Hili ni pengo kwa wana JF, lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe! Mme mfiwa ambaye ni mwana JF, tukopamoja nawe katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Mungu akutie nguvu!
Pole mme kwa kupoteza mwenza - Mungu akupe nguvu kukabiliana na haya, Poleni ndugu wa marehemu, Pole Maxe - marehemu alikua zaidi ya mwana JF kwako, alikugusa moja moja, Poleni wana JF wote, sehemu yetu imepungua na tuna maumivu. MUNGU AMWANGAZIE MAREHEMU MWANGA WA MILELE AMEN.
Mwanaume uliyefiwa pamoja na familia yako nzima, ndugu jamaa na marafiki pamoja na jumuia nzima ya JF, naomba nitoe pole nyingi sana kwa msiba huu uliotokea...... Bwana alitoa, naye ndiye aliyetwaa.... Jina la Bwana Lihimidiwe!!!
Huyu kwangu alikuwa zaidi ya mwana JF. Alikuwa sehemu ya familia kwangu. Mme wake kwangu ni kama kaka, yeye kwangu badala ya shemeji nilimwona dada kwani alikuwa ni mtu wa kunipa ushauri kila nilipouhitaji.
Mungu ndiye mpangaji, alimleta duniani na amemchukua mwenyewe kwa mapenzi yake. Mapenzi yetu yalikuwa ni kuendelea kuwa naye lakini yeye (Mungu) kampenda zaidi.
Pole sana mwenzetu kwa kuondokewa na mwenzi wa maisha, ni msiba mzito. Mwenyezi Mungu akupe nguvu za kukabiliana na hali hii, na akujaalie moyo wa subira na wa kuyakubali yote yatokayo kwake, kwa maana yeye ndiye ajuaye wakati wa kuvuna shambani mwake. Mshukuru Mungu kwa maisha aliyomjalia marehemu hadi kipindi hiki alipoamua kumtwaa.
Bwana ampokee pumzikoni milele
Aone mwanga wa milele
Apumzike kwa amani
Amina.