Comrade
gfsonwin una maana gani unaposema nimejibu kisiasa?. CCM ni chama cha kisiasa. Siasa zinaweza zisiwe na sheria iliyowazi bali sheria hazina siasa. Kwa maana hiyo, ndiyo maana nikamwambia kama ana swali kuhusiana na watendaji serikalini basi alipeleke serikalini.
Chama chetu kinaendeshwa kulingana na Katiba ya chama chetu iliyofatafsiliwa na kuzaa taratibu, kanuni, maadili, miongozo na miiko ya wanachama na viongozi.
Kama unavyofahamu, CCM haiingilii utendaji wa serikali bali inasimamia utendaji wa serikali.
Nimalizie kwa kusema kuwa,
FaizaFoxy anajaribu kumlisha maneno Waziri Lukuvi tofauti na kile kinachosemekana alikisema ndani ya Kanisa kulingana na maelezo ya Waziri Lukuvi.