Mama aliyejifungua watoto NJITI 3 anadaiwa gharama za hospitali Tsh. Milioni 113. Rais tunaomba ahadi ya bima za bure kwa watanzania itekelezwe haraka

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
SIMULIZI YA MAMA ALIYEJIFUNGUA WATOTO WATATU AKIWA NA UJAUZITO WA MIEZI 6. WATOTO WAWILI WALIFARIKI DUNIA. ANADAIWA TSH MILIONI 113 HOSPITALINI

Njiti.JPG

Mama wa watoto Njiti, Emelia Francis amesema haya...

Nilipata ujauzito nikaendelea na Kliniki kama kawaida lakini nilivyofika wiki ya 24 (miezi 6) nilianza kusikia maumivu nikawasiliana na daktari alijitahidi kuzuia maumivu ilishindikana ilikuwa ni uchungu tayari ilivyofika jioni uchungu ukaongezeka watoto walikuwa ni mapacha watatu, changamoto zikawa ni nyingi za kuwasaidia ili waweze kuishi kwani walikuwa ni wadogo sana ikachukukiwa ambulance kuelekea hospitali nikajifungua watoto watatu, wawili wamefariki amebaki mmoja.

Ni pesa nyingi sana zinahitajika tunaomba msaada kwa watu wote ambaye ataguswa sisi hatujapumzika tangu siku niliyojifungua unawaza ukauze kitu gani upate pesa mtoto aliyebaki anahitaji maziwa, yule mtoto wa kwanza aliyefariki bili yake ilikuwa mill. 10 na wa pili ambaye naye amefariki bili yake ni mil. 30 huyu aliyebaki ambaye yupo ICU billi yake Mil. 113 kama familia hatuna uwezo tunaomba msaada.

Huyu mtoto aliyebaki ana miezi miwili, afya yake kwa ujumla inaendelea vizuri alianza kuwekewa tube ya kumsaidia kupumua inakwenda moja kwa moja kwenye mapafu bado yupo ICU.

Hadi sasa tumeshalipia zaidi ya Mil. 50 na bado mtoto anadaiwa bili zaidi ya shs Mil. 113 tumepambana tumeuza mali lakini bado pesa haitoshi, tunaomba msaada kwa watu na taasisi mbalimbali.


Chanzo: Clouds Media


-----
MAONI YANGU

Siku za hivi karibuni mheshimiwa Rais wetu mpendwa dokta John Joseph Pombe Magufuli alirudia ahadi yake aliyoitoa kipindi Cha kampeni kwamba Serikali inakusudia kutoa bure bima za afya kwa Watanzania wote.

Leo nimeona taarifa kupitia Clouds mama mmoja akiomba msaada wa kulipia bill ya gharama ambazo zimetumika kwenye matibabu ya watoto wake ambao wawili tayari wamefariki. Gharama Ni kubwa Sana kwa Watanzania walio wengi.

Nimetafakari nikaona kwamba Kuna haja ya Rais wetu Kuja mpango wa dharura ili bima za afya alizoahidi kwa Watanzania wote ziweze kutolewa ilo kila mtanzania aweze kupata huduma za afya pale inapohitajika.

Rais aliahidi kuboresha upatikanaji wa afya kwa watu wote na bila Shaka atakuja na Health insurance company ambayo itakuwa na vifurushi vya Hali ya juu.
 
Siku za hivi karibuni mheshimiwa Rais wetu mpendwa dokta John Joseph Pombe Magufuli alirudia ahadi yake aliyoitoa kipindi Cha kapempeni kwamba Serikali inakusudia kutoa bure bima za afya kwa Watanzania wote...
Tanzania kuna aina ya watu wa ajabu kidogo, kumbuka hatuwezi kuondoa matatizo kwa kuwatumia watu na chama kilekile kilichoyasababisha! Miaka 59 ya uhuru ni umri wa babu, labda apake rangi nywele na ndevu.
 
Aise mbona bili kubwa hivyo?

Ila tunapo zungumzia swala la bima inabidi tutambue kuwa bima nazo zinalimitation sio kuwa na bima itakuwezesha kupata kila huduma na kila sehemu. Na pia bima ina package zake na kila package ina gharama zake
 
Jana kuna kipindi kilikuwa live Radio one na kuna mtu kama sio wa NHIF ni mtu wizara ya afya alihojiwa kuhusu hizi gharama za watoto njiti, na jibu lake lilikuwa kwamba Serikali hugharimia watoto hadi miaka mitano.. Sasa sijui alikuwa ana jibu kufunika kombe mwana haramu apite au kuna ukweli?

Maana kwa nchi yetu kila kitu kinawezekana
 
Tanzania kuna aina ya watu wa ajabu kidogo,kumbuka HATUWEZI KUONDOA MATATIZO KWA KUWATUMIA WATU NA CHAMA KILEKILE KILICHOYASABABISHA!Miaka 59 ya uhuru ni umri wa babu,labda apake rangi nywele na ndevu.
Sasa mkuu kama imeshindikana mwaka huu unadhani kuna mwaka mtaiondoa CCM madarakani? Nakuambia hakika mtoto wangu aliyezaliwa juzi na kizazi hicho kitapita huku CCM ikitawala, bado sana kuingoa CCM, inaweza chukua karne nane kuanzia sasa
 
Ninavyofahamu ni kwamba sera ya serikali inasema watoto chini ya umri wa miaka 5 wanatibiwa bure kwa gharama za serikali. Huyu alikuwa anatibia watoto wake wapi mbona gharama ni kubwa sana? Hospitali gani Tanzania hii ina gharama hizi?
Matibabu ya watoto chini ya miaka 5 ni bure nchini Tz
 
Back
Top Bottom