Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera

Bendera ya Bati

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
279
363
Nakumbuka, ilikuwa katikati ya miaka ya 90 nikiwa nasoma katika moja ya shule za sekondari katika moja ya wilaya zilizopakana na nchi za Rwanda na Burundi.

Ikumbukwe ni katika miaka hiyo yalikuwa yameanza mapigano ya kikabila yaliyokuwa yamezuka nchini Rwanda Kati ya Watutsi na Wahutu nchini humo yaliyoibuka tu baada ya kuuwawa kwa aliyekuwa raisi wa nchi hiyo Juvenary Habyarimana.

Twende pamoja...

Nakumbuka, ilikuwa saa 2:20 Usiku nilipokuwa natia timu pale katika bandari ya Mwanza ili nikate ticket ya meli MV Victoria kwa ajiri ya Safari ya kuelekea mkoani Kagera ambapo ningefika siku uliyokuwa inafuata kwa kweli simkumbuki siku hiyo ilikuwa siku gani ingawaje nakumbuka kipindi kile ratiba za meli Mwz to Bkb ilikuwa Kati ya J'nne, Alhamis na J'mosi.

Baada ya kushuka kwenye taxi nilielekea moja kwa maja mpaka lilipo gate la kuingilia na kuelekea kwenye moja ya mistari mirefu ya abilia waliokuwa kwenye foleni ya ukataji tiketi nami nikajipanga. Haikutumia muda mrefu nilikuwa na tiketi yangu mkononi huku nikielekea ulipo mlango wa kuingilia kutokana na daraja nililokata tiketi ambalo ilikuwa third class.

Mzee wangu alikuwa anapenda nisafiri on first class na alikuwa ananipa bajeti ya daraja hilo, Ila Mimi nilikuwa naona haina maana kwangu kwenda kujifungia kwenye hivyo vyumba vya kulala kwasababu, kwanza sikuwa na imani kusafiri majini nikiwa nimeupiga usingizi, nikiwa nimelala kabisa nimejinyoosha kitandani, kwa maana wakati wowote nilihofia kujikuta kwenye sakafu ya mchanga ziwani in case inatokea ajali nikiwa nimeupiga usingizi(it was my all days alert) nilipokuwa nikipanda meli. (Machale yangu hayakuwa mbali na nilichokifikilia maana ni nyakati hizohizo ilipotokea ajali mbaya ya meli ya MV BKB na kuua Mamia ya watu) pia ilikuwa ni njia mojawapo ya kujiongezea akiba kwenye pocket money ili ninapokuwa shule niwe nachekelea tu kutokana nakuwa na akiba yakutosha, lakini jambo la tatu, nilipenda sana kukaa daraja la tatu 'changanyikeni' maana kule kuna watu wa kila aina na story za hapa na pale ni nyingi lakini mwisho nilikuwa napenda sana mademu i see.

Safari ilianza saa 4 za usiku kuelekea Bk na kama kawaida story kwa wingi zilikuwa zikipita hapa na pale lakini muda huo mada nyingi zilizokuwa zinaongelewa karibu kila nilipokuwa navamia kusikiliza hazikuwa zikini- concur mpaka nilipokuja kujikuta navamia kikundi cha vijana wa rika langu ambapo nilikuja kutambua nao walikuwa wanafunzi wanarejea shuleni Kama nilivyokuwa Mimi. Tulipiga story nyingi Sana mpaka tunafika bila kulala usingizi. Na tulianza Urafiki ambao umedumu hata leo.

Alfajiri saa 12 tulikuwa tumefika bandari ya Bkb na kila mtu alikuwa na harakati zake za kushuka kuelekea njia yake. Mimi na washkaji zangu tulichukua taxi mpaka stand kisha wao wakaendelea na Safari yao kuelekea shule zao zilipo.

Nilichukua begi langu kubwa la mgongoni aina ya volcano(kipindi kile yalikuwa mabegi yako kwa fashion sana) Yalikuwa mabegi ya kijanja Sana wakati huo, unyama ulikuwa mwingi Sana those old days. Kwa msaada wa vijana wa Sasa Kama mnawaona watalii zile begi wanabeba mgongoni kupanda Mnt. Kili, sasa hata zile begi zilifanana hivyo, make zilikuwa zinabeba vitu vingi wakti mmoja. Mkononi nilibeba kibegi flani cheusi hivi simple , hicho nilikuwa nimepakia mazaga kibao ya kutumia shule. Kiujumla niliyapenda sana mabegi Yale. Cha kusikitisha hakuna nilichofika nacho shule.

Kwa kuwa ilikuwa bado asubuhi sana na kulikuwa na kibaridi kilichochagizwa na ukungu uliotanda kutokea mwambao wa ziwa Victoria, niliamua kupiga hatua kadhaa kutoka eneo nililokuwepo na kuelekea moja ya jengo kulikuwa karibu kabisa na maeneo hayo na baada ya kufika kwenye kibalaza, nilishusha begi langu chini Kisha nikakaa kwenye kijikuta cha balaza ili nitoe 'pullover

Muendelezo soma
Sitasahau nilivyonusurika kuchukuliwa mateka na majambazi mkoani Kagera
 
Nakumbuka, ilikuwa katikati ya miaka ya 90 nikiwa nasoma katika moja ya shule za sekondari katika moja ya wilaya zilizopakana na nchi za Rwanda na Burundi.

atua kadhaa kutoka eneo nililokuwepo na kuelekea moja ya jengo kulikuwa karibu kabisa na maeneo hayo na baada ya kufika kwenye kibalaza, nilishusha begi langu chini Kisha nikakaa kwenye kijikuta cha balaza ili nitoe 'pullover
Miaka hiyo kutekana nje nje,pori la kimisi,nk kuifikia ngara su biharamo ilikuwa mtihani,majambazi yana AK47
 
Nakumbuka, ilikuwa katikati ya miaka ya 90 nikiwa nasoma katika moja ya shule za sekondari katika moja ya wilaya zilizopakana na nchi za Rwanda na Burundi.

Ikumbukwe ni katika miaka hiyo yalikuwa yameanza mapigano ya kikabila yaliyokuwa yamezuka nchini Rwanda Kati ya Whaa kutoka eneo nililokuwepo na kuelekea moja ya jengo kulikuwa karibu kabisa na maeneo hayo na baada ya kufika kwenye kibalaza, nilishusha begi langu chini Kisha nikakaa kwenye kijikuta cha balaza ili nitoe 'pullover
Oyaa
Hance Mtanashati njoo
Chai hii hapa
 
Back
Top Bottom