MWABUKUSI atoa neno juu ya Wajumbe Chipukizi CCM "Wametutawala wao wanataka na watoto wao watutawale"

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,864
Afla za uchaguzi wa tisa wa Chipukizi Taifa zilizofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, zimeibua maswali mengi baada ya watoto walioshinda vinyanganyiro hivyo kuwa watoto wa viongozi tu kwa asilimia kubwa, ikilinganishwa na idadi ya watoto walioko Tanzania.

Katika vinyanganyiro hivyo, Bryan Augustino Mahiga mtoto wa aliyekuwa waziri wa Mambo ya Nje, na baadae kuwa Waziri wa Katiba na sheria, Hayati Balozi Augustino Mahiga, amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya uendeshaji chipukizi CCM Taifa kutoka Tanzania bara, akiwalisha wenzake wa nane.

Isack Mwigulu Nchemba, mtoto wa mbunge wa jimbo la Iramba na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amechaguliwa kuwa Mjumbe baraza kuu la UVCCM Taifa kutoka Tanzania bara.

Simba Jerry Silaa, mtoto wa waziri wa Ardhi Jerry Silaa amechaguliwa kuwa Mjumbe kamati ya uendeshaji chipukizi CCM Taifa kutoka Tanzania bara akiwakilisha wenzake wa nane.

Qailah Nurdin Bilal ambaye ni mtoto wa msanii wa Bongofleva, Shetta (Baba Qailah) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chipukizi CCM Taifa.

Katika vinyanganyiro hivi, watoto wa vigogo ndio wameonekana kuteka nafasi hizi za ushindani. Jambo ambalo limepelekea Mwanasgeria nguli, Mwabukusi kuja na hoja za kusema.

"Wametutawala wao na Sasa wanataka na watoto wao watutawale"

Kiashiria kwamba hizi nafasi zimetolewa tu kwa watoto wa viongozi, wakati huko Tandahimba au Shitohole hakuna mtoto aliyepewa taarifa juu ya nafasi hizi ili naye ashiriki. Tizama clip hiyo Mwabukusi akitoa neno.


View: https://www.instagram.com/reel/C1HGhbyKKcI/?igsh=MzRlODBiNWFlZA==
 
TUnaishia kulalamika bila kuchukua hatua.
Mbona Wahindi hurithishana biashara?

Mwanasiasa kwa sehemu kubwa wanae wanaiishi siasa wapende wasipende hivyo ni rahisi mtoto kutamani kuwa kama mzazi au mzazi kutanani mwanae awe kama yeye ale kiulaini
 
Kulalamika haitoshi, wazazi wawekeze kwa watoto wao. Utalalamika mpaka lini na kinyanganyiro kiko wazi.
 
Back
Top Bottom