Mambo sita yanayoifanya Tanzania kuipiku Kenya kiuchumi na nchi nyingine hadi 2028.

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
Kwa mujibu wa takwimu mpya za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), pato la Taifa la Tanzania limeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni $85.42 (Shilingi 200 trilioni za Tanzania) kwa mwaka huu wa 2023.

Hiyo inaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi sita Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi. Imeshazipiku nchi kama Ghana na Ivory Coast zilizokua juu yake.

IMF inasema kufikia mwaka 2028 uchumi wa taifa hili la Afrika Mashariki utazidi kukua na utafikia dola $136 billioni (Shilingi 318.8 trilioni za Tanzania) na pato la mtu mmoja mmoja litakua hadi kufikia dola 1,860 (Shilingi 4.3milioni) kutoka dola $1,350 za sasa (Sawa na 3.15milioni za Tanzania).

Kwa tathimini ya ripoti hiyo na kwa makadirio yaliyopo, si muda mrefu Tanzania huenda ikaipiku Kenya kiuchumi, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiongoza Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa IMF uchumi wa Kenya kwa mwaka 2023 umefikia dola $118.1billioni.


Wachumi wanabashiri pia Tanzania itaziacha kwa mbali pia nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na nchi zingine za ukanda huu. Huku ikizifukuzia kwa karibu nchi zinazofanya vizuri za Kusini mwa janga la Sahara kama Ethiopia, Afrika Kusini na Nigeria yenye uchumi mkubwa Afrika unaofikia dola $506.6 billioni.

Nini siri ya mafanikio ya Tanzania kiuchumi?
Kwa muongo mmoja uliopita, Tanzania kasi ya ukuaji wa kiuchumi wa nchi hiyo umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka. Pamoja na kuzuka kwa ugonjwa wa Covid-19 na vita vya Ukraine, uchumi wa nchi hiyo umepaa kutoka dola $69.9 bilioni mpaka dola $85.42 bilioni.

Siri kubwa katika mafanikio haya kwa muda mfupi huu moja kubwa ni uwekezaji mkubwa kwenye biashara unaosukumwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea wawekezaji wengi toka nje, ameruhusu uwekezaji mkubwa na mdogo, ameingiza matrilioni ya pesa toka nje kwa njia ya misaada na mikopo. Pesa zinazosaidia kuongeza mzunguko na kuchagiza shughuli za kiuchumi.


Mambo 6 yatakayofanya Tanzania kuipiku Kenya na nchi zingine kiuchumi.

Ripoti ya IMF inagusa makadirio katika kipindi cha miaka 10 kati ya mwaka 2018 mpaka 2028, kipindi ambacho kwa tathimini ya kiuchumi imeibeba zaidi Tanzania kuliko Kenya na nchi zingine zenye rasilimali nyingi kama DRC, Ivory Coast, Uganda na Ghana.

Haitashangaza kuiona ikiipiku Kenya katika kipindi hicho cha miaka 10. Haitashangaza kuona pia ikiipiku Angola yenye uchumi unaofikia dola $117.8 bilioni au hata Ethiopia yenye uchumi wa dola $156 bilioni.

IMF imezingatia masuala kadhaa ambayo pia uchambuzi wa kiuchumi unayabainisha kama mambo muhimu ambayo yanaipa Tanzania nafasi kubwa ya kuipiku Kenya kiuchumi inayoongoza Afrika Mashariki na ikitarajiwa pia kuipiku nchi kama Angola inayoshika nafasi ya Tano Afrika, kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

1: Uwekezaji na Sekta binafsi

Katika kipindi cha miaka 2 iliyopita Tanzania imejenga mahusiano muhimu ya kidiplomasia na mataifa ya kigeni kuruhusu wageni na biashara za kigeni kufanyika zaidi na kwa njia nyepesi. Uwekezaji umeomgezeka na ameithaminisha sekta binafsi.
Hili halikuonekana kati ya mwaka 2010 na 2021 wakati wa utawala wa Rais John Magufuli ambaye hakuwahi kufanya ziara yeyote ya nje ya bara la Afrika kwa miaka zaidi ya mitano ya utawala wake.

