Mwana-Chitchat - Unaishi wapi? mtaa gani?

Niko hungumalwa barabara ya mwanza shinyanga. Kuna nyumba mpya pale ndo nimeuza pamba nikajenga. Na ina mpaka vyumba vya wageni mnakaribishwa sana.

Dah kumbe ndio wewe!! tutafutane ndugu yangu... fika njia ya panda ya kwenda Mwamashimba karibu kabisa na barabara ya kwenda nera... ulizia tu hapo watakuambia
 
Mie kwa kweli niko Dodoma,Njia ya kuelekea mnadani kuna kituo kinaitwa 'Mti mkubwa'
Ukishuka hapo angalia nyuma yako utaona nyumba ina geti jekundu..karibuni!
 
halafu platozoom wewe sio huyu mchoma chipsi wa hapa jirani na kwangu? na charminglady wewe sio yule dada huwa nanunua matunda kwake hapa Nyakato NHC, na BAGAH wewe sio yule muuza kande wa pale mitaa ya Nera?
hivi ni kweli 99% ya wanachitchat mnaishi Mwanza isipokuwa Bishanga tu anayeishi kamachumu? nitonye uliondoka mwaka gani pale kijijini kwetu rushwa? Kongosho umehama pale mhandu? Erickb52 utahama lini Nyegezi? Baba V isamilo kwema? Asprin anza kuhama mabatini TMA wametangaza mafuriko!! Kaizer siku hizi ile hiace ya Igoma buhongwa huendeshi tena? Judgement habari za kirumba mkuu? Madame B hivi umeshamaliza kale ka-bachela kako pale saut? KARIA CBE hamjambo? Kimbweka ile benz nimeiona imepaki Nyamagana mbona inafanana na ya kwako? Wakati ndo sasa vumilia tu nawe siku moja utajenga nyamhongolo, Mamndenyi poleni kwa usafiri wa kubahatisha wa huko Luchelele! Zinduna pale kwa kifua wazi umehama? na wengine mnikumbushe mitaa yenu
Dogo siku hizi nimehamia Kona ya Bwiru ila kuna nyumba nimepata Buhongwa karibu na kwa Judgement ndio nataka kuhamia
Karibu sana
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom