masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Sakata la Hospitali binafsi kuingia mgogoro na NHIF juu ya huduma itolewayo na NHIF kutokidhi gharama halisi ilinaendelea kurindima.
Kinachojitokeza ni kwamba srikali, hasa Wizara ya Afya inaonekana kulega ega katka sekta inyoisimamia.
Waziri wa Afya hatujamsikia akitoa neno katika swala hili. Wagonjwa watadhurika, na wengine kupoteza uhai, huku wavaa tai wakilumbana.
Umahiri wa kisiasa wa Ummy Mwalimu sasa ndio unatakiwa uonekane, kuwasaidia watanzania, hasa wale walio vitandani mahospitalini na wanaougua.