Mwalimu Nyerere na ukabila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu Nyerere na ukabila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lizzy, Jun 11, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Habari zenu jamani?!

  Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.

  Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!

  Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
  Asanteni!
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wakati Ule Nchi Maendeleo yalikuwa ya Upande Mmoja na Siasa zetu ziliashiria wananchi kuendelea kimpango Mfano
  Wachagga na Wahaya sisi tulikuwe tumepata Elimu na wakati wa Mkoloni tulishika Madaraka sasa kama Nyerere asinge fuatilia hiyo nchi ingekuwa inatawaliwa na makabila makubwa au makabila yaliyokuwa na Elimu
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwani nchi inaongozwa na kabila au mtu?!
   
 4. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ijumaa usiku inaonekana jukwaa la mapenzi kweli linakuwa limedoda watarudi wasubiri, tafsiri yangu tu usinijie juu.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sio kuongozwa tu Madaraka Mbalimbali Nchini yangeegemea hayo Makabila na Usawa usingekuwepo Mfano Mzuri angalia Jirani zetu Kenya na Kabila la Kikikuyu wao walipendwa na wakoloni; wana Elimu zaidi ya wengine; Ardhi Zaidi ya Wengine; Mji bora zaidi ya wengine (NAIROBI) Wengi wana Madaraka na ni Mabwanyenye
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Aliyataja makabila yanayokula ndizi kwa sana ambayo yalitafsiriwa kama Wachagga,Wahaya na Wanyakyusa ambao walikuwa juu kielimu na uwingi na alipendelea nafasi za juu(urais,makamu na waziri mkuu) ushikwe na makabila madogo ili makabila haya yasi-manopolize power.Hajatamkaa hadharani lakini aliwaambia watu wengi in private angependa iwe hivo.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyerere hajawahi kusema makabila fulani Tanzania hayastahili uongozi wa aina fulani. Umeona vyema kwani angefanya hivyo ingekuwa ni kwenda kinyume kabisa na yote aliyoyasimamia na kuyaamini. Hii ni mojawapo ya myths ambazo zimetengenezwa.
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nyerere aloliteua watu wa kutoka karibu mikoa ypte ya Tanzania kushika madaraka mbalimbali ndani ya serikali yake. Utashangaa kuwa makatibu wakuu, wakurugenzi na makamishna wengi walikuwa wametoka katika hiyo mikoa unayosema ya ndizi.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanza unakosea unaposema watu wengi walimpenda sana. Naomba kukufahamisha kuwa mimi nilikuwepo kabla, alipokuwepo, na baada yake. Nyerere hakupendwa na wengi kama unavyotakiwa kufikiria, Nyerere alilazimisha kupendwa, ukionesha kumpinga unapotezwa au unaswekwa ndani. Nyerere kisha koswa kupinduliwa mara nyingi tu kuliko Rais mwingine yoyote wa Tanzania.

  Mengine hayo utajaza mwenyewe.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nami nilikuwepo na nipo hadi sasa. Pamoja na kuwasweka ndani watu lakini Nyerere alikuwa akipendwa na wengi. Huwezi kupendwa na kila mtu lazima wawepo wengine ambao hawakupendi lakini kwa ujumla ni kwamba alikuwa anapendwa. Kuhusu kukoswa koswa kupinduliwa ukilinganisha na Marais wengine utakuwa hutendi haki kwa kuwa kwenye miaka ya 90s Africa ilianza kunusa demokrasia ukilinganisha na miaka ya 60s na 70s ambapo demokrasia kwa Africa ilikuwa ndoto. Kipindi baada ya uhuru kwa nchi nyingi Africa kilitawaliwa na ubabe pamoja na udikteta kwa hiyo waroho wa Madaraka waliona hakuna njia nyingine ya kuchukua hatamu za uongozi zaidi ya kutumia mtutu wa bunduki. Miaka baada ya uhuru kulikuwa hakuna chaguzi za ushindani africa, vyama vingi vya siasa vilipigwa marufuku.

  Kuhusu mada ni kwamba Nyerere hakuwa mkabila wa waziwazi lakini alikuwa na vimelea vya ukabila. Hakupenda Makabila kama Wachaga ambao wengi waliosomeshwa kupitia KNCU, Wahaya kupitia KCU pamoja na Wanyakyusa (ambao sijui walipata wapi bahati ya kusoma) waje kuchukua uongozi wa juu wa nchi kwa kuwa wangekuwa na solidarity na kupeana madaraka na kuyapuuza makabila mengine kama wakurya ambao elimu yao ilikuwa chini sana baada ya wakoloni kuwaona kuwa wanaweza tu kufungua bunduki na kupiga na wala siyo kufungua kurasa za vitabu.
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Lizzy nilikuwa sifikirii kama na huku unakuwepo,hongera kwa mada yenye akili.BACK TO TOPIC,sikumbuki kuhusu hili kama alisema direct lakini wenye kumbukumbu watakujuza!
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Yaani nyinyi watoto mliozaliwa baada ya nyerere kunga'tuka hamumjui vizuri huyo nyerere

  alipoaapishwa urais,hotuba yake ya kwanza alisema

  wale waliokosa upendeleo wakati wa mkoloni watapendelewa

  lakini yaliyofuata ni maajabu

  aliwafunga na kulivunja baraza la wazee la tanu

  ambalo ndilo lilipigania uhuru na kumuwezesha yeye akubalike

  akabadili historia

  badala ya kusema chama cha taa kilibadilishwa kuwa tanu

  yeye akasema nyerere aliunda tanu.....

