maana sirudi za mwanzo. Molembe umeoa au umebahatisha tu. Mpange mkeo muwekane sawa hilo sio ombi kwamba unaasili mtoto. It is part of u as is ur leg! jwa upole na upendo mwelimishe naye kwa mapenzi aliyokupendea toka mwanzo aampokee huyo mtt km kiungo cha mwili wako. Wanawake wengine tuna laana kali. Natamani ungenipa huyo malaika nn ikulelee. Shame on that woman yy anajyaje ataishi kulea wa kwake??? mambo ya Mungu mengi
 
Daah namshukuru sana mzee wangu, tangu tukiwa wadogo alishaniambia madhara ya watoto wa ujanani wanavyotesa kwenye ndoa kwel najionea kwenye thread kama hii, pole sana bro@ molembe
 
utawajua wanaotegeshea ndoa.
Anyway peleka mtoto boading, akifunga shule akae kwako week siku zilizobaki mpeleke kwa dada yako. Kwan wew hauna mama?

Afu nyie mshawageuza mama zenu wazazi ni watu wakulea watoto wenu, acheni hizo mama amekulea wewe halafu unataka amlee na mwanao tena afu unakuta mama mwenyewe ameshachoka na umri umeenda hata nguvu za kukimbizana na malezi hana, acheni upumbavu huo
 
Mpeleke boarding school, likizo aje tu nyumbani kwako, hii inapunguza muda wa yeye kumlea..uskubali mwanao kukataliwa, hii pia itasababisha utengano na watotot wenzie ulonao.

na akiwa likizo mtafutie tuition mda wa kukaa hom uwe mdogo sn.
 
Kwakweli ina huzunisha sana,mama mtu alimtelekeza na kwenda kuolewa,walezi nao wamechoka kumlea,na sasa baba naye anapingamizi la kuishi na huyu mtoto,sasa aende wapi?
Kwa gharama yoyote ile mtoto huyu ana haki ya kulelewa na wazazi wake,kama sio mama basi ni baba mwenye jukumu hili.
Waswahili wanasema ukipenda boga penda na ua lake.
Bola ukosee kujenga nyumba lkn c kuoa.maana sasa mke huwezi kumwacha kwa jambo hili,lkn mtoto pia anaenda kuishi maisha ya kukataliwa na hilo litamwathili sana ki saikolojia maana atakakuja kujua tu kuwa mama yake wa kambo hakuwahi kumpenda,mama mzazi pia alimtelekeza,baba pia aliruhusu hilo litokee.na hata ndugu zake yani hao watoto wa pande nyingine hatowapenda maana kila atakachokikosa ktk maisha yake sababu itakuwa ni hii rejection.
 
Mtoto wangu wa kwanza ana miaka 8 nilimpata nikiwa mwaka 2 chuo ambapo kutokana na mamake kutokuwa mvumilivu kunisubiria nimalize kusoma aliamua kuolewa na kumuacha nyumbani kwao mtoto, nilipohitimu chuo na baada ya kupata kazi niliamua kumtafuta mwenza wa kuoa ambapo kabla ya yote nilimwambia ukweli kuwa nina mtoto na yeye akakubali atamlea lakini mara baada ya ndoa akanigeuka hataki kumuona mtoto huyo na kule anakokaa mtoto wanataka nimchukue.

Nimetumia kila njia imeshindikana msimamo wake ni hataki kumlea mtoto wa mwanamke mwingine, nifanyeje hapa wakuu maana nikilazimisha (uwezo huo ninao) anaweza kuwa anamtesa mtoto kipindi sipo akamsababishia matatizo ikitegemea huwa nasafiri mara kwa mara na sikai nyumbani sana na kuvunja ndoa siwezi maana ni ya kanisani na tayari tuna watoto
wengine wawili.

Ushauri wakuu

Mwambie aondoke aende kwao kuwa amevunja makubaliano yenu ya awali; amekiuka kile alichoahidi kutekeleza kwa mtoto wako. Aondoke na utafute mke mwingine ataekuwa tayar kuishi na mwanao. ukishindwa kodi kichwa changu japo kwa siku moja tu nitakunyoshea mawimbi-akina mama wengi hawajitambui linapokuja suala la mtoto wa nje but yeye yuko tayar kukuibia ili apeleke matumiz kwa mtoto wake wa nje, familia yake na michepuko yake
 
Mwezi mmoja umepita Molembe umekwisha patya suluhisho. Bas zaidi kwenye interest ya mtoto not otherwise!
 
Kama ulimwambia hata kabla ya ndoa na akaridhia, basi itakua alitafuta tu njia ya kukupata, lakini hana mapenzi ya dhati na wewe na ana roho mbaya, kumbuka mtoto ni damu yako na lazima uoneshe kuwa unaipenda damu yako tena kwa dhati na hauko tayari kuona mtoto wako ananyanyasika wakati baba yake yupo hai na una uwezo wa kulea, simama na umtete mwanao weka mikakati na uisimamie, zen mlete mtoto hapo home.

Ukiendekeza mapenzi unayopata kwa mkeo atakushawishi vibaya juu ya mwanao, mtetee mwanao, ajisikie ana baba la sivyo ataishi kwa manyanyaso. Mama yake tu hana time naye unadhani ataenda wapi akapate upendo kama sio kwako.

