Abtali mwerevu
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 637
- 432
Na: Mwalimu Makoba
1
Hadithi ya Idi Amin na wake zake ni miongoni mwa hadithi za kusisimua, kuchekesha na zilizojaa ukatili. Kuwa na wake watano na wote wazuri ni msisimko wa aina yake. Kuwa na michepuko thelathini na watoto thelathini na nne (namba ya idadi ya watoto wa Idi Amin haijawahi kuwa sawa, hutofautiana hata katika nyaraka rasmi).
Mke wa kwanza aliitwa Maryamu, mtoto wa mwalimu mkuu, Bwana Kibedi, na dada wa Waziri wa Mambo ya Nje, Wanume Kibedi.
Ingawa alizaa naye watoto kadhaa, hakufunga naye ndoa mpaka ilipofika mwaka 1966, mwaka alioshambulia makazi ya Kabaka na kujizolea umaarufu mkubwa. Kupata watoto bila kufunga ndoa siyo jambo la ajabu Uganda. Idi Amin alilipa mahari, ndoa ikatambulika.
Amin aliishi na mke huyu kwa miaka kumi na tatu. Alikuwa tayari kutafuta mke mdogo kama ilivyo desturi. Alihitaji mke kutoka kabila lake ndipo akampata Kay Adroa. Alimchagua Kay kwa sababu alikuwa msomi kutoka chuo Kikuu cha Makerere, mrembo, mpole na aliyekuwa na aliyekamilika kila idara.
Amin aliifahamu familia ya Kay vizuri. Hata mwaka 1966, bunge lilipoomba kusimamishwa kazi kwa Idi Amin kwa sababu ya tuhuma za wizi wa dhahabu, alikwenda mafichoni na Kay. Kay alikuwa mkiristo kama Malyam. Ndoa ya Idi Amin na Kay ilifungwa kiserikali. Kay alivalia shera nyeupe na Amin alivaa nguo za kivita kama anayeenda kupigana na adui! Sherehe ilifanyika Arua, nyumbani kwao Amin. Mpambe alikuwa Erinayo Oryema, ambaye baadae alizawadiwa uwaziri wa ardhi na maji, pamoja na yote, baadaye aliuawa!
Ndani ya mwaka mmoja, Amin aliongeza mke wa tatu, Nora, kabila lake mlangi kutoka nyumbani kwao Obote. Ndoa ya Amin na Nora ilikuwa ni mkakati wa kisiasa. Baada ya Amin kujizolea umaarufu, Obote akawa na mashaka kuhusu lengo hasa la Amin. Kuoa binti kutoka kabila la Obote, kungefanya ionekane kuwa tofauti yao ya makabila si tatizo na hivyo kupunguza wasiwasi. Mpaka inafika mwishoni mwa miaka ya 60, Amin alikuwa na watoto kumi au kumi na tano.
Inaendelea...
Soma: Jinsi ya Kuandika CV