MwanaDiwani na Nape Nnauye Nawaomba hapa...

MwanaDiwani na Nape Nnauye Nawaomba hapa...

Ahsante sana. Mie napenda kuona watu wanaohoji badala ya kushabikia na kupiga debe kila kukicha kama mataahira. Wakiona madudu wanaangalia pembeni huku wamefumba macho.

kiongozi mimi ni mpenzi sana wa ccm na ni mwanachama hai wa CCM, ila nakerwa sana na hizi kauli za viongozi wa serikali ambao wao wamekasimiwa madaraka kwasababu ni wanachama wa CCM. muda mwingine wanatutia aibu kwa kauli zao. na unapomtofautisha mtendaji wa serikali ambaye kiukweli unauhakika kwamba amekasimiwa madaraka hayo na serikali kwasababu ni mwanachama wa CCM naona kama vile tunafunika moto kwa gunia na kimsingi moshi lazima utatuumbua.
 
Comrade gfsonwin una maana gani unaposema nimejibu kisiasa?. CCM ni chama cha kisiasa. Siasa zinaweza zisiwe na sheria iliyowazi bali sheria hazina siasa. Kwa maana hiyo, ndiyo maana nikamwambia kama ana swali kuhusiana na watendaji serikalini basi alipeleke serikalini.

Chama chetu kinaendeshwa kulingana na Katiba ya chama chetu iliyotafsiliwa na kuzaa taratibu, kanuni, maadili, miongozo na miiko ya wanachama na viongozi.

Kama unavyofahamu, CCM haiingilii utendaji wa serikali bali inasimamia utendaji wa serikali.

Nimalizie kwa kusema kuwa, FaizaFoxy anajaribu kumlisha maneno Waziri Lukuvi tofauti na kile kinachosemekana alikisema ndani ya Kanisa kulingana na maelezo ya Waziri Lukuvi.

Maelezo? hukumsikiliza mwenyewe Kanisani? nimekuwekea mkanda hapo juu kidogo. Hujauona?

Nimlishe maneno ili iweje? huo ukisikia uzandik ndio huo.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko
 
MwanaDiwani na Nape Nnauye,

Nawaomba hapa mtowe majibu kwa haya maswali myepesi kwa majibu muafaka, ambayo kila msomaji humu ataridhika nayo, na kama ana la ziada ataongezea.

1) Jee, alivyohubiri William Lukuvi kanisani kuwa hofu yake ni kuwa Zanzibar "wakiwachwa watawale watasumbua". Nyinyi kama wana CCM wenzangu naomba mje hapa mtueleze kinaga-ubaga, hayo ni maneno ya Lukuvi? au ya CCM? au ya Serikali?

Sitaki kumalizia kasema watasumbua vipi, labda nyinyi na wachangiaji wengine mmalizie.

Mkimaliza hili namba 1) kuna mengine yaja.

Ninamshangaa sana Mh Lukuvi kwa kauli zake za uchochezi ambazo amekuwa akizitoa mara kwa mara na kusababisha hofu na taharuki isiyokuwa na msingi wowote. Kauli yake ya ovyo na isiyokuwa na mashiko ni ile aliyoitoa kanisani wakati alipoalikwa katika hafla ya kumsimika askofu wa kanisa la Methodist. Lukuvi amesikika laivu bila chenga akiwatisha wananchi kwamba ikiwa watazikubali serikali 3 kwenye kura ya maoni, basi wategemee jeshi kuchukua nchi! Kama ndivyo basi, sisi raia tunaoteseka chini ya utawala wa CCM tunalikaribisha jeshi lije litawale badala ya kuendelea kuishi ndani ya utumwa wa serikali ya CCM.

Na maneno haya Lukuvi ameyarudia tena alipohojiwa na waandishi wa habari kutaka atoe ufafanuzi zaidi (wakidhani labda mwanzo alinukuliwa vibaya) na ameendelea kutetea hoja yake hiyo. Alijitetea kwamba yeye sio mtu wa kwanza kutamka maneno hayo kwani yameishawahi kutamkwa na mkuu wa nchi wakati anazindua bunge la katiba. Huu ni utetezi wa kitoto na kijuha. Rais alitamka maneno hayo akiwa bungeni na ameyatamka akiwa kama amiri jeshi mkuu (Commander-in-chief of the armed forces). Haya sio maneno ya kutamkwa ndani ya kanisa wala mahali popote pale. Maneno haya yana ukakasi mkubwa mbele ya jamii na yanaweza kuisambaratisha nchi na hata kusababisha vita ya kimbari. Tukumbuke kwamba Intarahamwe walikuwa wakifanya uchochezi kama huu kupitia makanisani na matokeo yake kila mtu anayajua.

