Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Mwabukusi amesema huu mkataba haukuwa wa ghalfa, walikuwa nao wameuficha, na walivyoupeleka bungeni waliulizwa dharura imetoka wapi wakati wamekaa nao kwa miezi tisa na kusema kwamba yeye alitumia dakika tano tu kuutazama mkataba huo na kusema haufai hata kuwa toilet paper.
Akisema kuwa haamini kama mkataba huu ulifata mchakato wa kiserikali kwasababu ni mkataba wa hovyo kuliko wa Mangungo kuanzia kwenye utangulizi mpaka kwenye kiambata cha saini.
Mwabukusi akaongeza, Mangungo anasingiziwa sana, yeye hakuwa na ufahamu mkubwa kama walivyokuwa viongozi wa sasa, yeye alikuwa mtu wa kwanza kusaini mkataba na hakukuwa na ushahidi kwamba alikuwa na washauri waliofahamu lugha ya Kijerumani, lakini mzee Mangungo anafananishwa na viongozi wa sasa ambao waliambiwa hata kabla ya hawajaupitisha Bungeni kuwa haufai lakini wakufanya lolote kuzuia.
Mwabukusi ameyasema hayo katika mkutano unaofanyika Temeke kupinga mkataba wa Bandari leo tarehe 23/7/2023.