Samia alikwenda Ufaransa, nchi yenye pato la taifa linalokadiriwa kuwa ya dola za Kimarekani $2.6 Trilioni na kusaini mikataba 6 muhimu ukiwemo wa Euro 178 milioni za kuendeleza mradi wa ujenzi wa barabara za mwendokasi (BRT), akaenda Ubelgiji na akaenda Marekani kukutana na makamu wa rais Kamala Harris ambaye aliitembelea pia Tanzania na kuhaidi msaada wa dola milioni 560 mwaka 2024.

Ukiacha IMF yenyewe, Benki ya dunia imeitengea Tanzania dola za kimarekani bilioni 2.1 kati ya 2022- 2025.
‘Tanzania inapoingiza kwenye mzunguko wake wa fedha nyingi za kigeni kama hizi hasa za msaada ama mikopo yenye masharti nafuu, ni kuchochea uchumi, ni kuchagiza uchumi,na hilo linafanyika sana katika utawala wa sasa’, anasema Masaninga.

2: Bandari


Bandari hii mojawapo ya lango la kuu la kibiashara, ambapo asilimia 95 ya biashara ya kimataifa ya Tanzania inahudumiwa na Bandari hii. Inauwezo wa kuhudumia tani za metriki milioni 14 za shehena kavu na tani milioni 6.0 za vimiminika. Ukweli bandari hii ni silaha muhimu ya uchumi kwa Tanzania.

Ukiacha bandari ya mpya ya Bagamoyo iliyo katika hatua ya ujenzi, bandari ya Tanga na Mtwara, bandari yake ya Dar es Salaam inafaida kubwa ya kijiografia, inayotegemewa na nchi karibu 6 za Afrika.

Kwa ripoti za hivi karibuni usafirishaji wa mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam imeongezeka kwa 21% wakati bandari ya Mombasa, Kenya umeshuka kwa 6.2%. Uganda ambaye ni moja ya nchi zinazotumia sana bandari ya Mombasa, wafanyabiashara wake wengi wameanza kutumia bandari ya Dar es Salaam. Maboresho ya bandari hii itaendelea kuitishia ile ya Kenya kwenye mchango wake kiuchumi.


3: Madini adimu na ya kimkakati

Wiki hii, Tanzania imesaini mikataba na kampuni tatu za ubia kutoka Australia kwa ajili uwekezaji kwenye uchimbaji wa madini adimu kwenye mikoa ya Morogoro, Lindi na Songwe, mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani 667 milioni kufuatia utafiti ulioanza miaka zaidi ya 20 iliyopita.

‘Nimearifiwa kutokana na utafiti huo hadi sasa kuna tani milioni 67 zenye wastani wa asilimia 5.4 ya madini ya Kinywe yaliyogundulika katika kijiji cha Chilalo ambayo yatachimbwa kwa miaka 18.

‘Hili ni eneo lingine ambalo Tanzania itakwenda kufanya vizuri na kimapato kuliko Kenya’, anasema Dokta Barnos Willium, mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika, Moshi.

Mchango wa Sekta ya madini nchini Tanzania kwa sasa kwenye pato la taifa ni 9.7% nchi hiyo ikilenga kuliongeza mpaka 10% ifikapo 2025.

4: Gesi asilia, Bwawa la Nyerere na Reli ya kisasa (SGR).

Achilia mbali uwepo wa gesi wenye ujazo wa futi zafi ya trilioni 60, Kitakachoibeba Tanzania katika miaka 10ijayo ni reli ya kisasa inayojengwa kwa awamu kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza na kigoma. hiyo kuunganishwa na bandari ya Dar es Salaam inayohudumia nchi jirani zisizo na bandari kama vile Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda na Zimbabwe.

‘Kama unataka kufanikiwa kiuchumi ni kuwa na miundo mbinu thabiti inayounganisha kila sehemu, hasa sehemu za uchumi chochezi, hili litaipaisha Tanzania zaidi kibiashara na cnhi jirani’, Mchumi Willium.

Mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambalo litakuwa moja ya mabwawa makubwa duniani, litazalisha megawati 2,115 za umeme, ambao mbali na kusaidia viwanda na kuuzwa nje, pia utatumiwa kuendeshea mitambo ya SGR.