  Wachaga na wahaya kwa kuwa walikuwa na nguvu mfano vyama vya ushirika vya wachaga na wahaya

  akavivunja huku

  akiiimarisha vyama vya ushirika vya mikoa mingine

  magazeti huru akapiga marufuku,ikabaki gazeti la uhuru na mzalendo

  wahariri wenye mawazo huru mfano yule mama wa south afrika aliekuwa mhariri wa daily news

  aliwatimua............

  Vyama vya siasa marufuku........ikabaki tanu peke yake


  akasema tuunganishe afrika mashariki umoja ni nguvu,wakati huo huo

  jumuia ya waislamu ya afrika mashariki akaivunja,akawa undia waislamu bakwata....

  Shule za wahindi waislamu nazo zikabebwa pamoja na shule za makanisa......

  Akamuweka kawawa ndio mshauri wake mkuuu

  na dini zikawekwa kando,ushirikina na watu wasio na dini kama

  kingunge na wengine wakapewa kipaumbele.......

  Na mengineyo...meeengi tu
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kila aliempinga alionja joto yajiwe

  waulize kina bibi titi,kambona,edwin mtei na wengine weengi
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hayo ni mawazo yakufikirika tu...hamna mwenye uhakika kwamba kama hilo lingetokea nchi ingeenda kombo(zaidi ya ilivyo) au pengine tungekua mbali sana kimaendeleo!Kama kweli alijitahidi kuzuia/kushawishi mkabila haya yasipate uongozi wa juu ina maana kwamba alikua mbinafsi sana kwa kuinyima Tanzania nafasi ambayo ingeweza kutufikisha mbali!Swala la kupeana madaraka hata kama sio ndani ya makabila hata sasa hivi lipo...kama hili hakuliona inawezekana hakuweza kuona faida ya kuifanya Tanzania nchi yenye demokrasia ya kweli na sio danganya toto!!
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hakusema kabisa au hakusema kwa uwazi?!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante kwa kunirekebisha ila bado naamini waliompenda wanazidi walio/wanaomchukua...au labda tuseme hawakumtambua sawasawa kiasi cha kuamini aliwatakia mema hivyo hawana malalamiko juu yake. Binafsi naamini alikua dikteta wa kichinichini..wale waliokua karibu yake tu ndo wanaojua ni kwa jinsi gani hakupenda upinzani!!
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba Nyerere alikuwa dikteta kwa definition ya udikteta ya Ulaya Magharibi (by then). Ila kwa viwango vya Africa kwa wakati huo Nyerere alikuwa nafuu sana kulinganisha na viongozi wengine Madkiteta wa Africa ambao walikuwa wakiwaua wapinzani wao kwa maelfu. Nyerere alikuwa akiwanyima uhuru wapinzani wake kwa kuwapeleka huko vijijini na hawakutakiwa kufika mjini kujua nini kinaendelea. Mfano Kasanga Tumbo na Mzee Mapalala! Alikuwa Dikteta ila alikuwa si muuaji kama madikteta wengine wa Afrika wa enzi zake.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Well kwa hayo uliyoyasema hapo juu nadhani mwl alichangia sana kutusimamisha sehemu moja tu kwenye mstari wa maendeleo!Kama angetoa uhuru kwa wote wenye mawazo mazuri kusikika hata kama yalipingana na yake tungekua tumeendelea sana kisiasa!
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Basi hakua mshindani hata kidogo....inawezekana alikua anaogopa sana upinzani!
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna story ameandika edwin mtei
  kwenye kitabu chake ukiisoma

  na ukisikia uvumi kuwa alikuwa na matatizo ya kama ugonjwa hivi wa mentall hivi unaweza connect the dots

  mfano nyerere alikuwa impulsive sana

  analipuka lipuka mno....

  kwenye kitabu mtei anasema aliwapeleka wazungu wa imf ikulu,
  nyerere badala hata ya kuwasikilza na kukataa,akasusa kuonana nao.
  wakati mwanzo alikubali waje ikulu.
  yaani aibu tupu,mtei akamkuta nyerere yuko nje ya ikulu kanuna hataki hata kuongea...

  na ukichanganya na jinsi zoezi la vijiji vya ujamaa lilivyopelekwa

  yaani watu walihamishwa wakapelekwa kwenye mapori waanzishe hivyo vijiji wengine wakaliwa na simba

  na ukiangalia mfano sera yake ya marufuku magari,ni baiskeli tu

  unaweza ona
   
Loading...