Lukuvi hakuishia hapo tu lakini pia aliwadanganya wananchi kwamba wazanzibar wanataka uhuru kamili ili waifanye nchi yao kuwa ya kiislamu. Huu ni uwongo, uzandiki na unafiki wa kupindukia! Wazanzibar wanashindwa nini kujibadilisha kuwa nchi ya kiislamu wakati nchi yao ina mamlaka kamili tangu 2010? Ama kweli Lukuvi ana akili ndogo kama mbegu ya haradali! Hivi anadhani kwamba watanzania wa leo ni mbumbumbu kama wale wa 1947?

Watanzania tuwe makini na viongozi wenye akili ndogo kama Lukuvi kwani watu kama hawa ndio walioitumbukiza nchi ya Rwanda kwenye mauaji ya kimbari kwa kauli za kichochezi na zinazowagawanya wananchi. Kauli hii ya Lukuvi imezidi kulipasua taifa hadi kupelekea bunge la katiba kukaribia kuvunjika. Kauli za namna hii sio za kufumbia macho hata kidogo kwani madhara yake ni makubwa sana katika mshikamano na mustakabali wa nchi yetu. Akili za kuambiwa, changanya na za kwako!

Mungu ibariki ZANZIBAR, Mungu ibariki TANGANYIKA. Amina.
 
kuna jambo ambalo sijui ni makusudi ama ni kutoelewa kwa viongozi wa CCM, hasa wa miaka hii.

Hivi ilikuwaje Werema akatoa kauli ya kibagauzi kwa Zanzibar?? na je imekuwaje huyu Lukuvi akatoa kauli yakufanana na ya Werema ila kwa maneno tofauti kanisani??

mie nikionacho hapo ni kwamba, kwanza hawapimi kile wanachotakiwa kukisema na wanadhani wako juu ya sheria, pili hawajui kwamba wao kama viongozi wa serikali wana wajibu wa kuwaunganisha raia wake kwa upendo, umoja na ushirikiano na sio kuwatenga kwa kauli zilizojaa maneno ya kashfa, kibaguzi, na umwamba as if wao ni zaid ya watanzania wote.

rais mwenyewe hajawah kutamka kauli za kubagua lkn watendaji wake ndo wanaongoza sasa sijui ni kwamba uakishakuwa kiongaozi wa ccm unakuwa na uhuru wa kusema lolote hata kama linatishia umoja na mshkamano wetu.

wiki chache zilizopita tulisherehekea miaka 50 ya uhuru na umoja, mshkamano, amani na upendo vilikuwa ndio kauli mbiu yetu sasa je ina maana huyu Lukuvi alikuwa anaigiza tuu??

hebu aje hapa atujibu tena akiwa na akili timamu manake kama vile anapuliza cha arachunga zinaruka kidogo vile.
 
Maelezo? hukumsikiliza mwenyewe Kanisani? nimekuwekea mkanda hapo juu kidogo. Hujauona?

Nimlishe maneno ili iweje? huo ukisikia uzandik ndio huo.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko

mimi kama mwanachama hai wa ccm sitokubaliaa kukaa kimya pale viongozi wetu wapaokosea hasa kwenye masuala nyeti yanayo hatarisha amani na umoja wa nchi yetu.

tuseme wote hapana kwa kauli za kibaguzi kama hizi
 
Maelezo? hukumsikiliza mwenyewe Kanisani? nimekuwekea mkanda hapo juu kidogo. Hujauona?

Nimlishe maneno ili iweje? huo ukisikia uzandik ndio huo.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko

Hakika leo ndo nimekujua vizuri. Ukweli daima, fitina mwiko. Moja ya Ahadi murua za mwanaTANU.
 
