TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,764
- 21,237
Mzee RAO anamuangamiza kiuchumi Rais Ruto na makamu wake Gachagua kupitia maandamano.
Meli ya kitalii iitwayo MV Seabourn Sojourn, iliyopo njiani kwenda nchi mbalimbali duniani, ambapo kwa afrika mashariki ilikuwa isimame kwa siku 6 kwenye bandari ya Mombasa, sasa imebadiri uelekeo hadi Tanzania kutokana na maandamano ya upinzani yanayoendelea nchini Kenya.
Meli hiyo inayotoka Mahe, nchini Shelisheli, ina watalii 800 sasa itatia nanga kwenye visiwa vya Zanzibar na Dar es Salaam kwa siku sita kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.
Meli hiyo ilianza safari yake huko Miami Florida, mnamo Januari mwaka huu, ambapo safari yao inategemewa itakamilika Mei 27 huko katiak jiji la Barcelona, Uhispania.
Awali Kenya ilikuwa kwenye ratiba ya safari ya Mv. Seabourn Sojourn ambapo ilitegemewa kutia nanga katika bandari ya Mombasa.
Kufuatia hali hiyo nchi hiyo imepata athari kwenye sekta ya utalii huku wadadisi wakisema taifa hilo la Afrika Mashariki linapoteza mamilioni ya dola za kimarekani.
“Tumepoteza pesa nyingi sana, kutokana na matumizi ya awali, kila abiria hutumia angalau usd 200 kwa siku, kwa siku tatu hizo ni usd 600, tumepoteza usd 800,000, tukichukulia kila mmoja angetumia kiasi hicho,” kauli ya Bw Masemo, kutoka nchini Kenya.
Credit: The Citizens