Mwalimu afanywa chizi kisa na mkasa ni huu!

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,762
21,235
Ubhukile msani wa JF.

Kwa kifupi; Nilikuwa napita maeneo fulani hapa Lushoto nikamuona dada flani akipita na kuimba huku akikata kiuno ndipo nikakumbuka stori hii hapa chini.

Ilikuwa tarehe za mwishoni mwa mwaka nikitokea Dar to Iringa nikapata usafiri wa IT iliyokuwa inaenda Zambia, tulifika pale mlandizi - Pwani ikabidi jamaa asimame tupate mlo wa usiku.

Wakati nakaa nikasikia sauti ya kike "mwalimu umekuja, ninunulie chakula au naomba hela..."

Sikushituka sababu siyo mwalimu, ila nikageuka kumuangalia ni nani nikamuona mwanadada kasimama nyuma yangu alikuwa mwanamke mmoja mrefu hivi, mrefu kashika fimbo ananiangalia.

Sikumjibu chochote hadi akaondoka pale nilipokuwa nimekaa, ndipo nikamuuliza mama muuza chakula vipi huyu dada mbona mzuri na ana hali hii?, na haya ndiyo majibu yake.

"... Huyu mwalimu alikuwa anafundisha shule (x) hali aliyonayo ni kwa sababu alikuwa anatembea na mume wa mtu, hivyo mwenye mume kamuonya mara kadhaa aachane na mume wake akawa hasikii ndipo mwenye mume (mwanamke) akaenda kwa wataalam wakamshugulikia kwa kumuharibu akili na ndiyo unavyomuona"

Ukweli kwa mdau uliye JF unaishi maeneo ya mlandizi basi utakuwa umemfaham au kumuona huyo mwalimu, hakika ni mzuri kiumbo nadhani hata sura, ilikuwa usiku so nisingeweza kupata picha.

Ila in vision unaweza kupiga picha wale wanawake wa kinyarwanda walivyo ndivyo na huyo alivyo.

Swali na Jibu ni kwa nini huyo ke' aliyemfanya hivyo mwenzake asimzuie mumewe kwa kumfunga na hayo madawa badala yake amemuacha mumewe ambaye ni sababu na anaweza kutafuta ke' mwingine huku kamharibu mwenzake?.

Nawasilisha.
 
Kama ameweza kumzima mwenzie data, si angemuomba huyo mganga amsahaulishe mume wake juu ya kuchepuka.

Hawa waganga baadala ya kuumiza watu, siangemuomba mganga amsaidie yeye na mume wake wahame mlandizi na kwenda kuishi Paris-France.
 
Kama ameweza kumzima mwenzie data, si angemuomba huyo mganga amsahaulishe mume wake juu ya kuchepuka.

Hawa waganga baadala ya kuumiza watu, siangemuomba mganga amsaidie yeye na mume wake wahame mlandizi na kwenda kuishi Paris-France.
akimsahaulisha asiwe na wanawake wengine nyota ya mme wake inazima kiufupi ni kwamba hao walitunishiana misuli mmoja akajipiga kifua akasema tutaona ogopa sana
 
Back
Top Bottom