Sidhani kama hapa watakuja kutoa majibu. Hakuna halaiki; hakuna wa kuwapigia makofi; hakuna pilau! Sahau!

kwi kwi kwi kwi,mkuu umeua bendi khaa..nimecheka sana mana hao jamaa kwa kupenda misifa hawajambo.
 
kuna jambo ambalo sijui ni makusudi ama ni kutoelewa kwa viongozi wa CCM, hasa wa miaka hii.

Hivi ilikuwaje Werema akatoa kauli ya kibagauzi kwa Zanzibar?? na je imekuwaje huyu Lukuvi akatoa kauli yakufanana na ya Werema ila kwa maneno tofauti kanisani??

mie nikionacho hapo ni kwamba, kwanza hawapimi kile wanachotakiwa kukisema na wanadhani wako juu ya sheria, pili hawajui kwamba wao kama viongozi wa serikali wana wajibu wa kuwaunganisha raia wake kwa upendo, umoja na ushirikiano na sio kuwatenga kwa kauli zilizojaa maneno ya kashfa, kibaguzi, na umwamba as if wao ni zaid ya watanzania wote.

rais mwenyewe hajawah kutamka kauli za kubagua lkn watendaji wake ndo wanaongoza sasa sijui ni kwamba uakishakuwa kiongaozi wa ccm unakuwa na uhuru wa kusema lolote hata kama linatishia umoja na mshkamano wetu.

wiki chache zilizopita tulisherehekea miaka 50 ya uhuru na umoja, mshkamano, amani na upendo vilikuwa ndio kauli mbiu yetu sasa je ina maana huyu Lukuvi alikuwa anaigiza tuu??

hebu aje hapa atujibu tena akiwa na akili timamu manake kama vile anapuliza cha arachunga zinaruka kidogo vile.

Miss you dorin. Love you
 
Porojo nyiiiingi na kuhororoja sana. Jibu swali, kama huna jibu sema sina jibu. Wacha kuhororoja hovyo, uunajishushia hadhi yako kuhororoja sana bila mpango. Unakuwa kama mwana CCM wa kawaida usie na msimamo thabit.

Jikumbushe uelewe kuwa sina haja ya kumlisha maneno Lukuvi:
Ungepaswa kufahamu mapema kama mimi ni mwanaCCM wa kawaida. Inawezekana hata hujasoma na kulielewa bandiko langu #72 .

Hata katika majibu yangu ya mwanzo nimekuuliza na nikakueleza kuwa mimi ni mwanaCCM wa kawaida.

Mambo ya serikali haijabiwi na chama, vile vile mambo ya chama hayajibiwi na serikali.

Majibu ya chama yanapatikana kwenye vikao, na kama kuna umuhimu wa wananchi kufahamishwa, basi kuna channel zake . serikali nayo ina taratibu zake katika maamuzi.

Waziri Lukuvi hakuwa pale kama kiongozi wa CCM bali alikuwa pale kama Mtendaji wa Serikali.

Huhitaji kuelezwa kuwa mkuu wa utendaji wa serikali ni nani na kwa maana hiyo, nimekupa njia mbadala za kuwasilisha maswali yako.
 
Acha kuzungukazunguka mmezoa hoja nyepesi, kwa unyenyekevu tu mueleze faiza foxy hoja yake ni nzito na imekuzidi uwezo tutkuelewa.

kama mnajuwa kutofautisha chama na serikali ni kwa nini vikao vya kamati kuu mnafanyia ikulu? swali la pili ni kwa nini wakuu wa mikoa na wilaya tunawaona kwenye ziara zenu mikoani wamevaa kijani na njano na wanamwagika mauno kama hawana akili nzuri?
 
Ungepaswa kufahamu mapema kama mimi ni mwanaCCM wa kawaida. Inawezekana hata hujasoma na kulielewa bandiko langu #72 .

Hata katika majibu yangu ya mwanzo nimekuuliza na nikakueleza kuwa mimi ni mwanaCCM wa kawaida.

Mambo ya serikali haijabiwi na chama, vile vile mambo ya chama hayajibiwi na serikali.

Majibu ya chama yanapatikana kwenye vikao, na kama kuna umuhimu wa wananchi kufahamishwa, basi kuna channel zake . serikali nayo ina taratibu zake katika maamuzi.