5: Kilimo cha Mashamba makubwa ya Pamoja

Machi 20, 2023 Rais wa Tanzania Samia Suluhu alizindua kilimo cha mashamba makubwa ya pamoja (Block Farming) chini ya mpango wa Building a Better Tomorrow Youth Initiative for Agribusiness Program (BBT-YIA).

Mpango huu wa miaka 8 utakuza sekta ya kilimo mpaka asilimia 30 ifikapo mwaka 2030.
‘Huwezi kuwekeza dola $148mil kwenye mpango usio na mchango kwa uchumi, Kenya wanafanya lakini nimeuona mpango huu utaleta mapinduzi makubwa kwa namna ulivyoandaliwa’, anasema Masaninga

6: Amani na Utulivu
Masuala yote matano niliyoyataja, lakini hili la amani na Utulivu ni la kipekee kabisa na kinaitofautisha Tanzania na nchi zingine shindani kiuchumi hasa Kenya.
Kwa sasa Kenya inapitia kipindi kingine cha wasiwasi kiuchumi hasa baada ya kiongozi wa upinzani, Raila Odinga kuitisha maandamano nchi nzima pamoja na mambo mengine wanataka serikali ishughulikie suala la ugumu wa maisha.

Kawaida ghasia za maandamano zinazuia shughuli nyingi za kiuchumi. Unaonekana kuwapo kwa mvutano mkubwa wa kisiasa kati ya Serikali ya William Ruto na upinzani nchini Kenya. Kama wapinzani wataendelea na maandamano itafifisha uchumi wa taifa hilo ambalo mara kwa mara limekuwa likikumbwa na ghasia za uchaguzi ama za baada ya uchaguzi.
 
Kwanini mnapendaga kuyumbisha diplomasia ya nchi na majirani? Huo uchonganishi wa nini? Hizo nchi mnazotaja watu wake wake pia wanapita humu.

Kama nchi ikiwa tuna mipango yetu kiuchumi si tutekeleze kimyakimya?! Yanni kuweka hadharani? Halafu haya mambo ya kushindana na Kenya ya kazi gani? Badala ya kuangalia Dunia, Sisi tunahangaika na jirani. Kuwa na akili ndogo kama hivi ni hatari sana kwa taifa.

JF admini threads kama futulieni mbali. Hazina afya kwa diplomasia ya nchi hata kidogo.
 
Kwanini mnapendaga kuyumbisha diplomasia ya nchi na majirani? Huo uchonganishi wa nini? Hizo nchi mnazotaja watu wake wake pia wanapita humu.

Kama nchi ikiwa tuna mipango yetu kiuchumi si tutekeleze kimyakimya?! Yanni kuweka hadharani? Halafu haya mambo ya kushindana na Kenya ya kazi gani? Badala ya kuangalia Dunia, Sisi tunahangaika na jirani. Kuwa na akili ndogo kama hivi ni hatari sana kwa taifa.

JF admini threads kama futulieni mbali. Hazina afya kwa diplomasia ya nchi hata kidogo.
Umenena vema.

Kenya, na nchi zote za jumuia ya Afrika Mashariki, siyo washindani wetu, siyo washindani wa Tanzania. Kenya na nchi nyingine za EAC zinatakiwa kuwa partners in our economy.
 
Umenena vema.

Kenya, na nchi zote za jumuia ya Afrika Mashariki, siyo washindani wetu, siyo washindani wa Tanzania. Kenya na nchi nyingine za EAC zinatakiwa kuwa partners in our economy.
HeeeeeHeeee!
"...partners in our economy"?

Kuna nyakati huwa unashangaza sana na 'thought process' yako inavyofanya kazi!
 
5. Magufuli kukataa lockdown

Kuna watu roho zinawauma sana wakiona mama anavyopaisha uchumi wa Tanzania!! Wanatamani kama wangesikia Tanzania imeanza kudorora inakimbilia kuwa ya mwisho kwa umaskini barani Africa!!

Mama la Mama anapaisha uchumi watu wamebakia wamefunga domo zao🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom