kumbe helewi kitu wewe uliza tukwambie, Nyerere aliona ili kuua nguvu ya vyama vya ushirika kama VFCU, ilibidi awatenge viongozi wa vyama hivyo na chama chenyewe, alimchukua Bomani na kumpeleka Dar kuwa waziri wa Ushirika na Kilimo, akalazimisha kila eneo la kazi lazima kuwe na tawi la TANU! Akachukua vimwana-TANU viherehere toka vitokako akaviweka kila mahali kuwa vikatibu vya hayo matawi, na mameneja wa maeneo hayo kuwa wenyeviti.
Hapo ndipo siasa ilipo ingilia nyanja ya uzalishaji. Wale makatibu wa matawi ya TANU wakawa ni watendaji wakuu na ndipo Chama Kushika Hatamu ikatangazwa rasmi. Pesa zikawa zinachotwa toka viwandani na kwenye vyama vya ushirika na kupelekwa TANU/CCM. Wanasiasa wakatamalaki kila upande na uzalishaji viwandani ukazorota na mashirika mengi kufa.
Bomani kwa kujua ama kutokujua lengo la Mwl. lilikuwa ni kummaliza nguvu za umaarufu, alikubaliana na mawazo ya Mwl. akasahau na kwao, akenda kuoa huko huko viongozi wengi wapuuzi wasipenda kwao wanako-oa! CCM ikavuruga uchumi wa nchi, ilipo ona mashirika mengi yamekufa ikaanzisha shirika lake la uchumi, weeh kwa vile walizoea kula bila kuzalisha halikuchukua round wakalikomba pyuuu! CCM ikauza mashirika yaliyokufa ili wapate pesa, walipoyamaliza wakaingilia BOT, wakalamba kwa style ya EPA. Historia ni ndefu, naomba kuwasilisha!