Uchaguzi 2020 Mwana wa kulitafuta Lijualikali kalipata, baada ya kuangukia pua Ubunge ajaribu udiwani na kuambulia kura 5. Adaiwa kutamani kurudi CHADEMA

Ni kama nilivyoeleza hapo juu naona mwamba karudisha mpira kwa kipa

CCM inawenyewe kama ni kujifunza siku nyingine hata apewe kitu gani hawezi kukubali tena

Pole kwa wote waliotia nia wakaambulia namba za viatu

Lijualikali katia nia kwenye Udiwani na kupata kura 5 hii ni hatari

Wakuu au kilimo cha nn kinabamba Kilombero? 🤣🤣🤣View attachment 1524814
Nilipokuwa mdogo sikuelewa usemi wa wakubwa kwamba "mjumbe hauawi" sasa ndio nimekuja kuelewa kumbe maana yake ni kwamba wajumbe wenyewe ndio wauaji. Hahahhaa.
Asikate tamaa abaki huko huko kujenga chama adi 2025 anaweza kurudi tena mjengoni.
 
Huyu Lijualikali si ndiye aliyesababisha TAKUKURU wakachunguze matumizi ya fedha za makato ya posho/ mishahara ya Wabunge kwa ajili ya shughuli za Chadema?
Hivi TAKUKURU walishatoa matokeo ya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha wabunge wa Chedema?
Hahahahaha waitoe wapi,hiyo taarifa waelewa walijua mapema pale takokulu waliingia chaka!
 
Kama huyo ni mmoja wa walio saliti nguvu za wapiga kura wake pale kilombero, cheki alivyo anguka na kuzimia
Kuna mtu alionya kuhusu Karma humu,kuhusiana na hii hamahama,mtu unaondoka kwa dharau wakati watu walikupigania kwa Jasho na Damu! Unadhani utabaki salama
FB_IMG_1596386584590.jpeg
 
Huyo ndiyo aliye anguka leo na kuzimia pale kilombero
Kwa kipindi kile ccm jimbo la kilombero lilikuwa la chadema tu,maana hata aliekuwa mbunge mteketa aliteuliwa tu lkn ilishinda chadema na alikuwa regia mtema kwa hiyo baada ya kuona mambo magumu ccm wakamtuma kingunge aje kuweka mambo sawa ndio akatangazwa mteketa huku regia mtema akipewa viti maalum,kwa bahati mbaya alifariki huyu dada kwa ajali ya gari na maziko yake kikwete alikuja ,wakati huo lijua likali bado anatunza dawa stoo pale ifakara

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
FB_IMG_1596386584590.jpeg
 
Si wanasema siasa haina adui wa kudumu., apokelewe na apewe ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama
 
Bwege tu yule .Hana ujanja wala usmart wowote wa kuishi mjini libaki tu huko Kikwavila na Siginali..dadek zake
Hawa wanakuja cdm watu wanawaona
Yule mwenzake alipokuja cdm hata kuchana nywele alikuwa hachani muafro huo kutwa kuvaa sendles
Chama kimembeba hadi kumlipia Ada lkn eti Mwishowe wanaleta dharau
Wangeondoka kimya kimya tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ndugu yangu Lijua likali angebaki CDM angeshinda vizuri kwa jinsi alivyokuwa akiheshimika.
Nimemfuatilia wakati nalima mpunga huko. Lakini tulisikitika Sana alivyohamia ccm. Mbaya zaidi Mh Lijualikali alikuwa anakubalika Hadi na Wana ccm alivyokuwa CDM. Vijana tunapopewa nafasi tuache habari za kufanya ya akina Lijua. Siyo mazuri.

Hii ni aibu. Chadema wamsamehe. Mbowe Msamehe kijana ingawa alikudhalilisha.Tumsamehe tu arudi nyumbani. Iwe fundisho Sana.
BADO. Anatakiwa kwanza apate fundisho.
 
Mbinguni tutaenda kuhesabiwa tuu ila mambo mengine yoote ni hapahapa.

amelipwa sawasawa na matendo yake ng'ombe huyo😂😂😂😂😂
 
Hili ni zaidi ya funzo kwa lijuakali na viongozi wengine wa type yake

Lijuakali aliondoka kwa matusi na kejeli za kila aina na akajua kwmb ccm wao ni wajinga kiasi hicho ona aibu anazo pata sasa

Akatia nia ubunge kuptia ccm akapata kura 5 akasema ccm nyie msinitanie me ni mtoto wa mjini lazima niwe kiongozi wenu tu

Akachukua fomu udiwani akatia nia kura za maoni zmefika wajumbe wamemjaza upepo wako nae na akajaa wakaanza safari kugeuka nyuma hakuna mtu kapata kura 2 kwenye udiwani nako

Sasa wenyekiti wa mtaa ungemfaa lkn sio muda sahihi akagombee ata uenyekiti katka ukoo wanaweza kumuamini
Ijue nguvu ya wajumbe
 
Hawa wanakuja cdm watu wanawaona
Yule mwenzake alipokuja cdm hata kuchana nywele alikuwa hachani muafro huo kutwa kuvaa sendles
Chama kimembeba hadi kumlipia Ada lkn eti Mwishowe wanaleta dharau
Wangeondoka kimya kimya tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Nakumbuka Sana...Sasa hivi wanashinda kwa visuti vyao vya mariedo wanatuchukulia mapeasant
 
Back
Top Bottom