Nawakumbusha, Ndoa ndio ina talaka lakini Mapenzi hayana Talaka

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
NAWAKUMBUSHA, NDOA NDIO INA TALAKA LAKINI MAPENZI HAYANA TALAKA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Huwezi amua kumpenda Fulani. Upendo upo naturally. Mapenzi ni naturally. Mapenzi ya kuamua ni bandia. Huwezi amua umpende Fulani.

Nataka kusema, mapenzi yapo nje ya uamuzi wa Mtu. Ila kumfanya MTU kuwa Mumeo au mkeo huo ni uamuzi wa Mtu.

Ndoa ni maamuzi na hiyari ya MTU.
Wakati Mapenzi ni yanakuja automatically, naturally. Na Jambo lolote ambalo huja naturally ni very complicated, na mara nyingi sio kila mtu hulimudu.

Unaweza ukamuoa au kuolewa na mtu yeyote Yule lakini kamwe haitokuja kutokea ukaamua kumpenda MTU yeyote.

Mapenzi Yana Lugha zake ambazo sio Lugha za mdomoni.
Watu Wawili wanaopenda wakikutana huweza kuzungumza pasipo kuongea neno hata Moja.

Kikawaida mtu hupenda mara moja tuu.
Na huumia mara moja tuu.
Lakini MTU anaweza akafunga ndoa hata mara ishirini Huko.

Ukishampenda mtu hasa Yule wa Kwanza ndio ushampenda. Hakuna yeyote ambaye utakuja kumpenda kama mtu huyo.

Mapenzi hayana Talaka.
Ukishampenda mtu unaunganisha Nafsi na mioyo yenu pamoja.
Wakati ulishafunga ndoa na MTU mnaunganisha miili pamoja.
Miili huweza kutengana lakini sio mioyo au Nafsi.

Watu wanaweza kuvunja ndoa na ikaonekana hivyo lakini kamwe Watu hawawezi kuvunja Mapenzi Yao isipokuwa kifo pekee yake ambapo mmoja akifa basi aliyebaki hai hubaki na Nusu ya kipande cha Moyo.

Mdomo utakudanganya na hata MTU anaweza akadanganya kuwa Yule aliyekuwa anampenda Sana ameachana naye lakini kimsingi mtu huyo ni muongo. Ni aidha hakuwahi kumpenda(alidanganya) au anampenda lakini anasema tuu hampendi ili kuweka Mambo Sawa Kwa aliyenaye.

Unapoambiwa mtalaka hatongozwi ni Kwa sababu bado Watu hao wanapendana licha ya kuwa Miili Yao haipo pamoja Kutokana na mazingira ya Ndoa.

Kumbuka ndoa ni Sheria
Wakati Mapenzi ni Upendo.
Ndoa ni ushahidi/ vielelezo na Kanuni.
Mapenzi ni hisia zisizohitaji vielelezo na hayana Kanuni(miongozo)

Ndoa inahusisha makundi Matatu ambayo ni Familia ya Mwanamke, familia ya mwanaume na Mamlaka ya kuwaunganisha.
Mapenzi ni Watu Wawili mke na Mume tuu.

Ndoa inahusisha vitu vya ushahidi kama Mahari, Pete, vyeti n.k lakini
Mapenzi haihitaji hivyo vitu.

Ndoa ina-expire date,
Lakini Mapenzi hayana expire date, ni immortal. Hayafi.

Kwenye Ndoa kuna Ngono
Kwenye mapenzi kuna Mapenzi yenyewe.
Ngono haihusishi hisia Bali tendo, wajibu na malipo.
Mapenzi huhusisha hisia za ndani kabisa ambazo mtu huzipata akiwa katika tendo.

Ndoa Ipo ya Wake wengi, ndoa inagawanyika, unaweza OA hata Wake Elfu au kuolewa na wanaume elfu
Lakini Mapenzi hayagawanyiki. Moyoni atabaki mtu mmoja tuu. Daima.

Ndoa zinabadilika Kutokana na Sheria na Kanuni
Lakini Mapenzi hayabadiliki.

Ndoa huwa na Sababu
Mapenzi hayana Sababu.

Ndoa inawashauri na wafungishaji
Lakini Mapenzi hayashauriki na hayanaga third party.

Ndoa utapewa kitchen party, sijui makungwi, na unaweza kuingia mtandaoni kujitunza au kujisomea vitabu.
Lakini Mapenzi yapo moyoni Mwako. Hutokuja kujitunza popote pale kumpenda MTU unayempenda.

Na kama utajifunza basi upo ndoani na ndoa itakuwa ndoano Kwa sababu hakuna mapenzi.

Nipumzike sasa.

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Anaandika Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Back
Top Bottom