yaani nyerere mawazo yake yalikuwa finyu mpaka na yeye yamem cost
kutokuwepo kwa tv matokeo yake hotuba zake za tv zipo mbili tu....
na zilichukuliwa akiwa sio rais...na ni itv na channel ten tu ndo wanazo....
zingine nzuri hazipo kwenye tv
kitabu ni historia ya edwin mtei kimezinduliwa hivi karibuni
waulize watu wa chadema watakupa
Signature ya invisible ina maneno kwamba ficha upumbavu wako, onyesha hekima yako.
Leo hii tunaelekea kutimiza miaka 12 tangu mwalimu alipofariki lakini bado sehemu kubwa ya watanzania wanamkumbuka na kufanya reference kwake, wanafanya reference kwa uchapaji kazi wake, wanafanya reference kwa uzalendo wake, wanafanya reference kwa uwajibikaji wake, wanafanya reference kwa uongozi wake mahiri na kila aina ya utendaji wake.
Huwezi kumlinganisha mwalimu na hawa wanamagamba wa sasahivi, mwalimu alikuwa na vision sio hawa vilaza wa sasa hivi. Wewe mwenyewe huwezi kujilinganisha na mwalimu at any level na katika jambo lolote, ni mwendawazimu tu ndiye anaweza kusimama mbele ya hadhara na kusema kwamba mwalimu alikuwa na mawazo finyu, ni mwendawazimu pekee anyeweza kufanya hivyo!!
Eti ime-mcost? imemcost nini? kufariki? hilo nalo ni jambo la ajabu?kwani mwalimu hakuwa mwanadamu?mwanadamu kufa ni lazima au wewe unadhani mwalimu alikuwa malaika?
Kama tatizo lako ni tv, ni tatizo lako binafsi, si tatizo la watanzania wengi, kuna watu ndani ya nchi hii tv sio kipaumbele kwao
Radio ndio chombo pekee cha mawassiliano kinachoweza kuwafikia hata wale walioko vijijini mno, ambao angalau wanaweza kumudu kununua kiredio cha mkulima na kusikiliza. Kwahiyo hotuba zake kutokuwepo kwenye tv sio issue kabisa as long sauti yake ipo kwenye audio, mtu akitaka kupata ujumbe wa mwalimu anaupata. Tatizo lako nadhani unapenda kuuza sura kama viongozi wako wa sasahivi wanavyopenda kuuza sura ndio maana unalalam kutokuiona sura ya mwalimu kwenye tv. Mwalimu alikuwa anajali zaidi kuchapa kazi na kuwatumikia watanzania, sio kama hawa wasanii wenu wanaopenda kuuza sura lakini utendaji na uwajibikaji ni sifuri!!