Mwanafunzi mmoja afariki wengine hali tete wilayani Kilolo, Iringa baada ya kula futari ya msaada

Mzee Abaya

JF-Expert Member
Nov 20, 2023
700
1,826
Hii imetokea katika shule ya Sekondari Kilolo iliyopo katika Kijiji cha Luganga, kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.

Tukio hilo limetokea jana. Wanafunzi 7 wa kiislam waliokuwa wamefunga kwenye mfungo wa Ramadhani wamekumbana na kadhia ya kutapika na kuharisha kunakoelezwa kunatokana na Chakula cha msaada walichopewa msikitini siku ya juzi.

Tukio hili limesababisha mtoto mmoja wa kike kufariki jana huku wengine wawili wakiwa na hali mbaya na waliletwa hapa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kusemekana kupewa chakula cha msaada kilochogawiwa juzi kwenye msikiti uliopo Kijiji cha Luganga kama msaada kwa wenzetu waliofunga toka taasisi moja ya jumuia ya kiislam.

Kati ya wanafunzi saba, mmoja alifariki. Wawili tuliwapokea hapa Hospitali wakiwa na hali mbaya na wanne wanaendelea vizuri na walibaki kule Hospitali ya Wilaya ya Kilolo

Hawa wawili nitaleta taarifa zao baada ya kufuatilia maendeleo yao ila hadi jana hali ilikiwa mbaya.

Pole kwa familia kwa kupoteza binti yao. Binti huyo alitoka Dar na kuja kusoma huku Iringa alipokutana na hiyo mauti. Mungu ampe pumziko jema binti yetu. Tunawaombea wengine hususani hawa wawili Mungu awaponye na kuwatoa katika shimo la mauti.

-----

JamiiForums imezungumza na Afisa Afya wa Wilaya, Dkt. Fanuel Nyadwike kuhusu tukio hilo amesema:

Jumla ya Wanafunzi ambao wamepata madhara ya chakula hicho na ambao wanaendelea na matibabu ni 17, sampuli zimechukuliwa kupelekwa kwa Mkemia Mkuu tunasubiri majibu, bado hatuna majibu ya zaidi kwa sasa, tunachokifanya ni kuwapatia huduma hawa ambao wamelazwa.

Huyo mmoja ambaye amefariki Dunia alipoteza maisha akiwa hapa Hospitali wakati anaendelea na matibabu, tayari ndugu wa marehemu wameshakuja kuuchukua mwili.

Ushauri
Watu wote wanatakiwa kuhakikisha vyakula wanavyokula vinakuwa salama, mfano wakati huu wa mfungo vyakula vinaandaliwe katika mazingira ya usafi.

Ushauri kwa shule mbalimbali, uongozi unatakiwa kuhakikisha vyakula wanavyopewa Wanafunzi maandalizi yake ni mazuri na wale vikiwa vya moto.

Maswali kuhusu msaada huo wa chakula ulitoka kwa nani na kama kuna waliokula lakini hawakupata madhara ya kiafya? Aliyefariki alikuwa kidato cha ngapi na kama kuna hatua zimechukuliwa, alipotafutwa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Iringa, Allan Bukumbi, Msaidizi wake alisema yupo kikaoni wakati Uongozi wa Shule hakupatikana.
 
Tukio hili limesababisha mtoto mmoja wa kike kufariki jana huku wengine wawili wakiwa na hali mbaya na waliletwa hapa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kusemekana kupewa chakula cha msaada kilochogawiwa juzi kwenye msikiti uliopo Kijiji cha Luganga kama msaada kwa wenzetu waliofunga toka taasisi moja ya jumuia ya kiislam.
Ingefaa kuitaja hiyo taasisi kwa manufaa ya shule zingine zisipokee msaada kutoka taasisi hiyo

Wataalamu wa sheria, je familia ya marehemu inaweza kuchukua hatua gani za kisheria dhidi ya taasisi iliyosababisha kifo hicho?
 
Hizi futarifutari za mifungo huwa ni za kijinga, unakuta jitu fulani linajitolea kutoa uchafu wake kama msaada anajaza kwenye mandoo, majaba au mahotipoti linapeleka lilikokusudia huko magerezani, shuleni au mitaani kwa wapita njia. Nani anajua usalama wa vyakula hivyo vya kidini kama ni salama? Huu ni wakati wa kuwa makini na futari za hovyohovyo hata za mialiko toka kwa vigogo wanaofuturisha wakidhani wanafanya ibada zao
 
Hii imetokea katika shule ya Sekondari Kilolo iliyopo katika Kijiji cha Luganga, kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.

Tukio hilo limetokea jana. Wanafunzi 7 wa kiislam waliokuwa wamefunga kwenye mfungo wa Ramadhani wamekumbana na kadhia ya kutapika na kuharisha kunakoelezwa kunatokana na Chakula cha msaada walichopewa msikitini siku ya juzi.

Tukio hili limesababisha mtoto mmoja wa kike kufariki jana huku wengine wawili wakiwa na hali mbaya na waliletwa hapa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kusemekana kupewa chakula cha msaada kilochogawiwa juzi kwenye msikiti uliopo Kijiji cha Luganga kama msaada kwa wenzetu waliofunga toka taasisi moja ya jumuia ya kiislam.

Kati ya wanafunzi saba, mmoja alifariki. Wawili tuliwapokea hapa Hospitali wakiwa na hali mbaya na wanne wanaendelea vizuri na walibaki kule Hospitali ya Wilaya ya Kilolo

Hawa wawili nitaleta taarifa zao baada ya kufuatilia maendeleo yao ila hadi jana hali ilikiwa mbaya.

Pole kwa familia kwa kupoteza binti yao. Binti huyo alitoka Dar na kuja kusoma huku Iringa alipokutana na hiyo mauti. Mungu ampe pumziko jema binti yetu. Tunawaombea wengine hususani hawa wawili Mungu awaponye na kuwatoa katika shimo la mauti.
Mmmh inahuzunisha sana familia kupoteza mtoto

Hiyo futari ililiwa na watoto hao 7 pekee au kuna watu wengine walikula hapo msikitini? Je hao wanafunzi 7 wanatoka shule moja na walienda na kurudi pamoja au?

Inaleta maswali magumu baada ya majonzi
 
Back
Top Bottom