Mwanamke hana thamani, akitamkiwa TALAKA TALAKA TALAKA, ndoa imeisha hapo

Kwa hakika mwanamke ana thamani ndogo mnoooo.... Ukiachana na talaka halali pale mwanamke akikosea, kuna muda mwanaume anaweza kutaka tu kumfukuza mke wake, hapo akitamka tu Talaka mara 3 basi mwanamke anarudi kwao huko ndoa imeisha
Hapana. Si keli kwa Dini ya Kiislaam. Talaka ina sura nzima kwenye Qur'an jinsi ilivyopewa uzito.

Sharia ya talaka, kwanza ikitamkwa lazima wawepo mashahidi watu wazima wenye akili timamu. Pia mwanamke hata kama anaishi kwa mume huyo aliyempa talaka hakuna sheria ya yeye kuondoka hapo kwa huyo mwanamme mpaka amalize eda ya talaka. Na wakati wote wa kuwepo kwenye hiyo eda anatakiwa alishwe avishwe na atimiziwe mahitaji yake yote muhimu. Na ikiwa ana watoto anawalea basi hata ikisha eda si sheria yeye kuondoka na kutanga-tanga na watoto, inabidi akae hapo na watoto mpaka waingie utu uzima (balehe) au aamue mwenyewe mwanamke kuondoka kama anapo pa kwenda kuishi na watoto bila matatizo.

Huo ndiyo Uislam kuhusu talaka kwa uchache, msikae mnadanganyana kijinga. Tuulize Waislam tukupe darsa siyo unakuja kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Somo la talaka ni refu kiasi na lina vipengele vingi, lakini natumai hapo limegusa uongo wako na umeanza kuuelewa ukweli.

Hakuna dini iliyompa thamani mwanamke zaidi ya Uislam. Kwa kukujuza tu, mwanamke wa Kiislam anaweza kumuwacha mumewe ikiwa hatimizi vigezo vya kuwa mume, inaitwa "khulu'u.

Usilolijuwa ni usiku wa kiza.
 
Katupanga.
 
Thamani ya mwanamke haipo kwenye vitabu wala haipo kwenye sheria.
Kwa maana hayo yote yaweza kuwa yaliandikwa Kwa ubinafsi!

Thamani ya mwanamke ipo kwake mwenyewe, na Kwa watoto atakaowazaa.

Thamani ya mwanamke hutokea pale dunia nzima itakapokukataa lakini mama Yako kamwe hatakukataa!

Thamani ya mwanamke ni pale utakapozaa na Mkeo alafu ukashindwa kuwalea wanao ukamkimbja alafu utaona kile huyo mwanamke atakachokifanya.

Wanawake wanamadhaifu mengi lakini mengi ya hayo madhaifu yamesababishwa na wanaume waliowaamini
Ahsante
 
Back
Top Bottom