Mwanafunzi mmoja afariki wengine hali tete wilayani Kilolo, Iringa baada ya kula futari ya msaada

Hoja ya msingi kama huna uwezo wa ku afford futari usifunge.
Na nimengundua islams wengi wanashinda na njaa. Katika kipindi hiki
 
Hatuwezi kujua kwa uharaka ule alioandika.Na uwezekano mkubwa ni uongo kabla hakujatolewa uthibitisho na chanzo cha kitabibu na kisheria.
Achana na masuala ya kitabibu/kisheria naongelea hayo uliyoyaorodhesha hapo juu kwamba;
-Wanafunzi wa kiislamu,
-Wamekula futari,
- msikitini,
-Iliyotolewa na jumuiya ya kiislamu, ndio nakuuliza haya maelezo ni ya uongo?
 
Hii imetokea katika shule ya Sekondari Kilolo iliyopo katika Kijiji cha Luganga, kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.

Tukio hilo limetokea jana. Wanafunzi 7 wa kiislam waliokuwa wamefunga kwenye mfungo wa Ramadhani wamekumbana na kadhia ya kutapika na kuharisha kunakoelezwa kunatokana na Chakula cha msaada walichopewa msikitini siku ya juzi.

Tukio hili limesababisha mtoto mmoja wa kike kufariki jana huku wengine wawili wakiwa na hali mbaya na waliletwa hapa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kusemekana kupewa chakula cha msaada kilochogawiwa juzi kwenye msikiti uliopo Kijiji cha Luganga kama msaada kwa wenzetu waliofunga toka taasisi moja ya jumuia ya kiislam.

Kati ya wanafunzi saba, mmoja alifariki. Wawili tuliwapokea hapa Hospitali wakiwa na hali mbaya na wanne wanaendelea vizuri na walibaki kule Hospitali ya Wilaya ya Kilolo

Hawa wawili nitaleta taarifa zao baada ya kufuatilia maendeleo yao ila hadi jana hali ilikiwa mbaya.

Pole kwa familia kwa kupoteza binti yao. Binti huyo alitoka Dar na kuja kusoma huku Iringa alipokutana na hiyo mauti. Mungu ampe pumziko jema binti yetu. Tunawaombea wengine hususani hawa wawili Mungu awaponye na kuwatoa katika shimo la mauti.

-----


JamiiForums imezungumza na Afisa Afya wa Wilaya, Dkt. Fanuel Nyadwike kuhusu tukio hilo amesema:

Jumla ya Wanafunzi ambao wamepata madhara ya chakula hicho na ambao wanaendelea na matibabu ni 17, sampuli zimechukuliwa kupelekwa kwa Mkemia Mkuu tunasubiri majibu, bado hatuna majibu ya zaidi kwa sasa, tunachokifanya ni kuwapatia huduma hawa ambao wamelazwa.

Huyo mmoja ambaye amefariki Dunia alipoteza maisha akiwa hapa Hospitali wakati anaendelea na matibabu, tayari ndugu wa marehemu wameshakuja kuuchukua mwili.

Ushauri
Watu wote wanatakiwa kuhakikisha vyakula wanavyokula vinakuwa salama, mfano wakati huu wa mfungo vyakula vinaandaliwe katika mazingira ya usafi.

Ushauri kwa shule mbalimbali, uongozi unatakiwa kuhakikisha vyakula wanavyopewa Wanafunzi maandalizi yake ni mazuri na wale vikiwa vya moto.

Maswali kuhusu msaada huo wa chakula ulitoka kwa nani na kama kuna waliokula lakini hawakupata madhara ya kiafya? Aliyefariki alikuwa kidato cha ngapi na kama kuna hatua zimechukuliwa, alipotafutwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Iringa, Allan Bukumbi, Msaidizi wake alisema yupo kikaoni wakati Uongozi wa Shule hakupatikana.
Nchi inajiendea tu... Ipo tu hovyohovyo yani..
 
Hawa wawili nitaleta taarifa zao baada ya kufuatilia maendeleo yao ila hadi jana hali ilikiwa mbaya.
Samahani, pamoja na nia nzuri ya kuhabarisha, lakini inaonekana huna mamlaka yoyote na taarifa inaonekana imekaa kimajungu, uchonganishi, fitina, chuki, hasadi n.k

Naona lengo lako lilikuwa uwe wa kwanza kuleta taarifa! Ukisoma unaona kabisa ndani yake kuna papara, mhemko, hisia, uharaka n.k! Kuna kitu ulikuwa unakilenga!
 
Kilichotakiwa kuandikwa ni kuwa kuna wanafunzi wamekufa .inakisiwa walikula chakula chenye sumu.
Baada ya uchunguzi kufanyika na polisi kutoa ripoti ingefuata taarifa nyengine kuwa walidhuriwa na nini.
Yeye kwa haraka ameshajua kila kitu na hiyo ni kwa vile wanafunzi walikuwa ni waislamu na alihisi walikula futari ya msaada na kwamba ilitolewa na taasisi ya kiislamu.Ana ushahidi gani wa yote hayo.
Yeye karahizisha kaandika kuanzia chakula ,waliokula ni nani wanafunzi wa kiislamu kwa nini aseme wa kiislamu jibu ni kuwa kawaida wanafunzi hawaruhusuwi kutoka nje ya shule ila sababu masalumu sasa hao ni wanafunzi wa kiislamu wako kwenye mfungo wa Ramadhani walitoka kwenda msikitini kuswali.Huko wakapewa chakula cha kufuturu wakale shule wakala kumbe kina sumu