Waziri Lukuvi hakuwa pale kama kiongozi wa CCM bali alikuwa pale kama Mtendaji wa Serikali.

Huhitaji kuelezwa kuwa mkuu wa utendaji wa serikali ni nani na kwa maana hiyo, nimekupa njia mbadala za kuwasilisha maswali yako.

Siku nyingine una akili, au ugaidi Ni kwa wasio wana CCM tu?

Mkikutana kwenye vikao vyenu mwambie Mwigulu Savimbi kuwa dili yake ya bilioni 200 na Singasinga wa IPTL imeua bendi kabisa, serikali imekosa hata hela ya kununua vipimo vya dengue fever
 
Mkuu MwanaDiwani , Hoja zimewaishia, sasa wanajaribu kufanya PERSONAL ATTACK.
Comrade MSALANI kuna wanaJF hawawezi kuchangia hoja katika msingi wa hoja badala yake wanaanza kwanza kutafuta real identity ya mleta hoja. Mimi nimewambia ni mwanaCCM wa kawaida lakini bado wanajenga hoja za personal attack za kufikirika wakati hata hawanifahamu.

Waanzilishi wa Jamiiforums hawakuwa wajinga pale walipoweka nafasi kwa wanajf kuwa na chaguo la Verified and unverified user.

Ni kawaida ya binadamu anapofirisika kihoja, kitu anachoanza kufanya ni kutafuta madhaifu ya mleta hoja kama cheap shots.

Tutaenda nao polepole mpaka watafahamu maana na faida ya kujenga hoja katika msingi wa hoja.
 
Last edited by a moderator:
Hahahahah, William Lukuvi alichokifanya ni zaidi ya ubaguzi.

Werema, nawaachia Wazanzibari wenyewe, kwani wao ni wanafik, wakiwa Zanzibar wanasema mengine wakija Dodoma wanasema mengine. Astahili yao yawapate kwa Werema. Ingawa si vyema alivyosema na haitoshi, lakini niliona nnawatetea mazumbukuku, sikumuona hata mmoja akirudia hoja hiyo bungeni wala kulalamika kwenye vyombo vya habari. Wazanzibari wanajisaliti wenyewe kwa wenyewe, ni wanafik nambari moja.

Ff naona lile limbwata la ccm linaisha nguvu duu ama kweli hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho na nikuambie kitu ccm hawana tofauti na panya wanangata na kupuliza ukijashtuka imekula kwako.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Comrade MSALANI kuna wanaJF hawawezi kuchangia hoja katika msingi wa hoja badala yake wanaanza kwanza kutafuta real identity ya mleta hoja. Mimi nimewambia ni mwanaCCM wa kawaida lakini bado wanajenga hoja za personal attack za kufikirika wakati hata hawanifahamu.

Waanzilishi wa Jamiiforums hawakuwa wajinga pale walipoweka nafasi kwa wanajf kuwa na chaguo la Verified and unverified user.

Ni kawaida ya binadamu anapofirisika kihoja, kitu anachoanza kufanya ni kutafuta madhaifu ya mleta hoja kama cheap shots.

Tutaenda nao polepole mpaka watafahamu maana na faida ya kujenga hoja katika msingi wa hoja.
Nimekusoma uzuri Mkuu MwanaDiwani, tunawapa hoja za msingi, badala ya kujadili hoja mezani, wao wanajadili ID, na Avator. Tutaenda nao taratibu, naamini wataelewa tu!
 
Last edited by a moderator:
Nimalizie kwa kusema kuwa, FaizaFoxy anajaribu kumlisha maneno Waziri Lukuvi tofauti na kile kinachosemekana alikisema ndani ya Kanisa kulingana na maelezo ya Waziri Lukuvi.

Sijuhi labda unafikiri ni SIRI alichokisema wakati kilakitu kipo LIVE, Msikilize na kumuangalia hapa.

[video=youtube_share;jax6pSz9FVU]http://youtu.be/jax6pSz9FVU[/video]
 
Ff naona lile limbwata la ccm linaisha nguvu duu ama kweli hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho na nikuambie kitu ccm hawana tofauti na panya wanangata na kupuliza ukijashtuka imekula kwako.

Mnavutwa taraatibu, mnakuja!
 
Back
Top Bottom