Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 112,552
- 205,014
Haya ndio yaliyojili Kwenye Mahakama kuu leo , Jaji Anataka kuendesha kesi kienyeji utadhani Katiba ni ya familia yake .
Lengo kuwafurahisha waliomtuma .
Hebu jionee mwenyewe .
======
Jopo la mawakili tisa likiongozwa na Wakili Mpale Mpoki limefika Mahakama Kuu, Dar es salaam, Kanda ya Ardhi na kukutana na kamati ya nidhamu ya mawakili kwa lengo la kuutetea uwakili wa Wakili Boniface Mwabukusi .
Wakili Mwabukusi amefikishwa mbele ya kamati hiyo baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumshitaki kwa kile kilichodaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Katika shauri hilo Mwanasheria Mkuu analalamika juu ya kauli alizozitoa Mabukusi akiongea na vyombo vya habari.
Moja ya kauli iliyotajwa katika malalamiko hayo ni maneno ya Mwabukusi kwamba, “Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hawajui walichopitisha Bungeni kwamba hata Chifu Mangungo anasingiziwa maana yeye alijua ni Mkataba.”
Mwanasheria Mkuu anaelezea kuwa Wakili Mwabukusi alitoa kauli ambazo ni za kichochezi, zisizo na staha na zisizozingatia taaluma ya uwakili.
Kwa mujibu wa Wakili Alphonce Lusako ambaye ni miongoni mwa wanajopo hilo la kumtetea Wakili Mwabukusi kilichowasukuma wao kuamua kumtetea wakili huyo ni kutaka kupambana na njama za kukandamiza mawakili wanaoikosoa serikali.
Credit: Watetezi TV