Nb; Na nyie wanaume pia acheni kuwakataa watoto waliozaliwa na wake zenu kabla ya kuwaoa, ukute hata huyo mama mtoto ana tamani kuishi na mwanae lakini mumewe huko amekataa.
 
na akiwa likizo mtafutie tuition mda wa kukaa hom uwe mdogo sn.

Kwakweli huwa nashindwa kumwelewa mtu anaye shindwa kukaa na mtoto, tena huyu aliambiwa mapemaaa. Cheki ushauri huu unaomnyima haki ya kukaa kwao!. Huo kama si ubinafsi chukuchuku ni nini?
 
Kwan huna wazazi? Mpeleke kwa bibi yake(mama yako) itarahihisisha sana maisha ya huyo kijana
Yaan unamsapoti mtoto at the same time unamsapoti mama yako, vzr zaidi itajenga ukaribu zaidi kati yako na mamayako
 
Kama ulimwambia hata kabla ya ndoa na akaridhia, basi itakua alitafuta tu njia ya kukupata, lakini hana mapenzi ya dhati na wewe na ana roho mbaya, kumbuka mtoto ni damu yako na lazima uoneshe kuwa unaipenda damu yako tena kwa dhati na hauko tayari kuona mtoto wako ananyanyasika wakati baba yake yupo hai na una uwezo wa kulea, simama na umtete mwanao weka mikakati na uisimamie, zen mlete mtoto hapo home.

Ukiendekeza mapenzi unayopata kwa mkeo atakushawishi vibaya juu ya mwanao, mtetee mwanao, ajisikie ana baba la sivyo ataishi kwa manyanyaso. Mama yake tu hana time naye unadhani ataenda wapi akapate upendo kama sio kwako.

Nb; Na nyie wanaume pia acheni kuwakataa watoto waliozaliwa na wake zenu kabla ya kuwaoa, ukute hata huyo mama mtoto ana tamani kuishi na mwanae lakini mumewe huko amekataa.
Bibie utatumia kinywaji gani?
 
Njia rahisi ni kumpeleka tu boarding school, atakuwa anarudi nyumbani kwa muda tu mfupi. Akishakuwa mtu mzima atakuwa amejitambua na manyanyaso hayatakuwepo.
 
Mpe option hii, mtoto aje nyumbani au yeye aondoke....achague moja hapo....then msikilizie atajibu nini...mwanaume lazima uwe na msimamo kaka.

Huu ushauri mbovu kuliko wowote hapa. Usithubutu kuufuata
 
Muambie mkeo unahama hapo ukatafute nyumba ukae na mwanao. Yeye mtakuwa mnatembeleana kama mtu na bf wake. gfsonwin, namaanisha hapo sio utani. Hivi wewe kama mtu kakukuta na mwanao na mnaoana anajua huyo ni mwanao. Then anakuambia simtaki huyu mtoto ungefanyaje? I would have done exactly that

Mshenga hii nzuri, kwa hili suala demokrasia haitakiwi kabisa, ipo siku atasema dada, mama, baba au Rafik yako flani simtaki,
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana bado una tabia za kuchepuka ndo maana amekataa au una manyanyaso flani hivi kwa mkeo. Jiangalie kwanza mwenyewe.

Ila huwezi kumuacha mkeo kwa ajili ya mtoto mwenye mama yake mzazi aliye hai ni bora umuombe dada yako akulelee huyo mtoto.
. achana na mkeo uone sasa kama ni rahisi kupata mwanamke wa kukulelea watoto watatu asiowazaa yeye...angalia sana huu ushauri feki unaopewa hapa. Japo nawe kulingana na post yako inaonesha umeshamchoka mkeo ndo maana unasema una ndo ya kikristo huwezi achana..
 
Ni mwezi mmoja umepita tangu nilete suala hilo hapa jukwaani nisikuleta suala hilo kama mzaha ni jambo ambalo linanigusa kwa ukubwa wa kipekee na kwa kutambua umuhimu wa wanajf hasa MMU nilitegemea kupata ushauri mzuri toka kwenu wapo watu walitoa ushauri mzuri sana mpaka wengine wakaweka exprience ya maisha yao wapo wengi walitoa ushauri wa kubeza na kubomoa lakini kwa hakika niliupokea ushauri wenu kwa moyo mkunjufu kabisa.
Kuhusu suala la kuvunja ndoa ni jambo ambalo haliwezekani kwa sababu tayari nina watoto 2 ambao nimezaa nae hivyo nikivunja ndoa nitakuwa na watoto 3 ambao itabidi walelewe na mama wa kambo je, yeye atakubali.
Kuhusu kutumia nguvu kumleta nyumbani nimeona nitamsababishia matatizo mtoto maana ni mdogo ataishi kwa shida hasa wakati ambao sipo nyumbani na itamuadhiri kisaikolojia.
Nilichoamua
nimetafuta shule ya boarding nchini Kenya na nategemea kumpeleka huko mwezi wa nane mihula yao itakapoanza vile vile niliweza kumtafuta mume mamake nikaongea nae kwa mapana zaidi ikiwemo kumuomba mtoto kwenda kumtembelea mamake pindi atakapofunga shule ili angalau apate mapenzi ya mamake akakubali hivyo mtoto ataenda boarding akifunga atakuwa anachagua pa kwenda kwa maana kwamba nyumbani kwetu kwa mama,bibiake mzaa mama na kwa mamake mzazi mpaka pale atakapofikia umri wa kujitegemea na kujitambua ndipo atakuja kuishi nyumbani.

Mwanamke kamkataa mtoto wangu
 
Back
Top Bottom