Mustakabali wa IPP Media baada ya Reginald Mengi kutuaga

Acheni kujadili mambo yasiyo wahusu kama huna mada ya maana unakaa kimya..!
 
Nashauri IPP Media iendelee kuwa chini ya usimamizi wa Joyce Mhaville naamini amekuwa akiipatia na ataipatia.

Kwa upande wa kusimamia empire ya IPP group of companies nadhani mwanae wa kike Regina anaweza kusimamia hii empire.

IPP Companies ni kampuni ya kizawa ambayo imewanufaisha sana watanzania...hatutamani kusikia inadorora baada ya Mzee wetu kutangulia.
Hivi unafikiri Mengi ni mjinga kwamba hakutengeneza Channel ya Makampuni yake kusimama imara hata kama siku yeye kafariki?
 
Mengi is a more civilized person na ndiyo maana amefika hapa. Sidhani kama bado alikuwa na mawazo ya miaka ya 1980
hakuna mchaga anaeacha mali kwa mtoto wa kike. mtoto wa kike anaolewa na mpaka jina la ukoo anabadilisha na kutumia la mumewe, kwa hiyo automatical mali zinakuwa chini ya mume wake
 
Kwa wenye hekima sio mambo ya kujadili kwa sasa haya. ni vyema tujikite kwa maombolezo na kumuhifadhi mzee wetu ktk nyumba ya milele badala ya kuongelea mambo ambayo hata kwa wengine hayana faida!
 
Anza kwa kutaja kampuni ambazo zilikuwa zinajiendesha(corporate) alafu zikafa au kupungua ufanisi baada ya mmiliki kufa kabla ya kuuliza hilo swali lako. Labda tu nikwambie unachopaswa kujua ni kwamba IPP ndo kampuni ya kwanza kuwapo ambayo mmliki wake amefariki na kuiacha chini ya kizazi kingine baada yake. Hatuna mifano mingine kwa sababu miaka ya 85 kurudi nyuma hakuna mtu aliruhusiwa kumiliki biashara kubwa isipokuwa serikali.

Mengi ni mtu smart, alishatengeneza mfumo wa kutenga umiliki na utendaji wa kampuni.
Tatizo waswahili wengi tunachanganya ulimiki na utendaji na pia tunaweka kujuana kwenye utendaji kuliko weledi. Hapo lazima kampuni ife
Nitajie kampuni iliyoanzishwa na mswahili (awe mchaga au kabila lolote jingine ngozi nyeusi) mwenyewe akatwaliwa na imebaki ina-operate at least kwa kiwango alichokiacha mwanzilishi wake.
 
Nakuuliza mkuu hapa nchini kuna kampuni gani kubwa inayolingana na IPP ambayo inamilikwa na mswahili na bosi wake akafariki?
Umeuliza kitaalamu sana. Watu wengi wanachanganya proprietorships , partnership na corportion wakati hizi vitu ni tofauti.
 
Anza kwa kutaja kampuni ambazo zilikuwa zinajiendesha(corporate) alafu zikafa au kupungua ufanisi baada ya mmiliki kufa kabla ya kuuliza hilo swali lako. Labda tu nikwambie unachopaswa kujua ni kwamba IPP ndo kampuni ya kwanza kuwapo ambayo mmliki wake amefariki na kuiacha chini ya kizazi kingine baada yake. Hatuna mifano mingine kwa sababu miaka ya 85 kurudi nyuma hakuna mtu aliruhusiwa kumiliki biashara kubwa isipokuwa serikali.

Mengi ni mtu smart, alishatengeneza mfumo wa kutenga umiliki na utendaji wa kampuni.
Tatizo waswahili wengi tunachanganya ulimiki na utendaji na pia tunaweka kujuana kwenye utendaji kuliko weledi. Hapo lazima kampuni ife

Nakutajia zifuatazo; Scandinavia Express; Bobby Soap Industries, Ladwa, niendelee? Sasa wewe nitajie moja tu ambayo bado inafanya kazi baada ya muasisi wake kufariki. Unaemsema hata akiwa hai kuna kampuni zake nyingi tu zinapumlia mashine!
 
Hiyo ni kawaida hata akina Zuckerberg wana biashara ambazo zimekufa baada ya miaka 5. Kwa hiyo hilo haliusiani na maisha ya IPP tu
Nakutajia zifuatazo; Scandinavia Express; Bobby Soap Industries, Ladwa, niendelee? Sasa wewe nitajie moja tu ambayo bado inafanya kazi baada ya muasisi wake kufariki. Unaemsema hata akiwa hai kuna kampuni zake nyingi tu zinapumlia mashine!
 
Nakutajia zifuatazo; Scandinavia Express; Bobby Soap Industries, Ladwa, niendelee? Sasa wewe nitajie moja tu ambayo bado inafanya kazi baada ya muasisi wake kufariki. Unaemsema hata akiwa hai kuna kampuni zake nyingi tu zinapumlia mashine!
Unapaswa kujua hizo biashara zilikuwa katika level zipi. Je zilikuwa corporation? Maana kampuni ambayo ni corporation inaendelea kuishi hata mmiliki akifa tafauti na proprietorship au partnership
 
Kampuni za Ngorika (Bus na hotel) bado zipo baada ya mwenyewe kufa...
Nitajie kampuni iliyoanzishwa na mswahili (awe mchaga au kabila lolote jingine ngozi nyeusi) mwenyewe akatwaliwa na imebaki ina-operate at least kwa kiwango alichokiacha mwanzilishi wake.
 
Tanzania biashara zimeanza kufanywa baada ya raisi Nyerere kuachia madaraka. Kabla ya hapo tulikuwa chini ya ujamaa. Sasa miaka 100 inatimiaje kweli?
Biashara zimeanza Tanzania baada ya Nyerere whaaaaat?
Sisi tuna biasahara tangu mwaka 1952 na mpaka leo wajukuu wanaiendeleza na biashara zilikuwepo miaka na miaka
Sasa hizi biashara unazisema sijui ni za madawa ya kulevya?
 
Ninachojua under socialism during the reign of Nyerere, only the government was doing mojority of the business. Huo ndo ujamaa. Na hata maduka ya mangi yalikuwa ya serikali by that time

Sio kweli mkuu mimi nina ushuhuda hata kabla ya Uhuru biashara zilikuwepo ingawa wazawa walikuwa wachache sana na suppliers wakubwa kwenye kambi za majeshi na hospitals walikuwa foreigners wengi wakiwa na passports za Uingereza
 
Mara ya mwisho umeziona barabarani basi za Ngorika lini? Watoto walishagawana assets kitambo!
Mwezi uliopita, watoto wake wana mabasi yao na ile kampuni mama ipo.. Hotel ya Kindoroko pia bado iko poa tuu
 
Sio kweli mkuu mimi nina ushuhuda hata kabla ya Uhuru biashara zilikuwepo ingawa wazawa walikuwa wachache sana na suppliers wakubwa kwenye kambi za majeshi na hospitals walikuwa foreigners wengi wakiwa na passports za Uingereza
Kabla ya uhuru biashara zilikuwepo ila siyo kipindi cha ujamaa.
 
Back
Top Bottom