Mwanamke anayejitolea kukumbatia Watoto Njiti waliotelekezwa Hospitali ya Amana

Mwanamke mmoja mkazi wa Kinyerezi, Tabata jijini Dar es Salaam, Mariam Mwakabungu (25) amejitolea kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) na wanaotelekezwa na mama zao katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa Amana.

Mariam ambaye ni mke na mama wa watoto wawili, alianza kutoa msaada huo baada ya kumtembelea rafiki yake aliyejifungua mtoto njiti na kumuona mtoto ambaye aliishi kwa muda wa miezi minne bila kuongezeka uzito.

Anasimulia kuwa alipomuona njiti huyo wito ukamjia na kukumbuka kuwa yeye ni yatima ambaye hakupata bahati kulelewa na wazazi hivyo akaona hilo ni jukumu lake.


Chanzo: Mwananchi

Pia soma
Hongera sana
 
Politics mze hii...hiyo fursa ya kwenda kujiendeleza sijui kusomea ASTASHAHADA ya UUGUZI ndio MISSION ACCOMPLISHED...HARUDI TENA.
 
naelewa ila unapingaje wanaokuja kwamba hawana rohoo nzuri??? vipi wakitaka kufanyaa bure piaa... wala sikosoi ila haya mambo yapo
POLITICS...NAKUPA WIKI NENDA KAMA UTAMKUTA PALE...KAZI YAKE YA KUTENGENEZA TUKIO LA KUMPA RAIS MAILEJI YA KIASA ITAKUWA IMEISHA. UMESIKIA ATAENDA KUSOMEA ASTASHAHADA YA UUGUZI...NENDENI MKAMTAFUTE VYUO VYOTE KAMA MTAMKUTA.
 
POLITICS...NAKUPA WIKI NENDA KAMA UTAMKUTA PALE...KAZI YAKE YA KUTENGENEZA TUKIO LA KUMPA RAIS MAILEJI YA KIASA ITAKUWA IMEISHA. UMESIKIA ATAENDA KUSOMEA ASTASHAHADA YA UUGUZI...NENDENI MKAMTAFUTE VYUO VYOTE KAMA MTAMKUTA.
:D :D :D :D :Dila hili suala ni UONGOOOOOO... yani wazazi wa mtoto waache kujito kufanya natural incubation apewe mtu baki???mmmh awe analala wodin bureee
 
yupo clouds leooo anakiwashaa hukoo...sasa sijui watoto leo watapewa joto na nani!! nilitaka kuamini ila akili zimenirudiaaa :D :D :D mchongo huu
 
HUYO BWANA ANA HOJA...

KUINGIA KUFANYA KAZI HOSPITAL KUBWA KAMA AMANA, TENA YENYE RISK KAMA HIYO KUKUMBATIA VICHANGA...INAHITAJI IMANI NA KUFAHAMIKA HASA...

SWALI...ALIWEZAJE KUPENYA NA KUFANYA KAZI HIYO...?
Ndo bahati ya mwenzio hiyo mkuu Mimi niliwahi panda basi Dar-Tunduma bila tiketi pamoja na kaguzi zote nyingi njian
 
Haya mambo hayajawakuta ila kiukweli wife alizaa njiti na sasa ana miez sita shida ya kumkuza huyo mtoto hadi kufikia uzito unaotakiwa inahitaji moyo wa pekee iwapo sio mwanawe. Kwa ufupi huyo mama anahotaji pongezi
 
1.kuna vijana wengi sana wamemaliza vyuo mtaani, wamepeleka barua za kujitolea pale Amana, wamenyiwa hiyo nafasi,inakuwaje mtu from no where asie na kazi Wala taaluma husika akaomba nafasi ya kujitolea na akapewa?

2.Huyu binti ana Mume,na watoto (family) how comes Mwanaume amruhusu Mkewe akiwa anajua Hana taaluma husika, akajitolee sehemu?

Note: najua watu wengi, mmepongeza Sana,Ila wasiwasi wangu upo palepale!

Kuna Jambo kubwa nyuma ya pazia linaloendelea.
Dondosha nyama mukulu!!!au kutoana relini?
 
Back
Top Bottom