Maryam (Sombi Jr) aibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa tisa(9) wa Chipukizi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
MARYAM Sombi ambaye ni mdogo wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. Rehema Sombi, amechaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa kupitia Chipukizi.

Maryam (Sombi Jr) aliibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa tisa(9) wa Chipukizi uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, jana, Desemba 20, 2023 ambapo alichaguliwa kwa kura 284 sawa na asilimia 90.7 zilizopigwa na wajumbe katika Mkutano huo.

Akizungumza baada ya kupewa dhamana hiyo, Sombi Jr aliahidi utumishi uliotukuka akisema katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha anapigania maslahi ya watoto wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wananchi na Tanzania kwa ujumla.

Katika mkutano huo Qailah Nurdin Bilal ambaye ni mtoto wa msanii wa muziki wa Bongofleva, Shetta, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa.

Qailah aliibuka kidedea baada ya kupata kura 303 kati ya 402 zilizopigwa na wajumbe hivyo kuwashinda wenzake aliokuwa akigombea nao katika uchaguzi huo.
IMG-20231221-WA0005.jpg
 
Mungu wa rehema awalinde vijana wote wa Tanzania.

Awajazie busara na hekima.

Awaepushe na sumu zinazosambazwa na mahasimu na wakala wa mashetani waliomo humu Duniani na huko Mbiguni.

Amani iwatandae.
 
MARYAM Sombi ambaye ni mdogo wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg. Rehema Sombi, amechaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa kupitia Chipukizi.

Maryam (Sombi Jr) aliibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa tisa(9) wa Chipukizi uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, jana, Desemba 20, 2023 ambapo alichaguliwa kwa kura 284 sawa na asilimia 90.7 zilizopigwa na wajumbe katika Mkutano huo.

Akizungumza baada ya kupewa dhamana hiyo, Sombi Jr aliahidi utumishi uliotukuka akisema katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha anapigania maslahi ya watoto wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) wananchi na Tanzania kwa ujumla.

Katika mkutano huo Qailah Nurdin Bilal ambaye ni mtoto wa msanii wa muziki wa Bongofleva, Shetta, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa.

Qailah aliibuka kidedea baada ya kupata kura 303 kati ya 402 zilizopigwa na wajumbe hivyo kuwashinda wenzake aliokuwa akigombea nao katika uchaguzi huo.View attachment 2849110
Uharoooo tuuu
 
tuwaandae watoto wakuwe wakiwa na akili za kimapinduzipinduzi zitakazoleta matokeo chanya katika jamii ya Kitanzania.

Vijana watakaoukuwa na ujasiri wa kupigania maslahi ya Taifa na si maslahi binafsi na vikundi vyao, Vijana watakaokuwa tayari hata kuishi na kuingia msituni kwa ajili ya Taifa lao.
 
Back
Top Bottom