BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 2,966
- 6,900
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Kwalakamu wilayani Rombo kwa madai ya kuhusika na mauaji ya fundi nguo, mkazi wa Kijiji cha Ngaseni, Anord Tarimo (30).
Agosti 29, mwaka huu fundi huyo, anadaiwa kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na mwanaume huyo, muda mfupi baada ya kwenda kazini kwake na kumwomba amnunulie chakula kwa kuwa hali yake ya kipato ilikuwa mbaya.
Inaelezwa kuwa, baada ya fundi huyo kumkubalia kwenda kumnunulia chakula ilipofika jioni mwanaume huyo alimwomba ampeleke nyumbani kwake kuwa alikuwa na usafiri wa pikipiki na alipomfikisha nyumbani kwake mwanaume huyo aliingia ndani na kuchukua panga na kuanza kumshambulia na baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na pikipiki yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo amesema baada Jeshi la Polisi kupata taarifa za tukio hilo lilifika haraka eneo la tukio na kufanya ufuatiliaji uliowezesha kumakamata mtuhumiwa huyo akiwa na baadhi ya vielelezo ikiwemo pikipiki ya marehemu.
Kamanda Maigwa amesema mtuhumiwa huyo pia alimjeruhi mtu mwingine, wakati akijaribu kutoa msaada kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani na baadaye kutokomea na pikipiki ya marehemu.
Amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa na kwamba mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani tararibu za kisheria ziatakapokamilika kwa hatua zaidi.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linatoa rai kwa wananchi kuwa halitasita kuwachukulia hatua za kisheria watu wote wanaojihusisha na matukio ya kihalifu kama haya na mengine," amesema Kamanda Maigwa.
Akisimulia tukio hilo, Remmy Shirima, mkazi wa Usseri amesema wakati kijana huyo akiwa kazini kwake akiendelea na shughuli za ufundi mtuhumiwa huyo alimfuata kazini kwake na kumwomba amnunulie chakula kwa kuwa hali yake ya kipato sio nzuri na kijana huyo akamkubalia na kwenda kumnunulia chakula.
"Mtuhumiwa alimwendea huyo kijana ambaye kwasasa ni marehemu na kumwomba amnunulie chakula kwa madai kuwa hali yake ni mbaya na alikuwa hana fedha mfukoni, huyu kijana akaenda naye mahali kwenda kumnunulia chakula, wakala wakamaliza, huyu mtuhumiwa akamwomba ampeleke nyumbani kwasababu alikuwa na usafiri na wakati huo usiku umeshaingia," amesema.
"Alimchukua na pikipiki yake na kumpeleka nyumbani, walipofika nyumbani mtuhumiwa aliingia ndani akatoka na panga ndipo alipoanza kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake," ameeleza.
"Marehemu alijitahidi kupiga yowe wakati akicharangwa mapanga, bahati nzuri kukawa kuna majirani wametoka kumsaidia, wakati hawa majirani nao wanamsaidia wakajeruhiwa na huyu mtuhumiwa, marehemu alipata mwanya akatoroka, alikimbia mita 100 damu zilikuwa zinamwagika sana na alidondoka na kufariki," amesema.
MWANANCHI