Mwakasege ashangaa wasichana wa Dar kutoolewa

Mwakasege ashangaa wasichana wa Dar kutoolewa

Waoji wapo ila hamuwaoni kutokana na vigezo mlivyoweka kutaka mwanaume;
1. Aliyetia rasta na kuvaa hereni
2. Kutaka wanamuziki, au star wa bongo movie
3. Kutaka mwanaume aliyetayari kukubali kila utakachoongea au kushauri bila kupingwa
4. Kumtaka mwanaume aliye tayari kuishi na wewe na kukukubali kama ulivyo bila kushauri lolote mfano kama unapendelea club akuache ukajiachie na marafiki, kuvaa ovyo, kula hotelini hata kama mna uwezo wa kupika nk.
5. Kumtaka mwanaume awe tayari kugawana zamu za kupika, kufua nguo na kubeba mtoto wakati wewe ukiangalia TV

Kwa tabia hizi hakuna mwanaume serious na mwenye kutaka bright future atakuwa tayari kukuoa.
Wanaume wanataka waoe MKE NA MAMA WA WATOTO wake ambaye wakikaa wanaweza panga mambo muhimu kuhusu maisha yao ya sasa na baadaye, watoto wao na future yao na si mwanamke ambaye hana foresight bali yeye anaona mume kama source of income kwa mambo yake ya ovyo ovyo.

Si kweli kwamba waoji hawapo huo ni uongo na mtazamo wako ni wa aina ya wanawake nilioeleza hapo juu. Hatuna tu statistics kila wiki dar yenyewe wanaume wanaofunga ndoa ni wengi mno kwa hiyo ukiona hujaolewa usiseme waoaji hawapo labda wewe sema sijapata wa vigezo vyako

Unless you need a television set kama unataka kuolewa hakuna mtu anataka mke waaina hii
 
Yule binti ana mchumba !!!

Mchumba si mume. Tunaongelea ndoa, si mchumba. Mchumba hata masela wanaotaka kupakua mzigo na kusepa mbona wanatumia gia ya mchumba?

Hii habari inakusanya watu, na hivyo si ajabu watu kupata wachumba kama vile wanavyoweza kupata wachumba kwenye mikusanyiko mingine.

Ila hizi habari za maombi ni fix tu.
 
Maandiko Yanasema Kuna Wakati Wanawake 6 Watamwendea Mwanaume Mmoja Wakisema Tutajilisha Na Kujivisha Japo Tuitwe Kwa Jina Lako
 
"Mganga hajigangi" ni msemo wa waganga waongo kuridhisha wajinga wanaoibiwa.

Hao watumishi matapeli tu, hawana lolote ambalo wanaweza kufanya ambalo mkusanyiko wa watu wenye akili zao hautaweza kufanya.

Haya, na tuone hiyo hukumu basi.

Mtu kashindwa kumuoza bintiye, leo atoe ushauri na maombi kuoza wengine.

Ni sawasawa na kuenda kupata ushauri wa kupunguza uzito kutoka kwa mtu mwenye tatizo la uzito kwake.

Au uende kuomba ushauri wa kuacha ulevi kwenye nyumba iliyojaa walevi.

Hapo kinachotokea ni kwamba desperate people will believe anything that gives them promise.

Ukiweka jina la mungu ndiyo kabisaa, watu eanaondoa akili zote na kuachia autopilot ya maombi.

Kwa imani kama hizi tutazidi kuwa masikini kwa miaka mingi sana tu.

Nimegundua tatizo lako ndugu. Pole.
Umeshajibiwa binti yake ana mchumba tayari.
Usihukumu watu bila kuwa na uhakika, utapeli wao ni upi kuna aliyelazimishwa kwenda na akalazimishwa kutoa chochote hapana. Wako desparate na wamepata amani wewe unaumwa wapi wenzio wakiombewa? Umasikini upi unaoongelea mbona mnafanya matambiko .
Na hakuwa akiombea watu waolewe, alikuwa anaombea watu walioapa vitu ambavyo vinawaletea madhara ikiwa moja wapo ya sababu za kutooa au kuolewa.
Subiri hukumu kama ulivyosema.
 
Minimesoma nimeolewa nanimtiifu ,usilazimishe shida za kwenu kwenye maisha ya watu,kama wewe huolewi/huoi jiongeze ujue tatizo sio kukaa kujadili huduma za watu,ooh watoto wawatu kunamtu asietaka binti ake aolewe kwa heshima au kijana wake aoe?kutokuoa pia ni ulemavu maana huwezi kuongoza mwanamke mmoja utaweza hata ukiranja wewe?

Kuna watu washapita conventions zenu za ndoa. Kwa hiyo kama wewe unaona kijijini kwenu watu waneweka ndoa kama ultimate standard of morality, ujue kuna post modernist feminist ambao wanataka kuzaa tu na kusepa walee watoto wenyewe.

Usifikiri kila mtu ana moral conventions kama zako.
 
