EPISODE 2.
Nipo mikononi mwa askari kitengo cha udhibiti wa custums(douane).
Nikishikiliwa kwa mahojiano.
Nakumbuka baada ya wale askari kunipiga bega na kunisimamisha,
Waliomba ticket yangu pamoja na passport yangu.
Lengo lao ni kuangalia route nzima ya safari yangu.
Do you have anything eligal things like drugs, Ashish, marijuana,dirty money nk.
La Chief aliuliza,
Nikamjibu mm sina chochote humo.
Wakati wao wapo busy na kukaguwa mabag yng nikapata wasaa wa kufuta namba pamoja na sms zote za watu wa ulaya ambao nilikuwa nawasiliana nao na wengine wapo ktk phone contact zng .
DK 5 nikawa nimefuta conservation zote za watu wangu muhimu,,
Maana hata Kama kuna jamaa alinibeep Tu,,ujuwe angetafutwa.
.nilifanya hivyo sababu nilijuwa nikipata tatizo lolote pale France wangewasumbuwa wote waliokuwa kwenye contact list zangu kwa waishio ulaya.
-A good captain always sink with his ship..
Niliamua kuzama na meli yngu ili nisimsababishie yeyote matatizo..
Jamaa walitoa nguo zote pale kwenye mabag yangu ,,
search ikaanza .
Jamaa walianza kwa kuliinuwa juu bag likiwa tupu.
Nina maana kulipima uzito kwa mkono.
Wakalichukuwa wakalipitisha kwenye snanner machine yao ndogo iliyopo pale chumbani,
Nadhani hawakuona kitu.
Wakalichukuwa bag tena, wakalisimamisha likiwa tupu.
Bag lilianguka upande mmoja..
Walihangaika kama nusu saa hivi bila kujuwa bag lina kitu cha ziada ndani.,,huku mm nawaangalia kwa jicho la wizi nisigundulike.
Namlaani Sana mmoja wa Askari wale ,,ambaye alikuwa mweusi.
Jamaa aliongoza mashambulizi ya kukaguwa bag,,bila kuchoka.,jamaa ni kama alitaka kunitoa nishai.
Jamaa aling'ang'ania bag langu kama katangaziwa zawadi.
Hatimae jamaa akatamka humu kuna kitu ndani ya bag.
Wht is inside the bag?
Jamaa aliuliza..
Nikawajibu .
My bag is empty...there is nothing inside.
Jamaa wakaja na tools box DK 5 bag limechanwa lote.
Hatimae kibunda chote hadharani.
Pale pale jamaa wakanitia Pingu..
Whts that? Drugs?
Nikawajibu mm sijuwi chochote kuhusu hicho kitu..
Pale pale chumbani waliongezeka Askari wengine ikawa kama nipo kwenye maonyesho.
Wengine wakinichukuwa video kwa simu zao,,
Huyu kaongea hivi,,mara vile..mradi tu ndy nimeshakamatwa,nikawa kama kituko.
Askari walijiridhisha ni pesa cash euros 35000 ,+ wallet yng nilikuwa na euros 1700 zikachanganywa.
Whose money are these?
Nikawajibu pesa mm sizijuwi,,Hilo bag nimepewa na rafiki yng niweke nguo..
Kilichopo humo mm sikitambui.
Jamaa wakachek passport yangu,,muda na days nilizokaa Europe,.
Date of entry.
Akasema.
Do you deal with drugs?
Nikawajibu no?
Akasema inaonekana hapa europe
Una kama mwezi mmoja hivi.
How did you get this amount?
Twambiye nani kakupa hizi pesa,,au twambiye una deal na nani?
Nikawajibu na deal nn?
Tunajuwa wewe unaishi Africa,,hapa Paris unakuja kwa nani?
Twambiye ,,tunajuwa wewe pesa sio zako..
Walihitaji nionyeshe ushirikiano ili niwamalize wengine.
Bado nikakomaa hilo bag nimepewa na jamaa uswis niweke vitu tu,,nipeleke Africa.
If you deny this bag you will be in Trouble my friend.
Accept the bag then let the judge decide.
Judge will let u go..or pay the penalt.
Yule mkubwa wa kitengo alinambiya nisisumbuwe mahakama,,nikubali bag.
Still nikasema sijuwi chochote kuhusu bag.
Nikaandika maelezo,,then nikakabidhiwa kwa police,
Kituo kikuu cha police Paris.
Itaendelea..