Mwalimu wa Shule ya msingi Mbagala Kuu, mkazi wa Mwanamtoti aitwaye Ally Said Kaule (26) maarufu kama Sir Ally amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Temeke kwa kosa la kumuingilia kingono mwanafunzi wake wa darasa la sita.
Akisomewa mashtaka leo Jumanne mbele ya hakimu mkazi Aziza Mbajo, Mwendesha mashtaka wa jamhuri Grace Lwila amedai katika tarehe isiyojulikana Agosti mwaka huu eneo la Mbagala Mwanamtoti mshtakiwa alimuingilia kingono mtoto wa miaka 11 ambaye ni mwanafunzi jina limehifadhiwa.
Mtoto mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mbagala kuu mkoani Dar Es Salaam anadaiwa kubakwa na Mwalimu wake mnamo mwezi Agosti mwaka huu wa 2022 huku Mwalimu huyo akimpatia binti huyo ufunguo wa makazi yake binafsi ili endapo akimuhitaji aweze kufika kwake kwa urahisi.
Baada ya kukamatwa na polisi kata na kuhojiwa mwalimu huyo Ally Said Kaule (26) alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti huyo na kwamba mipango yao ni kuja kuwa wanandoa. Kutokana na hilo Ally alikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi Mbagala na kuwekwa mahabusu mpaka kesi yake ilipotajwa mahakamani.