Uzuri ni kwamba unanisaidia kufikiri misijafikiri ivyo,pili sikulazimishi kuelewa pia angalia hoja usikurupuke
 
Nimegundua tatizo lako ndugu. Pole.
Umeshajibiwa binti yake ana mchumba tayari.
Usihukumu watu bila kuwa na uhakika, utapeli wao ni upi kuna aliyelazimishwa kwenda na akalazimishwa kutoa chochote hapana. Wako desparate na wamepata amani wewe unaumwa wapi wenzio wakiombewa? Umasikini upi unaoongelea mbona mnafanya matambiko .
Na hakuwa akiombea watu waolewe, alikuwa anaombea watu walioapa vitu ambavyo vinawaletea madhara ikiwa moja wapo ya sababu za kutooa au kuolewa.
Subiri hukumu kama ulivyosema.

Tapeli analazimisha mtu? Unaelewa maana ya tapeli?

Unaniambia nisihukumu watu bila ya kuwa na uhakika mara baada ya kuniambia umegundua tatizo langu, una uhakika ganinwewe mwenyewe kwamba umegundua tatizo langu?

Au unanipa sheria ambayo hata wewe mwenyewe huwezi kuifuata?

Wapi ninesema naumwa watu wakiombewa? Na kwa nini kusema ninachoona kwamba huku kuombewa ni utapeli tu mpaka niumwe?

Nani anafanya matambiko? Umepata wapi habari ya matambiko? Imelewa kikevi gani mpaka kuleta habari ya matambiko?

Kuombewa ndiyo nini kama si utapeli na uganga wa uongo tu?

Kama huyo mtu anaweza kuombea wengine kwa nini hajamuombea binti yake aolewe?
 
Pole sana
 
Maandiko Yanasema Kuna Wakati Wanawake 6 Watamwendea Mwanaume Mmoja Wakisema Tutajilisha Na Kujivisha Japo Tuitwe Kwa Jina Lako

Maandiko yamejaa kujipinga, ndiyo maana anything goes, pamoja na utapeli wa kika aina.

Deaperate people will always do desperate things.
 
Tatizo jamii zetu zinawapa wanaume majukumu makubwa sana kama providers, wanaume wenyewe wengi maisha hayajakaa vizuri wanaona kuoa bado, na hivyo wanawake wengi wanabaki hawajaolewa.

Badala ya kukesha mkiomba, wawezesheni watu wapate kazi, wanawake kwa wanaume, watu wenye uwezo wa kiuchumi naturally huelekea kwenye kuoana zaidi.

Hii ndo sàbabu kubwa nyingine ni sababu ndogo sema watu wanakimbilia mambo yasiyo husika kabisa
 
Wengi wao ambao hawajaolewa wapo lile lichama chakavu,amieni 'mabadiliko' muone huo msururu wa watangaza nia.

umenena Mkuu, yaan hata hapa nawaona wanavyonunuliwa na kutwa kushinda wanazunguka kuimba hilo lichama, hivi kama hawajielewi hata matatizo yao, hizo changamoto za ndoa je?
 
nadhani tatizo hili ni kubwa mno kwa kuwa mabinti wengi kwenye umri wa kkuolewa ndipo mabinti wa Mjini hasa Dar wanapojisahau na kufikiri kuwa kuolewa ni jambo la kuamuka na kuondoka tu. Wakati huo wamekuwa wakibehave tofauti na mtu unayeweza kusema huyu anaweza kuwa mke au anaweza kulea watoto na familia, wengi wanakuwa wanabahve kama ma malikia wa Ngwasuma.
 
Hii ndo sàbabu kubwa nyingine ni sababu ndogo sema watu wanakimbilia mambo yasiyo husika kabisa

Kila kitu maombi.

Mvua hazinyeshi kwa sababu watu wanakata miti, solution maombi.

Matatizo ya watu kutokuoa kutokana na social economic issues, solution maombi.

Tunakuwa kama vilema wa kufikiri, kila tatizo maombi.

Mwishowe kutakuwa na maombi ya kuombea foleni za barabarani zipungue.
 
Hamna shida nini? Utaacha kuwa msukule wa matapeli?

Kama hutaacha hujanielewa bado.

Bado sijatapeliwa niko njia sahihi, sina mashaka. Najua nataka nini. Huna umuhimu kiasi hicho unachodhani, ushauri unakubaliwa au kukataliwa hata ukieleweka ni uamuzi wangu nikuhandle vipi
 
Bado sijatapeliwa niko njia sahihi, sina mashaka. Najua nataka nini. Huna umuhimu kiasi hicho unachodhani, ushauri unakubaliwa au kukataliwa hata ukieleweka ni uamuzi wangu nikuhandle vipi

Ulichoelewa kipi?
 
Kama maziwa napata tena kwa bei nafuu....kuna haja gani ya kufuga ngo'ombe.....???
 
Back
Top Bottom