Kaeleza kusaidia hata upelelezi uwe mwepesi polisi wanajua pa kuanzia wapi

Mleta yuko sawa tu
 
Wanafunzi walienda msikitini pale kwa Shehe Ally Bakwa. Wakapewa Futari (Tambo, viazi na maziwa).
Huyo Shehe anaitwa Shehe Bakwa huko walikoenda msikitini.Kwa nini anaitwa Shehe Bakwa ? Wote tunaelewa mambo yanayoitwa ya kubakwa
Hilo Jina la Shehe Bakwa linatokana na nini? Hadi akapewa? Kwamba huyu ndie Shehe Bakwa mwenyewe
 
Hoja ya msingi kama huna uwezo wa ku afford futari usifunge.
Na nimengundua islams wengi wanashinda na njaa. Katika kipindi hiki
Umepima ulichokiandika kweli yaani ushindwe ku afford futari basi usifunge kwahiyo usipofunga ndo utaweza ku afford milo mitatu kwa siku
 
Hizi futarifutari za mifungo huwa ni za kijinga, unakuta jitu fulani linajitolea kutoa uchafu wake kama msaada anajaza kwenye mandoo, majaba au mahotipoti linapeleka lilikokusudia huko magerezani, shuleni au mitaani kwa wapita njia. Nani anajua usalama wa vyakula hivyo vya kidini kama ni salama? Huu ni wakati wa kuwa makini na futari za hovyohovyo hata za mialiko toka kwa vigogo wanaofuturisha wakidhani wanafanya ibada zao
 
Ukialikwa kama umefunga kula taratibu na kama hujawahi kula hicho chakula basi onja tu
Mkiona pilau mnafakamia haswa
Nimeshuhudia watu wakiharisha kisa pilau ambalo hawajala mwaka mzima
Mnakimbilia ooh uchafu huku mkijijua mnakula uchafu kila leo
Mama ntilie anamuosha Mavi mtoto na maji hayo hayo anayooshea viombo na mnakula hamdhuriki
Ila mkipewa mualiko labda uwe ugali ndio mjaze tumbo
Pole kwa wafiwa
Tunajuana kwa kejeli na maneno ya maudhi ila kuwaza ndio vigumu
 
Msaada na zawadi huwa kuna nia imejificha nyuma yake so sio kila unachopewa unapokea, chunguza kwanza
Kwahiyo ukikaribishwa futari ikulu unachunguza kwanza! JF kila mtu anajiona anabusara kuliko wengine.
Akipita mtu anauza sumu ya panya unachunguza kwanza kwa kuonja kiduchu.
Hii kwa vijana wa sasa pamoja na Bashe, watanganyika karibu wote wa mpaka mwaka 1980 walikula unga wa yanga toka marekani, na asilimia kubwa ya wanafunzi walikula buruga, maziwa ya unga na mafuta ya kula toka marekani pia walikula mchele kitumbo toka china, na hawakugeuka mashoga. Tatizo lililopo sasa ni kila mtu mwanasiasa za kibaguzi japo hamsemi kama yule mwalimu wa madrasa jimboni kwa Bashe aliyewatafuna wanafunzi wake wa kiume kama naye alikula mchele wa marekani au tende za uarabuni.
 
Umepima ulichokiandika kweli yaani ushindwe ku afford futari basi usifunge kwahiyo usipofunga ndo utaweza ku afford milo mitatu kwa siku
Namaanisha kuepuka adha kama hizo za kula futari ya bure mwisho uishie kufa kwa kuhara
 
Mimi nimejaribu kuwa na fikra kama zako lakini aliyeyakuza ni huyo daktari au nesi wa hiyo hospitala ambaye ameona ataje futari,msikiti,jumuiya ya kiislamu.
lakini si ni kweli ni futari na ni kweli kimetolewa na jumuiya ya kiislamu kwani kuna ubaya? mi sioni kama kuna ubaya. hata ingekua jumuiya ya kikristo maadamu ndio wametoa chakula tunaitaja. si kwa ubaya. ukiniuliza nachojua mimi jumuiya ya kiislamu iliyotoa msaada hawakua na lengo baya. lakini uchunguzi ni muhimu kwa lengo la kuepusha madhara wakati ujao na kuchukuliwa hatua kama kuna uzembe ulifanyika ama na waandazi au waliotoa msaada.
 
Kwahiyo ukikaribishwa futari ikulu unachunguza kwanza! JF kila mtu anajiona anabusara kuliko wengine.
Akipita mtu anauza sumu ya panya unachunguza kwanza kwa kuonja kiduchu.
Hii kwa vijana wa sasa pamoja na Bashe, watanganyika karibu wote wa mpaka mwaka 1980 walikula unga wa yanga toka marekani, na asilimia kubwa ya wanafunzi walikula buruga, maziwa ya unga na mafuta ya kula toka marekani pia walikula mchele kitumbo toka china, na hawakugeuka mashoga. Tatizo lililopo sasa ni kila mtu mwanasiasa za kibaguzi japo hamsemi kama yule mwalimu wa madrasa jimboni kwa Bashe aliyewatafuna wanafunzi wake wa kiume kama naye alikula mchele wa marekani au tende za uarabuni.
Ndiyo maana ni mazwazwa mnapinga hadi ujenzi wa bwawa la umeme ambao ni kwa ajili yenu wenyewe.

Kucha kuombaomba tu walichofanyia kazi wanaume wenzenu
 
Back
Top Bottom