TUNASONONEKA MWANAFUNZI MWENZETU KAJINYONGA.
Ni ukweli kuwa mnenaji anayenenea sikio lililojiandaa kusikia kabla maneno yaliyonenwa na mnenaji huyo hayajanenwa, ananafasi kubwa ya kueleweka kuliko yule anayenenea wasikilizaji waliojiandaa kwa dmaharula kusikiliza maneno ya mnenaji huyo, lijalo kwa dharula huwa halina maanani.
Ni jambo linalotusikitisha sana kuwa rafiki yetu, kijana mwenzetu, ndugu yetu mpendwa ametutoka. majonzi tulonayo ni makubwa sana na sijui tutayafuta kwa kutumia kitambaa cha aina gani.
basi niseme, japo si mchunguzaji wa tatizo, ila ninaamini ya kuwa, na huwa ninasema ya kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI KUBWA SANA DUNIANI,
INAUA
INAHARIBU MALENGO
INAONDOA MATUMAINI
NA INASABABISHA KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO.
UTATUZI SAHIHI(nasema kwa vijana wote) NI KUWA NA NIA SAHIHI, MALENGO SAHIHI, NA KUWA NA MATUMAINI KATIKA YALE TUNAYOYAFANYA KATIKA MAAISHA YETU
Ndio, tunakutana na changamoto nyingi, lakini maatatizo yanapotuzidi nguvu, ni vema kuwashirikisha hata marafiki zetu wanaweza kutushauri na sio kuchukua uamuzi unaotuzidi umri.
KUWA WAZI, KATIKA YANYOTUSIBU, NI NJIA YA AWALI SAHIHI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZETU.
tunaponyamaza, changamoto zinajenga ngome imara ndani ya nafsi na kumfanya mtu aone kuwa aanaweza kuamua lolote kama hilo.
marehemu amejinyonga, rakini hata kama angekuwa na matatizo kama mlima, naamini kuwa kama angeyaweka wazi asingekosa ushauri wa busara ambao ungeweza kumsaidia.
tusiwe wepesi wa kukata tamaa, sababu tutajiona hatuwezi, hali tunnaweza, tutajiona hatustahili kuishi duniani, na tutashindwa kufanikiwa na maamuzi magumu kama haya ni rahisi sana, kwaa saababu yya kukata tamaa na kupoteza matumaini.
TUJENGE MATUMAINI IMARA, TUZAME KATIKA MALENGO CHANYA ILI TUEPUKE TATIZO KAMA HILI.
Zaidi niwaombe wadau wa JF mjue kuwa aliyejinyonga ni kijana aliyekuwa akitegemewa na taifa letu zuri, sisi wanadarasa wenzake tulimfahamuvizuri kwa utendaji kazi wake mahili, utu wema, na fikla sahihi.
tatizo la kukata tamaa na kufanya maamuzi ya kuinyonga ndiyo yanabidi kushauriwa kwenye thread hii na si kujadili kama alikuwa na ngoma, mpenzi, na mengine.
hayo hayatusaidii sisi kama VIJANA.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.